• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

SIMBA MZUKA UMEPANDA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 13, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
SIMBA MZUKA UMEPANDA
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

KUFUATIA ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Black Stars, Kocha wa Simba, Steve Barker amesema kuwa ushindi huo umewaongezea morali na kasi ya kupambana katika mchezo unaofuata.

Simba, iliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida BS katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Airtel uliopo mkoani Singida.

Baada ya mchezo huo Simba imefunga safari kuelekea Arusha kwa ajili ya mchezo wake mwingine dhidi ya TRA utakaochezwa kesho katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Kocha Barker alisema kuwa ilikuwa mechi ngumu kwao kwani walicheza uwanja wa ugenini, lakini wachezaji wake walipambana kuhakikisha wanafikia malengo ya kupata ushindi.

Alisisitiza, ushindi huo umewaongezea morali na kasi ya kupambana kuhakikisha wanaendelea kufanya vyema katika mechi zitakazofuata za michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Alisema amefurahia matokeo hayo na kwamba anawapongeza wachezaji wote kwani kila mmoja alitimiza majukumu yake uwanjani na kuhakikisha wanaibuka kidedea.

Alisema bado anahitaji wachezaji wake kutumia vyema nafasi ambazo wanazipata ili kuweza kushinda mabao mengi katika kila mchezo.

“Ujue mchezo huo umetuongezea morari ya kutosha kuelekea katika mechi zinazofuata hasa dhidi ya TRA, hivyo hatuna muda wa kupumzika tutapambana kuhakikisha tunafanya maandalizi kwa ajili ya mchezo wetu huo, lengo likiwa ni kupata ushindi na kujizolea pointi tatu muhimu,” alisema Barker.

Kocha huyo alisema kulikuwa na makosa ambayo wachezaji wake waliyafanya katika mchezo uliopita, hivyo ameyafanyia kazi katika uwanja wa mazoezi na kwamba ana imani watapata ushindi mechi inayofuata.

Alisema hana hofu na kikosi alichokuwa nacho kwani kila mchezaji amekuwa akijituma na kuonesha uwezo mkubwa kuhakikisha anaisaidia timu kufanya vyema.

Naye Kocha wa Singida BS, David Ouma alisema kuwa timu yao ilipoteza mechi hiyo baada ya kuzidiwa mbinu na wachezaji wa Simba.

Alisema timu yake ilicheza vizuri na kuonesha kiwango kikubwa tofauti na wapinzani wao lakini bahati haikuwa yao baada ya kuzidiwa mbinu, hivyo watahakikisha wanakwenda kufanyia marekebisho katika mapungufu yaliyojitokeza ili kupata ushindi katika mechi zijazo.

“Timu bora imepoteza katika mchezo wetu jambo ambalo limeniumiza japokuwa wachezaji wangu walicheza katika kiwango kizuri, ninajua tuna mechi nyingi mbele yetu tutapambana mwanzo hadi mwisho kuweza kupata ushindi na kujihakikishia nafasi nzuri katika msimamo wa ligi,” alisema Ouma.

Kocha huyo alisema kuwa kwa hivi sasa wanakwenda kujipanga kwa ajili ya mchezo unaofuata dhidi ya Mbeya City na lengo lao ni kuhakikisha wanapata ushindi.

Katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 27 baada ya kushuka dimbani mara 12 huku Singida BS ikishika nafasi ya 10 kwa pointi 19 baada ya kushuka dimbani mara 13.

Previous Post

MAKUBWA YAFICHULIWA

Next Post

SERIKALI KUWABEBA WASANII, WANAHABARI

Next Post
SERIKALI KUWABEBA WASANII, WANAHABARI

SERIKALI KUWABEBA WASANII, WANAHABARI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA, MWINYI WAMELETA MAENDELEO NCHINI – DK. NCHIMBI

DK. SAMIA, MWINYI WAMELETA MAENDELEO NCHINI – DK. NCHIMBI

6 months ago
TWIGA STARS YAPEWA MCHONGO WAFCON

TWIGA STARS YAPEWA MCHONGO WAFCON

4 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?