Na ZIANA BAKARI
MSANII wa filamu na tamthilia, Miriam Ismail ‘Cecy’, amewasihi Watanzania kuendelea kudumisha amani ya nchi.
Akizungumza na UHURU Dar es Salaam,, msanii huyo amesema amani ni nguzo muhimu ya maendeleo na ustawi wa taifa.
Amesema kuwa, kila mwananchi ana jukumu la kuhakikisha jambo hilo linafanyika na kupewa kipaumbele.
“Bila ya amani hakuna maendeleo endelevu ni muhimu kwa jamii kushirikiana na kuishi kwa upendo, mshikamano na kuheshimiana kwa kila mmoja.
“Nawaomba Watanzania wenzangu tuendele kupendana na kuthaminiana sisi wote kitu kimoja, jambo la muhimu kwetu ni kuendelea kulinda tunu yetu ya taifa ambayo ni amani,” alisema.
Msanii huyo ambaye alifanikiwa kushiriki katika tamthilia na filamu mbalimbali zikiwemo, ‘Mzani wa Mapenzi’, ‘Single Mama’ na ‘Jeraha’ alisema bila ya kufanya hivyo hakuna kitu kinaweza kufanyika kama amani haipo.




