• ePaper
Tuesday, April 21, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 15, 2026
in Habari, Kitaifa
0
TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI MAALUMU, Njombe

TIMU ya netiboli ya Ofisi ya Makamu wa Rais, inatarajia kufungua pazia la Michezo ya Mei Mosi kwa kuumana na kikosi cha Wizara ya Maji Aprili 16, 2026.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Kamati ya Mashindano ya Mei Mosi Taifa, jana, mtanange huo utafanyika katika Uwanja wa Mji Mwema mjini Njombe ukiwa ni sehemu ya shamrashamra ya maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani, ambayo kitaifa yanafanyika mkoani humo.

Akizungumzia mashindano hayo, Katibu wa Klabu ya Michezo Ofisi ya Makamu wa Rais, Marwa Nyaisawa, alisema timu yao imejiandaa vyema kutoa ushindani katika michezo hiyo.

“Tunatambua ni mara yetu ya kwanza kushiriki michezo hii kupitia timu ya mpira wa pete (netiboli) lakini kwa maandalizi tuliyofanya tunatarajia kutoa ushindani kuanzia hatua ya makundi na kuendelea,” alisema Nyaisawa.

Alisema wanatambua ugumu wa michezo ya Mei Mosi kutokana na kila timu kufanya maandalizi makubwa, hata hivyo wamedhamiria kuibuka washindi bila kujali ubora wa washiriki wengine.

“Benchi letu la ufundi la limeweza kujenga morali na hali ya kujiamini kwa wachezaji, kwa hiyo tunaamini tutaingia katika mashindano tukiwa fiti kuonesha ushindani,” alitamba.

Alisifu ratiba ya michezo hiyo kupangwa vizuri ambapo katika hatua ya makundi, timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais imepangwa Kundi H pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Maji na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Katibu huyo alieleza baada ya mchezo dhidi ya Wizara ya Maji, Aprili 17 watavaana na timu ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na mechi ya mwisho ya hatua ya makundi itakuwa dhidi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Aprili 18.

Kwa upande wake, Kocha wa timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Mafuru Buriro alisema kikosi chake kipo tayari kwa michezo hiyo ambayo wataitumia kusuka kikosi imara kinachotarajia kutoa ushindani katika mashindano mengine ya kitaifa ya netiboli.

“Wachezaji wote wapo tayari na tunazidi kuimarika siku hadi siku na benchi la ufundi linafanyia kazi kasoro tunazoziona katika uwanja wa mazoezi na tumekusudia kuonesha kitu tofauti kwa wapinzani wetu katika michezo hii,” alisema Buriro.

Kaulimbiu ya Michezo ya Mei Mosi, 2026 inasema: “Michezo kwa Afya, Ajira, Furaha na Kazi Inaendelea; Kazi zenye staha ni Nguzo Imara kwa Maendeleo Endelevu katika Utekelezaji wa Dira 2050”.

Previous Post

SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

Next Post

SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

Next Post
SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA ATAJA FAIDA ZA MPANGO WA NISHATI

RAIS DK. SAMIA ATAJA FAIDA ZA MPANGO WA NISHATI

2 months ago
TUMAINI JIPYA LA MIKOPO KWA VIJANA

TUMAINI JIPYA LA MIKOPO KWA VIJANA

2 weeks ago

Popular News

  • MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

    MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‘MISS WORLD’ KUIPAISHA TANZANIA DUNIANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BIL. 195.66/- KUJENGA BONDE MTO MSIMBAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ULEGA AJIBU MAPIGO KUHUSU MTANDAO WA BARABARA NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NEEMA YAJA, MIKAKATI HADHARANI KUINUA VIJANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?