• ePaper
Wednesday, April 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

PROFESA SEMBOJA, KINYONDO WAGUSWA MATANKI YA MAFUTA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 5, 2026
in Habari, Kitaifa
0
PROFESA SEMBOJA, KINYONDO WAGUSWA MATANKI YA MAFUTA
0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

ATHNATH MKIRAMWENI NA IRENE MWASOMOLA

BAADHI ya wataalamu wa uchumi wametoa maoni tofauti, baada ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa matanki ya mafuta 15 ya kupokea mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam.

Akizungumza na UHURU, Mhadhiri wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Abel Kinyondo, alisema mradi huo utasaidia Tanzania kuwa na uchumi imara, hasa kunapotokea migogoro ya nje ya nchi inayosababisha bei ya bidhaa hiyo kupanda.

“Katika kipindi tulichopo hadi cha kati, uwekezaji huu ni muhimu sana kwasababu dunia hivi sasa ipo katika mitanziko mingi, moja kati ya namna ya ‘kudeal’ na mitanziko ni kuhakikisha una ‘storage’ kubwa,”alisema.

Amesema Tanzania ikiwa na sehemu kubwa zaidi ya kuhifadhi mafuta, nchi inaweza kwenda sokoni kununua mafuta na hivyo hata vita vya nje vikiibuka havitaathiri.

“Kama vita ya Ukraine inayoendelea Iran ikitokea, sisi tunakuwa ‘stable’ maana una ‘storage’ kwahiyo kuwa na hifadhi kunakupa ‘stability’,”alisema.

Aidha, Profesa Kinyondo, alishauri serikali kuendeleza jitihada za kuwekeza katika nishati mbadala, ikiwemo gesi kwa kuwa ndiyo suluhisho la kudumu hasa kipindi kunapotokea changamoto ya mafuta.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA), Profesa Haji Semboja, amesema Tanzania mradi huo utaimarisha uchumi na kudhibiti bei kipindi cha machafuko yanapotokea nchi za nje.

Profesa Semboja aliishauri serikali kuona namna ya kuendelea kuboresha sera na sheria katika usimamizi wa nishati hiyo kuongeza tija.

Mtaalamu wa uchumi, Fredy Naftari, alisema ujenzi wa matanki hayo utasaidia kuwa na hifadhi ya kutosha ya mafuta, hatua itakayoimarisha uchumi hasa katika kipindi cha misukosuko katika baadhi ya mataifa ya nje.

“Napongeza ujenzi wa matanki ni hatua nzuri kiuchumi, tukiwa na hifadhi kubwa ya mafuta, itasaidia nchi kuwa na akiba, kudhibiti uingizwaji holela wa mafuta na utakatishaji fedha,”alisema.

Naftari alisema ujenzi wa matanki hayo utasaidia shilingi ya Tanzania kuimarika, kwasababu mafuta yakiwepo nchini bidhaa hazitapanda bei.

Aidha, alimpongeza Rais Dk. Samia kuagiza kusomana mifumo ya Wizara ya Nishati, Wizara ya Uchukuzi, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuwa itaboresha mazingira ya uwekezaji.

Mchambuzi wa uchumi, Dk. Yohana Lawi,  alisema ujenzi wa matanki hayo utaongeza uwezo wa Bandari ya Dar es Salaam kuhudumia shehena za mafuta kwa ufanisi  mkubwa.

“Mradi huo utasaidia kudhibiti mabadiliko ya bei za mafuta yanayosababishwa na misukosuko ya soko la dunia, kuwa na akiba kubwa ya mafuta kunatoa uhakika wa upatikanaji wake hata panapotokea changamoto za kimataifa,” alisema.

“Mradi huo unaotekelezwa bila mikopo ya nje unapunguza utegemezi, unaepusha mzigo wa riba na kuonesha kuwa taifa lina uwezo wa kugharamia miradi mikubwa kwa mapato yake,” aliongeza.

Alisema kuongezeka uwezo wa kuhifadhi mafuta kutapunguza muda wa kuhudumia meli na gharama za ucheleweshaji, hivyo kuongeza mapato ya bandari na serikali.

Alisema uwekezaji huo ni nguzo muhimu katika kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara na usafirishaji wa nishati katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Mhadhiri wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) Dk. Timoth Lyanga, alisema ujenzi wa matanki hayo utasaidia kujenga uchumi imara unaojitegemea katika sekta ya nishati.

Dk. Lyanga alieleza miundombinu hiyo itaipa nchi uhakika wa nishati hata ikitokea migogoro au kupanda bei katika soko la dunia.

“Nchi yenye akiba ya kutosha haiyumbishwi kirahisi na mishtuko ya kimataifa, hatua hiyo itatoa muda wa kutosha kutafuta suluhisho endapo changamoto zitatokea,” alisema.

Akizungumzia maagizo ya Rais Dk. Samia ya kutaka mifumo isomane, Dk. Lyanga alisema itaimarisha uwazi, kuongeza ufanisi, kudhibiti mianya ya upotevu wa rasilimali na rushwa.

Kwa upande wake, Mchambuzi wa Masuala ya Uchumi na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Dk. Philip Daninga, alimpongeza Rais Dk. Samia kwa maono  ya kujenga msingi imara wa maendeleo.

Dk. Daninga alisema mafanikio ya miradi mikubwa kama huo, inategemea uwajibikaji wa kila Mtanzania katika nafasi yake, taifa liendelee kusonga mbele kwa umoja, uzalendo na kujitegemea.

Juzi, Rais Dk. Samia aliweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa matanki 15 ya kupokea mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam utakaogharimu sh. bilioni 678.6, ambazo zikijumlishwa na sh. bilioni 23.2 za thamani ya mkataba jumla ni sh. bilioni 701.8.

Previous Post

MAAGIZO YA DK. MIGIRO KWA SHULE YA UONGOZI MWALIMU NYERERE

Next Post

TIBA ZA KIBINGWA BENJAMIN MKAPA ZAMVUTIA DK. MWINYI

Next Post
TIBA ZA KIBINGWA BENJAMIN MKAPA ZAMVUTIA DK. MWINYI

TIBA ZA KIBINGWA BENJAMIN MKAPA ZAMVUTIA DK. MWINYI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TRILIONI 1.7/- ZANUFAISHA MIRADI MKOANI SINGIDA

TRILIONI 1.7/- ZANUFAISHA MIRADI MKOANI SINGIDA

7 months ago
AZAM KUSAKA MAKALI KUIVAA SIMBA

AZAM KUSAKA MAKALI KUIVAA SIMBA

3 weeks ago

Popular News

  • UCHAGUZI WA WAJUMBE EALA WAANZA RASMI

    UCHAGUZI WA WAJUMBE EALA WAANZA RASMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUME ILIYOUNDWA NA RAIS DK. SAMIA ILIVYOBEBA MATUMAINI YA AMANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DCEA YAKAMATA SHEHENA YA MIRUNGI KUTOKA KENYA, YAKAMATA BOTI BAGAMOYO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ASKOFU MNDOLWA: TUME YA JAJI CHANDE ITAIPELEKA NCHI PAZURI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WASHIRIKI MISS WORLD TANZANIA WAPEWA SOMO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?