• ePaper
Thursday, June 25, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

YANGA YAKUBALI YAISHE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 17, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
YANGA YAKUBALI YAISHE
0
SHARES
9
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

BAADA ya  Yanga kushindwa kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika,uongozi wa klabu hiyo umesema umejifunza mambo mengi katika michuano  hiyo.

Yanga ilishinda mabao 3-0 dhidi ya JS Kabylie mchezo wa hatua ya makundi uliofanyika katika Uwanja wa New Amaan Complex, visiwaani Zanzibar.

Akizungumza baada ya kumalizika mchezo huo, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe alisema wataenda kupiga hesabu zao vizuri ili msimu ujao isitokee tena.

“Hii hali inaumiza kabisa asikwambie mtu unashinda mabao 3-0, halafu unasubiri matokeo ya timu nyingine kiukweli unatamani kulia kutokana na aina ya matokeo hayo,” alisema.

Ofisa huyo alisema mbali ya matokeo hayo, amekiri wachezaji wao walipambana na kuonesha kiwango bora ambacho kimewavutia mashabiki wa timu hiyo.

“Tumetoa jasho letu katika kundi ambalo lilionekana ni kundi la kifo, tunashukuru Mungu tumekusanya pointi nane lakini haikuwa bahati tumeshindwa kupata pointi nyingi za kuendelea robo fainali.

“Nawapongeza wachezaji wetu wamejituma sana siku ya mchezo, wamejitoa sana wamefanya kile ambacho wana Yanga walikitaka kwa kufunga mabao matatu, lakini mabao hayo hayatoshi maana mechi nyingine  timu zilitoka sare,” alisema.

Ofisa  huyo alisema wacezaji wao walipambana sana na kuonyesha kiwango kikubwa.

“Hizi pointi tulizovuna michuano hii tunajiona kabisa msimu ujao tuna uwezo wa kufika mbali zaidi, pia kila shabiki wa Yanga ameondoka uwanjani akiwa na furaha kutokana na kiwango bora ambacho wachezaji walionyesha,” alisema.

Ofisa huyo alisema hasira zao za kushindwa kutinga robo fainali wanaenda kuzimalizia katika Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho (FA).

“Mechi ya Kariakoo dabi ambayo itafanyika Machi Mosi, mwaka huu itafanyika dimba la New Amaan Complex hivyo tutakutana hapa siku hiyo kutakuwa na mambo mengi ambayo watu wataona hasira zetu,” alisema.

Previous Post

MAKONDA AJITOSA MABADILIKO SIMBA

Next Post

WASHINDI ‘CHANJA KIJANJA’ WAPATIKANA

Next Post
WASHINDI ‘CHANJA KIJANJA’ WAPATIKANA

WASHINDI 'CHANJA KIJANJA' WAPATIKANA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. YONAZI APOKEA TAARIFA AFUA ZA UKIMWI PWANI

DK. YONAZI APOKEA TAARIFA AFUA ZA UKIMWI PWANI

1 month ago
WASIRA : TUSAHAU MCHAKATO WA UCHAGUZI, SASA TUUNGANE KUSAKA DOLA

WASIRA : TUSAHAU MCHAKATO WA UCHAGUZI, SASA TUUNGANE KUSAKA DOLA

10 months ago

Popular News

  • SERIKALI YAZITAKA TAASISI ZOTE KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL-NINO

    SERIKALI YAZITAKA TAASISI ZOTE KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL-NINO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SAMAMBA AWAFUNDA WAKAGUZI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RUNGU ZITO KUWASHUKIA WAWEKEZAJI ‘JANJAJANJA’

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, SIMBA KAZI KAZI UBINGWA LIGI KUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, AZAM FC HAIJAISHA HADI IISHE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?