• ePaper
Wednesday, April 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MAAGIZO YA DK. MIGIRO KWA SHULE YA UONGOZI MWALIMU NYERERE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 5, 2026
in Habari, Kitaifa
0
MAAGIZO YA DK. MIGIRO KWA SHULE YA UONGOZI MWALIMU NYERERE
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Asha-Rose Migiro ameitaka Bodi ya Wadhamini ya Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJNLS), kutekeleza mpango mkakati wa 2026/30 wa Shule hiyo ili kufikia malengo ya kuanzishwa kwake.

Kauli hiyo aliitoa alipofungua Kikao cha Bodi ya Wadhamini ya Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJNLS) iliyopo Kibaha mkoani Pwani.

Dk. Migiro alisema katika mpango huo mkakati umeainisha vipaumbele vitano vikiwemo kuimarisha malezi ya kiitikadi na kiuongozi.

Alisema vipaumbele vingine vilivyopo katika mpango huo ni kuongeza uwasilishaji wa programu na umuhimu wa kuongeza matokeo ya utafiti na sera.

“Vipaumbele vingine katika mpango huo ni kukamilisha misingi ya taasisi, ikiwemo mifumo ya kidijitali na uhakiki wa ubora na kuhakikisha uendelevu kupitia ufadhili unaotabirika na matumizi yanayoakisi umiliki wa Vyama,”alisema.

Alisema vipaumbele hivyo vilivyopo katika mpango huo vinaipa Shule hiyo mwelekeo wa kutoka hatua ya mwanzo iliyofanikiwa hadi kuwa taasisi iliyokomaa, yenye dira na inayozalisha viongozi na mawazo kwa ajili ya uongozi.

“Hali hizi ndizo zinazoipa muktadha na umuhimu Mpango Mkakati wa 2026–2030 ulioko mbele yetu ambapo unatutaka kufikiri kuanzishwa kwa taasisi hii,” alisema. 

“Kikao chetu cha Januari mwaka 2024 kilikuwa hatua muhimu ya mabadiliko wakati huo tulikutana kama Kamati Elekezi, tukiisindikiza taasisi iliyokuwa bado inaweka misingi yake na leo tunakutana ndani ya mfumo wa uongozi ulioimarishwa,” alisema. 

Alisema kufuatia uzinduzi huo wa Bodi ya Uongozi na uanzishwaji wa mifumo muhimu ya kiutendaji hatua hiyo inawakumbusha funzo kuwa taasisi hukomaa kwa juhudi za makusudi.

“Kwa hiyo, kikao hiki kina wajibu wa vitendo zaidi ya kupokea taarifa, lazima tutoe mwelekeo na tufanye maamuzi yatakayogeuza Mpango Mkakati wa 2026–2030 kuwa programu hai ya utekelezaji — yenye ufadhili, matumizi na ufuatiliaji madhubuti,”alisema.

Alisema majadiliano hayo yanapaswa kutimiza mambo manne muhimu, ikiwemo kuthibitisha Shule kama taasisi ya kimkakati, kukubaliana juu ya ufadhili na matumizi yenye kuaminika.

“Kuimarisha nidhamu ya uongozi kupitia ratiba thabiti za vikao na mifumo ya ufuatiliaji na kutoa mwongozo wa kisiasa,” alisema.

Wajumbe waliohudhuria kikao hicho ni Katibu Mkuu wa Chama cha ANC (Afrika Kusini), Fikile Mbalula, Katibu Mkuu wa Chama cha FRELIMO (Msumbiji), Chaki Felizardo Passadas Aboobacar, Katibu Mkuu wa Chama cha ZANU-PF (Zimbabwe), Jacob Francis Nzwindamilimo Mudenda, Chama Cha SWAPO  (Namibia), kimewakilishwa na Mjumbe wa Kamati Kuu, Dkt. Samuel Abraham Peyavali Mushelenga na Chama cha MPLA (Angola) kimewakilishwa na Mjumbe wa Kamati Kuu, Frederico Toth Jorge De Miranda.

Previous Post

TASWIRA VIGOGO VINNE LIGI KUU BARA IKO HIVI

Next Post

PROFESA SEMBOJA, KINYONDO WAGUSWA MATANKI YA MAFUTA

Next Post
PROFESA SEMBOJA, KINYONDO WAGUSWA MATANKI YA MAFUTA

PROFESA SEMBOJA, KINYONDO WAGUSWA MATANKI YA MAFUTA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WAZIRI CHONGOLO AELEKEZA MIFUMO TOSCI ISOMANE

WAZIRI CHONGOLO AELEKEZA MIFUMO TOSCI ISOMANE

5 months ago
MAPATO TRA YAZIDI KUTIKISA

MAPATO TRA YAZIDI KUTIKISA

3 months ago

Popular News

  • UCHAGUZI WA WAJUMBE EALA WAANZA RASMI

    UCHAGUZI WA WAJUMBE EALA WAANZA RASMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUME ILIYOUNDWA NA RAIS DK. SAMIA ILIVYOBEBA MATUMAINI YA AMANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DCEA YAKAMATA SHEHENA YA MIRUNGI KUTOKA KENYA, YAKAMATA BOTI BAGAMOYO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ASKOFU MNDOLWA: TUME YA JAJI CHANDE ITAIPELEKA NCHI PAZURI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WASHIRIKI MISS WORLD TANZANIA WAPEWA SOMO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?