• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DK. NCHIMBI ATANGAZA NEEMA YA MAJI UBUNGO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 29, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
DK. NCHIMBI ATANGAZA NEEMA YA MAJI UBUNGO

MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi

0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NJUMAI NGOTA

MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amesema wakazi wa maeneo ya Sinza, Ubungo, Makurumla, Kimara na Mabibo jijini Dar es Salaam, wataondokana na tatizo la upatikanaji majisafi na salama.

Hiyo, inatokana na kuimarisha miradi ya maji, kama sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka mitano ijayo.

Balozi Dk. Nchimbi, alisema hayo Viwanja vya EPZA, Mabibo Hosteli, Dar es Salaam, alipowahutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa kampeni wa Chama, kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu.

Alisema Ilani ya CCM, imeainisha mikakati madhubuti ya kumaliza kero ya maji, inayowakabili wakazi wa maeneo hayo kwa kuboresha vyanzo vya maji na kuimarisha miundombinu ya usambazaji wake.

“Mbunge wenu wa Ubungo, Profesa Kitilla Mkumbo, amenidokeza kuhusu shida ya maji inayowakabili wananchi wa jimbo hili.

“Ninatambua kero hiyo, niwahakikishie kuwa, Ilani ya CCM imeweka mkazo wa kipekee katika kutatua changamoto hii, kupitia uboreshaji wa vyanzo na miradi ya maji katika maeneo ya Kimara, Mabibo, Sinza, Ubungo na Makurumla,” alisema.

Alisema iwapo watapewa ridhaa ya kuongoza nchi, wataongeza ufanisi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), kwa kuimarisha mifumo ya mawasiliano, kuwawezesha wananchi kutoa taarifa za matatizo ya maji haraka na ufanisi zaidi.

MASOKO YA KISASA NAHUDUMA BORA

Katika kuhakikisha wananchi wa Ubungo wanapata huduma karibu na makazi yao, Balozi Dk. Nchimbi, alisema wamedhamiria kutekeleza mpango wa ujenzi na ukarabati wa masoko ya kisasa 13 ndani ya Wilaya ya Ubungo.

Alisema hatua hiyo, itapunguza adha ya wananchi kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hizo.
“Nimeelezwa kuwa, wakazi wa Ubungo hulazimika kwenda Mlimani City au Kituo cha Kimataifa cha Afrika Mashariki kununua bidhaa.

“Hili tunaliona na tunalifanyia kazi. Katika miaka mitano ijayo, tutajenga masoko ya kisasa 13 katika wilaya hii, huduma zote zipatikane karibu,” alisema.

UBORESHAJI HUDUMA ZA AFYA

Alisema serikali ijayo ya CCM, itaendelea kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa Ubungo, kufanya ukarabati mkubwa katika Hospitali ya Manispaa ya Ubungo kwa kuongeza majengo, vifaatiba na idadi ya watumishi, itoe kutoa huduma za upasuaji wa dharura na matibabu ya magonjwa yote.
Pia, alisema wamekusudia kujenga zahanati tatu na kituo cha afya katika maeneo yenye uhitaji mkubwa, kupunguza msongamano wa wagonjwa na kuimarisha upatikanaji wa huduma.

MIKOPO ASILIMIA 10

Alisema wamedhamiria kuongeza kasi ya utoaji mikopo ya asilimia 10 kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, kupitia halmashauri huku akisisitiza kuwa, mfumo huo, utaboreshwa na kuondoa upendeleo.

Hivyo, aliahidi kuwekwa utaratibu wa kurasimisha biashara za wajasiriamali wadogo, kutambuliwa rasmi na kupata mikopo, elimu ya biashara na fursa nyingine za kiuchumi.

MIPANGO MIJI, MAZINGIRA SAFI

Kuhusu mpango wa makazi na mazingira, Dk. Nchimbi, alisema serikali ijayo ya CCM, itasimamia kikamilifu sheria za mipango miji, kuboresha makazi, kupanga miji kwa ramani rasmi na kuhakikisha mfumo wa ukusanyaji taka, unafanya kazi kwa ufanisi huku wananchi wakihusishwa katika utunzaji wa mazingira.
“Lazima miji yetu ipangwe vizuri. Hili tutalisimamia kwa nguvu zote kwa kuhakikisha kila eneo, lina ramani, makazi bora na mazingira safi,” alisema.

UFANISI WA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

Akielezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia, alisema yamejikita katika kusimamia uchumi, kupunguza mfumuko wa bei na kuongeza kasi ya ukuaji wa pato la taifa.

“Agosti, mwaka huu, mfumuko wa bei, ulikuwa asilimia 3.1, ukilinganisha na Malawi ambako mfumuko ulifikia asilimia 28.

“Hii ni dalili ya usimamizi mzuri wa uchumi. Kwa miaka minne, uchumi wa Tanzania, ulikua kwa asilimia 4.8, hivi sasa umepanda hadi asilimia 5.6,” alisema.

Alisema hatua za Rais Samia katika kuimarisha diplomasia ya uchumi, zimewezesha Tanzania kuvutia wawekezaji wengi na kuongeza kiwango cha bidhaa zinazouzwa nje ya nchi hasa Kenya.

“Hivi sasa tunauza bidhaa nyingi zaidi nje ya nchi na kiwango cha utoaji wa leseni kwa wafanyabiashara kimeongezeka. Haya ni mafanikio ya kazi kubwa ya Rais wetu,” alisema.

MBOMBEA UBUNGE UBUNGO

Naye, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ubungo, Profesa Kitilla Mkumbo, alianisha mafanikio mengi yaliyopatikana jimboni humo ukiwemo ujenzi wa barabara.
Pia, Mkumbo alimwombea kura Dk. Samia, wabunge na madiwani wanaotokana na Chama kwa wananchi, katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Previous Post

CHINI YA DK. SAMIA, USTAWI UMEONEKANA – DK. MIGIRO

Next Post

DK. SAMIA AAHIDI NEEMA TANGA AKIPEWA RIDHAA YA KUONGOZA NCHINI

Next Post
DK. SAMIA AAHIDI NEEMA TANGA AKIPEWA RIDHAA YA KUONGOZA NCHINI

DK. SAMIA AAHIDI NEEMA TANGA AKIPEWA RIDHAA YA KUONGOZA NCHINI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WATANZANIA 37,647,235 KUPIGA KURA LEO

WATANZANIA 37,647,235 KUPIGA KURA LEO

6 months ago
YANGA, SIMBA ZAPEWA MBINU KULIPA KISASI 

YANGA, SIMBA ZAPEWA MBINU KULIPA KISASI 

3 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?