• ePaper
Tuesday, September 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

VIJANA 400  WAAGWA KWENDA KUFANYA KAZI NJE YA NCHI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
June 27, 2026
in Habari, Kitaifa
0
VIJANA 400  WAAGWA KWENDA KUFANYA KAZI NJE YA NCHI
0
SHARES
11
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, amewaaga vijana 400 wa Kitanzania wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi, akisisitiza umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kuchangia katika Mfuko huo ili kujihakikishia ulinzi wa kijamii na ustawi wa maisha yao ya sasa na baadaye.

Amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwaaga vijana hao, ambao pia walipata elimu ya hifadhi ya jamii kutoka NSSF ikiwa ni sehemu ya kuwaandaa kwa maisha na ajira zao nje ya nchi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Sangu amempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake imara unaoendelea kuimarisha diplomasia ya ajira na kufungua fursa salama kwa Watanzania kufanya kazi nje ya nchi, hatua inayoongeza usalama na heshima ya wafanyakazi wa Kitanzania katika soko la ajira la Kimataifa.

Aidha, amesema Serikali inaendelea kupanua wigo wa hifadhi ya jamii ili kuwafikia Watanzania wengi zaidi, hususan vijana na wananchi waliojiajiri, akieleza kuwa Hifadhi Skimu imekuwa nyenzo muhimu ya kuwaunganisha wananchi na mfumo wa hifadhi ya jamii.

“Nitumie fursa hii kuipongeza Benki ya CRDB na NSSF.Hii ni kazi ya kimkakati kwa mustakabali wa vijana wetu. Zamani walikuwa wakiondoka bila uelewa wa hifadhi ya jamii, lakini sasa kupitia Hifadhi Skimu wanapata elimu na kuelezwa faida za kujiunga na kuchangia, ikiwemo kunufaika na mafao mbalimbali yakiwemo ya matibabu kwao na familia zao,” amesema Waziri Sangu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, amemshukuru Waziri Sangu kwa kuendelea kuipa kipaumbele sekta ya hifadhi ya jamii katika ajenda ya kazi zenye staha, sambamba na kumpongeza Rais Dk. Samia kwa kuendelea kufungua fursa za ajira ndani na nje ya nchi kwa Watanzania.

Amesema NSSF inaendelea kuboresha huduma zake kupitia mafao mbalimbali, yakiwemo pensheni ya uzee, urithi, ulemavu, uzazi, upotevu wa ajira pamoja na matibabu, akisisitiza kuwa lengo ni kuhakikisha kila mwanachama analindwa katika kila hatua ya maisha yake.

Kwa upande wake,  Mkurugenzi  wa Huduma za Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano Jane Sorogo, amemshukuru Rais Dk. Samia kwa uongozi wake unaoendelea kupanua fursa za ajira nje ya nchi kwa Watanzania, pamoja na Waziri Sangu kwa kuhakikisha wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi wanafuata taratibu sahihi na haki zao zinalindwa.

Amebainisha kuwa mafanikio ya ajira za nje yanategemea ushirikiano kati ya Serikali, taasisi za umma na sekta binafsi. Aidha, alizishukuru Benki ya CRDB na NSSF kwa kutoa elimu ya hifadhi ya jamii na kuwaandikisha vijana hao katika Hifadhi Skimu ili waanze kujiwekea akiba na kunufaika na mafao yanayotolewa na Mfuko.

Previous Post

‘NAFUU YA MAFUTA KUANZA KUONEKANA JULAI’ NDEJEMBI

Next Post

YANGA, SIMBA SIKU YA KILIO,KICHEKO

Next Post
YANGA, SIMBA SIKU YA KILIO,KICHEKO

YANGA, SIMBA SIKU YA KILIO,KICHEKO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

JKT YATAKATA LIGI KUU BARA

JKT YATAKATA LIGI KUU BARA

10 months ago
TAIFA STARS KUTUA MOROCCO KWA KISHINDO

TAIFA STARS KUTUA MOROCCO KWA KISHINDO

9 months ago

Popular News

  • SIMBA HII GUSA UNASE CAFCL

    SIMBA HII GUSA UNASE CAFCL

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UNDANI UGONJWA WA FIGO NA MATIBABU YAKE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA NI KIONGOZI WA MATOKEO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA, NDEJEMBI TURUFU YA MAENDELEO KWA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI AONYA, ATOA SIKU 60 WENYE SILAHA HARAMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?