• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MAFURIKO KILOMBERO, KAYA 150 ZAKOSA MAKAZI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 26, 2026
in Habari, Kitaifa
0
MAFURIKO KILOMBERO, KAYA 150 ZAKOSA MAKAZI
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na IGAMBA LIBONGE, Kilombero

KAYA 150 zimeathirika kutokana na mafuriko, kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.

Maeneo yaliyoathirika zaidi ni Mabukula (Kata ya Kibaoni), Kata za Lumemo, Michenga, Mbasa, Kiberege, Mbingu na Chita.

Akizungumza na UHURU, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Dunstan Kyobya, amesema vikosi vya uokoaji vipo eneo la tukio kusaidia wananchi walioathirika.

Kyobya amesema hadi sasa, hakuna taarifa ya vifo vilivyoripotiwa, baada ya kutembelea maeneo yaliyoathirika, ambapo alitoa rai kwa wananchi wanaoishi mabondeni kuhama kwa muda kwenda sehemu salama kuepuka madhara.

Aidha, Kyobya amewataka wananchi hao kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko, yanayoweza kutokea kufuatia mvua hizo.

Katika Kata ya Mbingu mafuriko hayo yamesababisha athari kubwa baada ya kuharibu makazi, miundombinu ya barabara na mali za wananchi.

Pia, maji yamejaa maeneo mengi na kusababisha kukatika mawasiliano ya barabara, hatua iliyochangia ugumu wa upatikanaji huduma muhimu za kijamii.

Vilevile, Daraja la Rufuru linalounganisha Kata ya Chita na Mlimba, limevunjika usiku wa kuamkia jana na kukatisha mawasiliano ya barabara kati ya Ifakara na Mlimba.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba, Jamali Idrissa, alisema serikali inaendelea kuchukua hatua kwa kutoa msaada kwa waathirika wa mafuriko hayo.

Previous Post

DK. NCHIMBI ATOA KAULI UBORESHAJI WA MITAALA

Next Post

DK. MWIGULU: TUENDELEE KUMUOMBEA LUKUVI

Next Post
DK. MWIGULU: TUENDELEE KUMUOMBEA LUKUVI

DK. MWIGULU: TUENDELEE KUMUOMBEA LUKUVI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA AMELETA MIRADI MIKUBWA LINDI – MAJALIWA

DK. SAMIA AMELETA MIRADI MIKUBWA LINDI – MAJALIWA

7 months ago
DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

6 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?