• ePaper
Tuesday, April 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

DIARRA, LOEMBA, OURA WALIVYOTIKISA DABI YA K’KOO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 3, 2026
in Burudani, Habari, Michezo
0
DIARRA, LOEMBA, OURA WALIVYOTIKISA DABI YA K’KOO
0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ABDUL DUNIA, Zanzibar

MCHEZO wa Yanga na Simba umeacha historia ya aina yake kwa wachezaji Djigui Diarra, Inno Loemba na Anicet Oura kutikisa katika mchezo huo wa watani wa jadi uliopigwa juzi.

Pambano hilo la Ligi Kuu Tanzania Bara, mzunguko wa kwanza, lilipigwa katika Uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar kuanzia saa 2:15 usiku ambapo timu hizo zilitoka suluhu.

Katika mchezo huo, Diarra alifanya kazi kubwa ya kuhakikisha nyavu zake hazitikiswi na wachezaji wa Simba.

Mlinda mlango huyo alifanya kazi ya ziada kuokoa mashuti ya Inno Loemba katika mchezo huo na kuwa mwiba mkali kwa nyota wa Simba.

Pia, Diarra alifanya hivyo, kuondoa mpira uliopigwa na Anicet Oura ambaye alipiga shuti kwa mguu wa kulia, lakini kipa huyo aliokoa.

Umahiri wa kipa huyo ulionekana zaidi, dakika za mwishoni mwa mchezo huo, baada ya Ellie Mpanzu kupata nafasi, lakini shuti lake la mguu wa kulia, liliokolewa na Diarra. Baada ya mchezo huo, kipa huyo alitangazwa na Bodi ya Ligi kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.

Lakini mara kadhaa, wachezaji hao wa Simba walionekana kuisumbua sana ngome ya Yanga na kumpa wakati mgumu kipa huyo kuhakikisha anakuwa makini ili kuokoa timu yake isifungwe.

Diarra ni raia wa Mali, wazi kwamba alisaidia timu yake kuambulia alama moja katika mchezo huo wa watani wa jadi.

SIMBA ILIKOSA BAHATI, UMAKINI

Simba ilitawala kwa kiasi kikubwa kipindi cha kwanza ikiwalazimisha Yanga kufanya makosa mara kwa mara.

Timu hiyo ilipata nafasi nyingi kipindi cha kwanza lakini ukosefu wa umakini wa ‘mastraika’ wake na ubora wa kipa Diarra ulikua kikwazo kuandika bao la kuongoza.

Kipindi cha pili, Selemani Mwalimu aliiandikia bao Simba, lakini mwamuzi wa pembeni, Kassim Mpanga alinyoosha kibendera akiashiria Mwalimu aliotea.

Kukataliwa bao hilo, kumeibua gumzo kwa wadau mbalimbali wa soka wakihoji, huku wengine wakipinga na wengine wakisema alikuwa bao.

Hata hivyo, Simba bado haikuwa bahati yao, baada ya De Reuck kupiga mpira kwa kichwa lakini uligonga mwamba.

MBINU ZA MAKOCHA

Yanga inanolewa na Pedro Goncalves na Simba inafundishwa na Steve Barker zilipiga soka la aina yake hatua ambayo iliufanya mchezo huo kuwa na ushindani wa hali ya juu.

Kocha wa Simba alichagua kuingia na mpango wa kutotumia mshambuliaji halisi wa kati na badala yake akiamua kuanza na ‘straika’ kivuli, Inno Loemba.

Kwa upande wa Yanga, kutokana na kumkosa Pacome Zouzoua anayeuguza majeraha, Pedro alimwanzisha Prince Dube kama mshambuliaji anayetokea pembeni huku viungo wakiwa Maxi Nzengeli, Mudathir Yahya, Duke Abuya na Mohamed Damaro.

HESABU MBIO ZA UBINGWA

Suluhu dhidi ya Simba ni wazi imeendelea kuiweka Yanga katika nafasi nzuri ya kutetea taji lake la tano mfululizo katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga hivi sasa inaendelea kusalia kileleni mwa msimamo ikiwa na alama 29 baada ya kucheza mechi 11 wakati Simba imefikisha pointi 24 katika mechi 11.

MECHI TANO ZIJAZO

Yanga itakuwa na kibarua dhidi ya Pamba Jiji, Singida Black Stars, Mbeya City na Tanzania Prisons.

Kwa upande wa Simba itakabiliwa na kibarua dhidi ya Fountain Gate, Coastal Union, Namungo, Azam FC na JKT Tanzania.

Katika ligi hiyo, Yanga ndiyo kinara wa mabao baada ya kupachika magoli 27 wakati Simba ikifunga mabao 18.

Yanga imefunga mabao hayo dhidi ya Pamba Jiji (3), Mtibwa (2), KMC (4), Fountain Gate (2), Coastal Union (1), Mashujaa (6), Dodoma (3), Namungo (1) na JKT Tanzania (5).

Wakati miamba hiyo ikifanya hivyo, Simba nayo imefunga mabao hayo dhidi ya Fountain Gate (3), Namungo (3), JKT Tanzania (2), Mbeya City (3), Mashujaa (2), Mtibwa (1), KMC (2) na Prisons (2).

MWENDO WA MABAO

Katika ligi hiyo, Yanga ndiyo kinara wa mabao baada ya kupachika magoli 27 wakati Simba ikifunga mabao 18.

Yanga imefunga mabao hayo dhidi ya Pamba Jiji (3), Mtibwa (2), KMC (4), Fountain Gate (2), Coastal Union (1), Mashujaa (6), Dodoma (3), Namungo (1) na JKT Tanzania (5).

Wakati miamba hiyo ikifanya hivyo, Simba nayo imefunga mabao hayo dhidi ya Fountain Gate (3), Namungo (3), JKT Tanzania (2), Mbeya City (3), Mashujaa (2), Mtibwa (1), KMC (2) na Prisons (2).

WAFUNGAJI YANGA

Katika mabao 27 iliyofunga Yanga, matano yamefungwa na ‘straika’ raia wa Zimbabwe, Prince Dube sawa na Depu kutoka Angola.

Depu alifunga mabao hayo dhidi ya Mashujaa, Dodoma Jiji (2), Namungo na JKT Tanzania wakati Dube akipachika dhidi ya Fountain Gate, Coastal Union, Mashujaa, Dodoma Jiji, JKT Tanzania

Pacome Zouzoua raia wa Afrika Kusini amepachika mabao matatu dhidi ya KMC, Mashujaa na Fountain Gate sawa na Mudathir Yahya aliyefunga dhidi ya Pamba Jiji, Mashujaa na JKT Tanzania.

Wengine ni Max Nzengeli aliyefunga mabao mawili dhidi ya Pamba Jiji na KMC sawa na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar na JKT Tanzania na Andy Boyeli dhidi ya KMC.

Waliofunga bao moja kila mmoja ni Duke Abuya dhidi ya Mashujaa, Celestine Ecua dhidi ya Mtibwa Sugar, Kouma dhidi ya Pamba Jiji, Damaro

Dhidi ya Mashujaa na Shekhani Rashid dhidi ya JKT Tanzania.

WAFUNGAJI SIMBA

Katika mabao 18 iliyofunga Simba, manne yamewekwa kimiani na Selemani Mwalimu na matatu yakifungwa na Rushine De Reuck.

Mwalimu alifunga mabao hayo dhidi ya Namungo, Mashujaa, KMC na Tanzania Prisons wakati De Reuck akifunga dhidi ya Fountain Gate, Namungo na Tanzania Prisons sawa na Jonathan Sowah aliyefunga dhidi ya Fountain Gate, JKT Tanzania na Mbeya City.

Aliyefunga mabao mawili ni Libase Gueye ambaye alipachika dhidi ya Mashujaa na KMC.

Waliofunga bao moja kila mmoja ni Charles Ahoua, Chamou Karaboue, Morice Abraham, Wilson Nangu, Mohamed Bajaber na Ellie Mpanzu.

VIKOSI

 Yanga iliwakilishwa na Djigui Diarra, Israel Mwenda, Mohamed Hussein, Dickson Job, Ibrahim Bacca, Damaro, Maxi Nzengeli, Duke Abuya, Depu, Mudathir Yahya na Prince Dube.

Simba: Kassali, Shomari Kapombe, Nickson Kibabage, Toure, Toure, De Reuck, Yusuph Kagoma, Libasse Gueye, Kante, Anicet Oura, Inno Loemba na Clatous Chama.

Previous Post

NHIF YATOA FARAJA KWA WAFUNGWA GEREZA LA ISANGA, DODOMA

Next Post

UBINGWA LIGI KUU WAWATEGA BARKER, PEDRO 

Next Post
UBINGWA LIGI KUU WAWATEGA BARKER, PEDRO 

UBINGWA LIGI KUU WAWATEGA BARKER, PEDRO 

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MAKATIBU WAKUU VYAMA VYA UKOMBOZI WAJADILI HALI YA KISIASA KUSINI MWA AFRIKA

MAKATIBU WAKUU VYAMA VYA UKOMBOZI WAJADILI HALI YA KISIASA KUSINI MWA AFRIKA

1 month ago
SINGIDA BS, YANGA SC KAZI IPO LEO

SINGIDA BS, YANGA SC KAZI IPO LEO

1 month ago

Popular News

  • UCHAGUZI WA WAJUMBE EALA WAANZA RASMI

    UCHAGUZI WA WAJUMBE EALA WAANZA RASMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUME ILIYOUNDWA NA RAIS DK. SAMIA ILIVYOBEBA MATUMAINI YA AMANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DCEA YAKAMATA SHEHENA YA MIRUNGI KUTOKA KENYA, YAKAMATA BOTI BAGAMOYO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ASKOFU MNDOLWA: TUME YA JAJI CHANDE ITAIPELEKA NCHI PAZURI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WASHIRIKI MISS WORLD TANZANIA WAPEWA SOMO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?