• ePaper
Saturday, June 27, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DK. MWIGULU: TUENDELEE KUMUOMBEA LUKUVI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 26, 2026
in Habari, Kitaifa
0
DK. MWIGULU: TUENDELEE KUMUOMBEA LUKUVI
0
SHARES
12
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI MKUU, Dk. Mwigulu Nchemba amewaomba Watanzania waendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, marehemu William Lukuvi aliyefariki jana Machi 25, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma.

Akiongea kwa niaba ya Serikali nyumbani kwa marehemu Area D, jijini Dodoma leo, Alhamisi, Machi 26, 2026, Waziri Mkuu amesema: “Kwa niaba ya Serikali natoa pole kwa familia, ndugu, jamaa. Jambo hili zito, gumu kulielewa, gumu kulipokea.”

…Lakini ndio limeshatufika na sote hatukutarajia maana Mheshimiwa Waziri alikuwa kazini. Tuendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu na kuifariji familia. Mwenyezi Mungu awaimarishe kwa sababu yeyé ndio mfariji mkuu,” amesisitiza.

Vilevile, Dk. Mwigulu ametumia fursa hiyo kuihakikishia familia kwamba Serikali itaendelea kuwa pamoja nayo katika kipindi hiki chote cha majonzi.

Viongozi wengine waliokuwepo msibani hapo ni pamoja na Naibu Spika, Daniel Siro, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Masauni, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumisi wa Umma na Utawala Bora), Ridhiwani Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Dk. Toba Nguvila.

Previous Post

MAFURIKO KILOMBERO, KAYA 150 ZAKOSA MAKAZI

Next Post

PBPA YAAGIZWA KUHARAKISHA UPOKEAJI NA USAZAMBAZAJI WA MAFUTA NCHINI

Next Post
PBPA YAAGIZWA KUHARAKISHA UPOKEAJI NA USAZAMBAZAJI WA MAFUTA NCHINI

PBPA YAAGIZWA KUHARAKISHA UPOKEAJI NA USAZAMBAZAJI WA MAFUTA NCHINI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA, DK. NCHIMBI WAIMWAGIA SIFA STARS

RAIS DK. SAMIA, DK. NCHIMBI WAIMWAGIA SIFA STARS

6 months ago
MTANDAO WA GESI KINYEREZI HADI CHALINZE, SASA WANUKIA

MTANDAO WA GESI KINYEREZI HADI CHALINZE, SASA WANUKIA

9 months ago

Popular News

  • YANGA, SIMBA SIKU YA KILIO,KICHEKO

    YANGA, SIMBA SIKU YA KILIO,KICHEKO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VIJANA 400  WAAGWA KWENDA KUFANYA KAZI NJE YA NCHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‘NAFUU YA MAFUTA KUANZA KUONEKANA JULAI’ NDEJEMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAZITAKA TAASISI ZOTE KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL-NINO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SAMAMBA AWAFUNDA WAKAGUZI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?