• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

SERIKALI YATENGA BIL. 240/- KUJENGA MASOKO 30 NCHINI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
July 23, 2026
in Habari, Kitaifa
0
SERIKALI YATENGA BIL. 240/- KUJENGA MASOKO 30 NCHINI
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na FRED ALFRED, Dodoma

SERIKALI imetenga sh. bilioni 240 kwa ujenzi wa masoko 30 ya kisasa yenye hadhi ya mkoa nchini.

Hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa kuboresha mazingira ya biashara, kuongeza ajira kwa vijana na kuimarisha uchumi wa wananchi.

Hayo yalibainishwa jijini hapa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, alipotembelea Soko la Machinga.

Msigwa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, alisema pamoja na ujenzi wa masoko makubwa, itaendelea kujenga mengine madogo katika maeneo mbalimbali ya miji na vituo vya biashara.

Pia, kuwapa wafanyabiashara wadogo, hususan wamachinga maeneo salama na rafiki ya kufanyia shughuli zao.

“Serikali itaendelea kujenga masoko madogo katika maeneo ya katikati ya miji kurahisisha mazingira ya wamachinga kufanya biashara zao kwa utulivu na usalama,” alisema.

Pia, serikali imetenga sh. bilioni 264 za ujenzi wa stendi 32 za kisasa katika maeneo yenye muunganiko mkubwa wa usafiri na biashara, utekelezaji wake ukiwa umefikia zaidi ya asilimia 80.

Akizungumzia Soko la Machinga la Dodoma, Msigwa alisema awali lilipangwa kuwahudumia wafanyabiashara 2,700, hivi sasa lina wapo zaidi ya 4,800, jambo linaloonesha mafanikio ya mpango wa serikali wa kujenga masoko ya kisasa kwa vijana na wafanyabiashara wadogo.

Msigwa alisema takribani asilimia 80 ya wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao katika soko hilo ni vijana, hali inayodhihirisha masoko hayo yamekuwa chanzo muhimu cha ajira na kipato.

“Soko hili ni miongoni mwa masoko 15 yanayojengwa na serikali nchini. Masoko 10 tayari yamekamilika kwa asilimia 100 na ujenzi wa masoko matano unaendelea. 

“Dhamira ya serikali ni kuendelea kutengeneza mazingira bora ya kufanyia biashara,” alisema.

Aliendelea kusema,  masoko hayo yamejengwa kwa gharama ya zaidi ya sh. bilioni 15 na Soko la Machinga la Dodoma pekee, hupokea zaidi ya watu 10,000 kwa siku wanaofika kununua bidhaa.

Aliwataka vijana kutumia fursa zinazotolewa na serikali kupitia masoko hayo kujiongezea kipato na kujiepusha na vitendo vya uhalifu.

KUHUSU MIKUTANO YA HADHARA

Msigwa alisema serikali itaruhusu tena kufanyika mikutano ya hadhara, baada ya vyombo vya ulinzi na usalama, kujiridhisha kama hali inaruhusu.

Alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali ya utekelezaji wa shughuli za serikali.

Alisema uamuzi wa kuruhusu mikutano ya hadhara, utategemea tathmini ya vyombo vya ulinzi na usalama, ambavyo vina wajibu wa kuhakikisha amani na utulivu vinakuwepo nchini.

Alisisitiza kuwa, suala la ulinzi na usalama halina mbadala.

Alieleza kuwa, serikali imepokea taarifa za kuwepo baadhi ya watu wenye nia ovu wanaoweza kutumia mikutano ya hadhara kufanya vitendo vitakavyohatarisha usalama wa nchi.

“Ni jukumu la serikali kuhakikisha inalinda wananchi na mali zao,”alisema.

Msigwa alisema kazi ya vyombo vya ulinzi na usalama ni kuzuia vitendo vya uhalifu kabla havijatokea.

Alisema vikibaini hakuna tena viashiria vya vitendo vyenye nia ovu, mikutano ya hadhara itaruhusiwa kuendelea kama kawaida.

Alitoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kudumisha amani.

Previous Post

RAIS DK. SAMIA AHIMIZA UWEKEZAJI AFYA AFRIKA

Next Post

WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

Next Post
WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MSIGWA AELEZA MANUFAA UBORESHAJI RELI YA TAZARA

MSIGWA AELEZA MANUFAA UBORESHAJI RELI YA TAZARA

7 months ago
KWAHERI WILLIAM LUKUVI

KWAHERI WILLIAM LUKUVI

4 months ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?