• ePaper
Friday, May 1, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

VIJANA MSIKUBALI KUBEBA AJENDA MSIZOZIJUA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 5, 2026
in Habari, Kitaifa
0
VIJANA MSIKUBALI KUBEBA AJENDA MSIZOZIJUA
0
SHARES
0
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na SELINA MATHEW

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, amewasihi Watanzania, hususan vijana kutokubali kutumika kubeba ajenda za watu wasiofahamu malengo yao. 

Amewasisitiza kukiamini Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuwa ni Chama pekee kinachohubiri amani, akisisitiza kulinda utulivu huo, maendeleo yazidi kuja katika Mkoa wa Shinyanga. 

Kihongosi alitoa kauli hiyo, alipohutubia wananchi wa Kata ya Isaka, Jimbo la Msalala,  baada ya kuwasili kwa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo, kusikiliza changamoto za wananchi na kuimarisha Chama. 

Kwa mujibu wa Kihongosi, vijana wanapaswa kuwa makini na kulinda mustakabali wa taifa, badala ya kushawishika kujiingiza katika vitendo vitakavyovuruga amani. 

“Msidanganywe mkaleta vurugu ndani ya maeneo yenu kwa sababu wanaofanya hivyo hawatoki hapa nchini, lindeni amani na utulivu mlionao,”alisema.

Kihongosi alisisitiza kuwa, amani ya Tanzania ni mtaji mkubwa unaowezesha wananchi kufanya shughuli zao za kiuchumi kwa utulivu na mafanikio. 

Alisema hakuna maendeleo yatakayoipatikana bila kuwepo kwa amani, umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi. 

“Tunashuhudia baadhi ya mataifa yakikumbwa na machafuko makubwa yanayosababisha vifo vya watoto, wanawake na wazee kwa sababu ya kukosekana kwa utulivu,” alisema. 

Kihongosi alisema Tanzania imejaliwa amani na umoja, hivyo ni wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha tunu hiyo inalindwa kwa gharama yoyote.

Alisema vijana wanapaswa kutambua kuwa wao ni nguvu kazi ya taifa na msingi wa maendeleo endelevu, hivyo wasikubali kupotoshwa. 

Katibu huyo aliwataka waendelee kushiriki katika shughuli halali za kiuchumi na kijamii zitakazochochea ustawi wa taifa badala ya kushiriki katika vitendo vya migawanyiko. 

Aliwasisitiza kukiamini Chama kwa kuwa ni Chama pekee kinachohubiri aman,  hivyo aliwasisitiza kulinda utulivu huo , maendeleo yazidi kuja katika mkoa huo. 

“Msidanganywe mkaleta vurugu ndani ya maeneo yenu kwa sababu aanaofanya hivyo hawatoki hapa nchini, lindeni amani na utulivu mlionao,”alisema. 

Kihongosi alisema amani ya nchi ikichafuka watakaopata tabu ni wanawake na watoto, aliwasihi Watanzania kutambua kuwa, amani ni maisha na uhai. 

“Amani ikitoweka hakuna umeme, barabara wala maendeleo yoyote, asije mtu yeyote wa kabila lolote akakusihi uharibu amani iliyopo, kuna watu wapo radhi nchi iharibike kwa maslahi yao binafsi. 

“Wanaofanya hivyo wanaishi ulaya wakishaharibu wanaondoka, wanapenda kuwatumia vijana kwamba komaa, pambana, Mwenyezi Mungu alikupa mwili kwa baraka, utunze utumie kutafuta fedha,”alisema. 

Kihongosi aliwasihi kutambua kuwa maisha yao ni mali yao, hivyo  asitokee mtu akawadhihaki kwa kutaka kuandamana na kwamba kama wanataka kufanya hivyo ni vyema wakaandamana kuleta maendeleo nyumbeni siyo kuchoma miundombinu ya serikali. 

“Wanaowashawishi mchome shule, hospitali wanapata huduma nje ya nchi, tulinde miundombinu yetu ya serikali, usikubali kupambana ndani ya ardhi uliyozaliwa,”alisema. 

Aliwasihi Watanzania kuendelea kumwombea Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, aendelee kuijenga nchi kupitia utekelezaji miradi. 

Kihongosi alisema katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake miradi mingine imetekelezwa kupitia ujenzi wa shule, reli na hospitali zimejengwa.

“Dk. Samia mapenzi yake kwa nchi ni makubwa, kaa jiulize kosa la Rais ni nini… utakuta ni chuki za kuambukizwa ziliopo miongoni mwa watu dhidi yake, jambo la kujiuliza hata ukimuuliza mtu anasema unajua..sunajua…usicheze ngoma usiyoijua.

Previous Post

TIBA ZA KIBINGWA BENJAMIN MKAPA ZAMVUTIA DK. MWINYI

Next Post

SINGIDA BS, YANGA SC KAZI IPO LEO

Next Post
SINGIDA BS, YANGA SC KAZI IPO LEO

SINGIDA BS, YANGA SC KAZI IPO LEO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

NITAONGOZA KWA KUZINGATIA USHIRIKIANO – SIMBACHAWENE

NITAONGOZA KWA KUZINGATIA USHIRIKIANO – SIMBACHAWENE

5 months ago
KOCHA SERENGETI BOYS AANIKA SIRI KUTWAA UBINGWA CECAFA

KOCHA SERENGETI BOYS AANIKA SIRI KUTWAA UBINGWA CECAFA

5 months ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?