• ePaper
Wednesday, April 22, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MWIGULU AWAZUIA MAWAZIRI TANGA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 18, 2026
in Habari, Kitaifa
0
MWIGULU AWAZUIA MAWAZIRI TANGA
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI MAALUMU

WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, amewaagiza baadhi ya mawaziri alioambatana nao, wabaki mkoani Tanga kufuatilia masuala yaliyoibuliwa na wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.

Masuala hayo, yalitokana na hoja zilizoibuliwa katika mikutano ya hadhara na wabunge wa mkoa wa Tanga na wananchi mbalimbali katika sekta za ardhi, mifugo, kilimo, maji, elimu na barabara.

Alitoa agizo hilo, akizungumza na wakazi wa Soni na Bumbuli katika mkutano wa hadhara uliofanyika stendi ya Soni, wilayani Lushoto, Mkoa wa Tanga.

Mapema, akijibu hoja kuhusu ubovu wa barabara wilayani Lushoto, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, alisema Rais Samia Suluhu Hassan, ametoa kibali cha kuanza ujenzi wa pande mbili barabara ya Soni – Bumbuli- Dindira hadi Old Korogwe.

“Barabara hii ilishatangazwa na sasa tunakamilisha taratibu za wakandarasi. Zikiwa tayari, mmoja ataanzia Soni kwa kujenga kilometa 22 na mwingine ataanzia Old Korogwe (KwaMeta hadi Kwa Shemsi) kwa kujenga kilometa 9.5,” alisema.

Alisema barabara ya sasa ya kutoka Mombo – Soni hadi Lushoto yenye urefu wa kilometa 32, imefanyiwa usanifu na inatafutiwa fedha ifanyiwe upanuzi.

Naye Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde, alisema Msajili wa Hazina, anamalizia uhakiki wa madeni ya zamani ya wakulima wa chai waliokuwa wanadai malipo katika kiwanda cha chai cha Mponde na kuongeza kuwa katika kipindi cha hivi karibuni hakuna madeni yoyote yaliyolimbikizwa.

Alisema kiwanda hicho ambacho kinahudumia Halmashauri mbili za Bumbuli na Korogwe, kinafanyiwa mpango wa kupata ‘line’ nyingine ya uzalishaji ili kupunguza mlundikano wa majani ya chai yaliyovunwa.

Alisema Bodi ya Chai imenunua kiwanda kingine Korogwe ambacho kinatarajiwa kuanza kazi kabla ya Juni, mwaka huu kisaidie kupunguza mzigo unaoenda kiwanda cha Mponde.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alikagua na kuzindua shule mpya ya sekondari ya amali ya Majulai iliyopo katika Kijiji cha Majulai, Kata ya Mwangoi, Tarafa ya Mlalo wilayani Lushoto.

Shule hiyo ambayo imejengwa kupitia mradi wa SEQUIP, tayari imesajiliwa, ina walimu sita na wanafunzi 89 ambao walianza masomo Januari 13, mwaka huu.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa shule hiyo, Mkuu wa shule ya Sekondari Shita, ambayo ni shule mama, Mwalimu Ramadhani Mohammed, alisema mradi huo ambao umegharimu sh. milioni 584.28, ulianza kutekelezwa Oktoba 23, 2024 na hadi sasa, umetumia sh. milioni 581.81 na kwamba sh. milioni 2.46 zilizobakia ni za angalizo, kukamilisha ujenzi wa tenki na kulipa mafundi.

Previous Post

WASHINDI ‘CHANJA KIJANJA’ WAPATIKANA

Next Post

KIHONGOSI AVALIA NJUGA MGOGORO WA MIAKA 30

Next Post
KIHONGOSI AVALIA NJUGA MGOGORO WA MIAKA 30

KIHONGOSI AVALIA NJUGA MGOGORO WA MIAKA 30

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WASIRI : CCM INAFANYA KAZI KUBWA YA KULETA MAENDELEO

WASIRI : CCM INAFANYA KAZI KUBWA YA KULETA MAENDELEO

7 months ago
MAJIHA APANIA KUTETEA MKANDA WBO AFRIKA

MAJIHA APANIA KUTETEA MKANDA WBO AFRIKA

4 months ago

Popular News

  • DK.NCHIMBI AMTAJA ASKOFU MFUMBUSA NGUZO YA UMOJA

    DK.NCHIMBI AMTAJA ASKOFU MFUMBUSA NGUZO YA UMOJA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SITAWAANGUSHA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA YATIMUA VUMBI CAF, SIMBA MMH

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AMPA TANO SIMBU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAAJABU YA DP WORLD SIKU 730 BANDARINI DAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?