• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TANZANIA INAYO HIFAHI YA KUTOSHA YA MAFUTA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 24, 2026
in Habari, Kitaifa
0
TANZANIA INAYO HIFAHI YA KUTOSHA YA MAFUTA
0
SHARES
18
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na SELINA MATHEW, Dodoma

SERIKALI imewahakikishia wananchi uwepo wa nishati ya mafuta ya kutosha nchini, huku ikitangaza mkakati wa kudhibiti kupanda kiholela kwa nishati hiyo muhimu nchini.

Pia, imesema tayari baadhi ya zipo meli zipo njiani zikiwa zimebeba shehena ya mafuta, ambayo yataongeza wigo wa uwepo wa bidhaa hiyo.

Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, amesema hayo jijini hapa jana, baada ya kuzungumza na taasisi zilizo chini ya wizara walivyojipanga vizuri kuhakikisha upatikanaji wa mafuta na usalama wake unakuwepo nchini.

“Tuna usalama mkubwa wa mafuta nchini, serikali inatarajia kuona shughuli zote zikiendelea kama kawaida.

“Niwahakikishie Watanzania mafuta yapo na Serikali itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha shughuli zinaendelea kama kawaida kupitia upatikanaji wa nishati hii,” alisema.

Amesema taasisi hizo zimeeleza kuhusu mchakato wa uagizaji mafuta ulivyofanyika kupitia mikataba, jambo linaloonesha utoshelevu wa bidhaa hiyo.

“Ikumbukwe kabla ya vita kuanza bei ya pipa moja ilikuwa inaanza Dola 60 hadi 65, hivi tunavyozungumza leo (jana) asubuhi bei ilikuwa Dola 112 hadi 120, utaona ndani ya siku hizi kadhaa za vita bei ya kidunia imeongezeka mara mbili

“Tunaendelea kuangalia namna ambavyo bei inaendelea duniani ili na sisi kama Serikali tuhakikishe tunaweka mikakati ya kuwa na bei hilimivu katika soko,”amesema Ndejembi.

MAAGIZO MATATU

Ngejembi aliitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), kuhakikisha mafuta yote yaliyopo nchini yanatumika na hakuna kampuni inayoficha bidhaa hiyo kwa kigezo cha kusubiri bei zipande duniani.

“Hakikisheni wakati wote mafuta yanapatikana kuanzia Dar es Salaam hadi Kyerwa, yawe yanapatikana wakati wote. Sitarajii kuona watu wakisema hawana mafuta wakati matanki ya kuhifadhi yana mafuta.

“Tufanye kazi kwa jirani zaidi na TRA kuhakikisha mafuta ambayo yameshaidhinishwa kutumika yanatoka haraka katika matanki yawafikie wananchi,”alisema waziri huyo.

Pia, aliutaka Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), kuhakikisha mafuta yote ambayo wameingia mikataba yanafika nchini.

“Tuhakikishe na tukague meli ipi ipo wapi, inafika lini, nimeangalia mwenendo duniani kuna meli nyingine zinageuka zinapelekwa katika masoko ambayo hayana mafuta kwa sababu wanapata faida mara mbili hadi tatu.

“Sasa watatuacha sisi bila kuwa na mafuta, katika hili iundwe timu kati ya PBPA, EWURA, TPDC na vyombo vya ulinzi na usalama kufuatilia kwa karibu meli hizi kuwa mzigo wote uliodhamiriwa kuja Tanzania unafika kwa wakati,” aliongeza.

Aidha, Ndejembi aliliagiza Shirika la Maendeleleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuhakikisha mafuta yote ya miezi ambayo hatuna yanafika nchini.

Naye Mkurugenzi Mkuu EWURA, Dk. James Andilile, alisema mamlaka hiyo inafuatilia kwa ukaribu hali ya mafuta na hifadhi zote zilizopo katika kanda zake sita.

Mkurugenzi Mkuu PBPA, Erasto Simon, alisema hadi jana mafuta ya petrol yalikuwa lita milioni 230 ambayo yanatosheleza kwa matumizi ya siku 38.

Kiwango cha mafuta ya dizeli yaliyopo ni lita milioni 180 yanayotosheleza siku 28, mafuta ya ndege lita miioni 31 kwa matumizi ya siku 47.

“Mafuta ambayo yamepakiwa na meli ambazo zipo baharini kuja bandari ya Dar es Salaam, petroli lita milioni 245, dizeli lita milioni 208 na mafuta ya ndege ni lita milioni 23.

“Ukijumuisha mafuta ya petroli yaliyopo na yaliyopo melini yatatosha kwa matumizi ya siku 78, dizeli siku 50 na mafuta ya ndege siku 91,” alisema Simon.

“Tumepitia mikataba ya uagizaji mapema kwa mwezi wa sita na saba tumeshaisaini na itakapofika mwezi wa tano katikati yataanza kuingia nchini,” alisema Mkurugenzi Mkuu TPDC, Mussa Makame.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati (Mafuta na Gesi Asilia) James Mataragio, alisema Tanzania ipo vizuri katika hifadhi ya mafuta kulinganisha na nchi jirani.

Previous Post

MAREKANI YAKOSHWA KASI MAENDELEO Z’BAR

Next Post

KATIBU MKUU CCM ZIARANI UCHINA

Next Post
KATIBU MKUU CCM ZIARANI UCHINA

KATIBU MKUU CCM ZIARANI UCHINA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

Wachezaji wa SIMBA na YANGA

YANGA, SIMBA MECHI YA KISASI NA HESHIMA

8 months ago
SABABU WATOTO 4,000 KUTELEKEZWA KILA MWAKA DAR ES SALAAM ZATAJWA

SABABU WATOTO 4,000 KUTELEKEZWA KILA MWAKA DAR ES SALAAM ZATAJWA

3 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?