• ePaper
Sunday, May 31, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TIBA ZA KIBINGWA BENJAMIN MKAPA ZAMVUTIA DK. MWINYI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 5, 2026
in Habari, Kitaifa
0
TIBA ZA KIBINGWA BENJAMIN MKAPA ZAMVUTIA DK. MWINYI
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameipongeza Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma kwa mageuzi na mafanikio makubwa katika utoaji huduma za matibabu ya kibingwa kwa wananchi.

Rais Dk. Mwinyi alisema hayo, alipokutana na Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Abel Makubi, Ikulu, Zanzibar.

Alisifu hatua kubwa ya utoaji huduma za kibingwa, yakiwemo matibabu ya figo, moyo na ubongo kufanyika nchini.

Rais Dk. Mwinyi alieleza hospitali hiyo umeipunguzia serikali na wananchi gharama za kuwapeleka wagonjwa kutibiwa nje.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi alishauri uongozi wa hospitali hiyo, kuendeleza utaratibu wa matibabu ya nje kwa kuwafikia wananchi katika maeneo yao kupitia mpango wa ‘outreach programme’, kwa kuwa unasaidia kuwatibu wagonjwa wengi zaidi.

Pia, Rais Dk. Mwinyi aliahidi serikali kupitia Wizara ya Afya Zanzibar, itaendeleza ushirikiano na hospitali hiyo na kutafuta njia bora za kufanya kazi pamoja.

Pia, Rais Dk. Mwinyi aliipongeza hospitali hiyo kuendeleza mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji kupitia taasisi za ndani na wadau kutoka nje.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Makubi alisema wamepata mafanikio makubwa kipindi cha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake, baada ya kutoa huduma za matibabu bobezi na kibingwa zaidi ya 20.

Profesa Makubi alitaja baadhi ni upandikizaji wa figo, upasuaji wa ubongo na matibabu ya moyo, hatua iliyochangiwa na jitihada za serikali kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya afya.

Previous Post

PROFESA SEMBOJA, KINYONDO WAGUSWA MATANKI YA MAFUTA

Next Post

VIJANA MSIKUBALI KUBEBA AJENDA MSIZOZIJUA

Next Post
VIJANA MSIKUBALI KUBEBA AJENDA MSIZOZIJUA

VIJANA MSIKUBALI KUBEBA AJENDA MSIZOZIJUA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TANZANIA YATAJWA KINARA AFRIKA MAPAMBANO USUGU WA VIMELEA

TANZANIA YATAJWA KINARA AFRIKA MAPAMBANO USUGU WA VIMELEA

6 months ago
MIKOPO YA SERIKALI KWA VIJANA, FURSA MPYA KUKUZA UCHUMI WA UVUVI

MIKOPO YA SERIKALI KWA VIJANA, FURSA MPYA KUKUZA UCHUMI WA UVUVI

2 months ago

Popular News

  • SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?