• ePaper
Sunday, May 31, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

PBPA YAAGIZWA KUHARAKISHA UPOKEAJI NA USAZAMBAZAJI WA MAFUTA NCHINI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 26, 2026
in Habari, Kitaifa
0
PBPA YAAGIZWA KUHARAKISHA UPOKEAJI NA USAZAMBAZAJI WA MAFUTA NCHINI
0
SHARES
11
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, ameutaka Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) kuhakikisha kuwa maghala yote makubwa ya usambazaji wa mafuta yanapata bidhaa hiyo kwa wakati, ili kuimarisha upatikanaji wake nchini.

Hayo yamesemwa  jijini Dar es Salaam wakati wa kikao chake na viongozi wa PBPA, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na kampuni ya TIPER kwa lengo la kujadili hali ya upokeaji wa mafuta yanayoingia nchini.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Ndejembi ameielekeza PBPA kuweka mfumo madhubuti wa upangaji wa ratiba ya ushushaji wa mafuta (sequencing) ili kuhakikisha maghala yote makubwa yanayohusika na usambazaji yanapata mafuta kwa usawa na kwa wakati.

Amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza changamoto za upatikanaji wa mafuta katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Aidha, ameeleza kuwa Serikali imekubaliana kuharakisha ushushaji wa meli za mafuta zinazoingia nchini, hususan kwa ajili ya matumizi ya ndani, ili kuhakikisha upatikanaji wa mafuta unaendelea kuwa wa uhakika na salama.

Ameongeza kuwa Serikali imefanya mazungumzo na Tanzania International Petroleum Reserves Limited (TIPER), na kuelekeza kuwepo kwa utaratibu mzuri wa kupanga ushushaji wa mafuta ili wasambazaji wote wapate huduma kwa usawa.

Waziri Ndejembi amewaasa Watanzania kutokuwa na taharuki kuhusu upatikanaji wa mafuta, akisisitiza kuwa nchi ina akiba ya kutosha.

Vilevile, Ndejembi,  ameitaka EWURA kuhakikisha kuwa mafuta yote yanayotoka kwenye maghala yanafika kwa walengwa na kutumika ipasavyo, huku vituo vya mafuta vikihimizwa kuuza bidhaa kulingana na mahitaji halisi ya soko.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi Asilia, Dkt. James Mataragio,  Mtendaji Mkuu wa PBPA, Erasto Simon, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dk. James Andilile pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TIPER,  Mohamed Mohamed na wataalam mbalimbali wa sekta ya mafuta.

Previous Post

DK. MWIGULU: TUENDELEE KUMUOMBEA LUKUVI

Next Post

MRADI WA BILIONI 18.9/- BUKOBA WAMPA SIFA RAIS DK. SAMIA

Next Post
MRADI WA BILIONI 18.9/- BUKOBA WAMPA SIFA RAIS DK. SAMIA

MRADI WA BILIONI 18.9/- BUKOBA WAMPA SIFA RAIS DK. SAMIA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MPINZANI WA MWAKINYO HADHARANI

MPINZANI WA MWAKINYO HADHARANI

6 months ago
‘HAPPY BIRTHDAY’ RAIS DK. SAMIA, KINARA WA UTUNZAJI MAZINGIRA

‘HAPPY BIRTHDAY’ RAIS DK. SAMIA, KINARA WA UTUNZAJI MAZINGIRA

4 months ago

Popular News

  • SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?