• ePaper
Wednesday, April 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 15, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

KIKOSI cha Simba kinatarajiwa kushuka dimbani kumenyana na Fountain Gate FC, kocha wa Simba, Steve Barker amesema anajua mchezo utakuwa mgumu lakini hawatakubali kupoteza mchezo huo muhimu kwa lengo la kuweka heshima ya kuchukua pointi tatu.

Simba leo inatarajiwa kushuka dimbani kupambana na Fountain Gate katika mchezo wake wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa katika Uwanja wa Tanzanite, Kwaraa Babati jijini Arusha  kuanzia saa 10:00 jioni.

Akizungumza kuelekea katika mchezo huo, Barker alisema ligi ni ngumu kwani kila timu imejipanga kupata matokeo mazuri, lakini yeye anajivunia wachezaji wake kutokana na maandalizi mazuri waliyoyafanya.

 “Najua tunaingia katika mchezo mgumu na wenye changamoto kubwa, lakini tutapambana kuhakikisha timu inapata ushindi na kujizolea pointi tatu muhimu,” alisema Barker.

Kocha huyo alisema wamefanya marekebisho yaliojitokeza katika mchezo uliopita kuhakikisha tim u yake inafanya vizuri katika mchezo huo.

Nyota wa timu hiyo, Selemani Mwalimu alisema kuwa wachezaji wote wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata ushindi katika pambano hilo.

 “Tunajua mzunguko wa pili unakuwa mgumu na wenye changamoto kubwa lakini tumejipanga vizuri kuhakikisha tunapata ushindi katika mchezo huo muhimu na kila mchezaji hataki kuona tunapoteza,” alisema Mwalimu.

Naye Kocha Msaidizi wa Fountain Gate, Abubakar Ally alisema wanajua wanacheza na Simba yenye wachezaji  wazuri lakini watapambana kupata matokeo mazuri.

Alisema hawataingia na hofu katika mchezo huo kwani

“Simba ni timu bora ina wachezaji wenye uzoefu mkubwa, lakini sisi tutacheza mchezo huo bila ya kuwa na hofu kwani tutatumia nafasi zote ambazo tutazipata kupata ushindi,” alisema.

Abubakar alisema wanaiheshimu Simba na hawatoruhusu kutengeneza makosa mengi kwani watawapa fursa wapinzani wao kuyatumia na kupata ushindi.

Nahodha wa timu hiyo, Jackson Shija alisema kuwa wachezaji wote wa timu hiyo, wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata ushindi katika pambano hilo.

 “Sisi kama wachezaji, tumejipanga vizuri kuhakikisha tunapata ushindi katika mchezo huu, kila mchezaji ana hamu ya kuipambania timu na kutoruhusu mabao katika lango letu,” alisema Shija.

Katika msimamo wa Ligi, Simba ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 36 huku Fountain Gate, ikishika nafasi ya 14 na pointi 16 baada ya timu zote mbili kushuka dimbani mara 17.

UONGOZI WA SIMBA WATOA NENO KUHUSU SOWAH

Wakati huo huo, uongozi wa Simba wamemrejesha rasmi mchezaji wao Sowah katika kikosi cha klabu hiyo baada ya kusimamishwa kwa takribani mwezi mmoja na siku 20.

Februari 25, 2026 wakati Simba ikiwa Dodoma siku hiyo ikijiandaa kucheza dhidi ya Dodoma Jiji, zilitoka taarifa za Sowah kurudishwa Dar es Salaam kwa kile kilichodaiwa ni kuhitajika na Kamati ya Nidhamu ya klabu hiyo kujibu tuhuma zinazomkabili za utovu wa nidhamu.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema ni kweli Jonathan Sowah walimsimamosha kutoka katika kambi yao mwezi Machi, mwaka huu, waliposafiri kwenda Dodoma kucheza na Dodoma Jiji amerejeshwa ndani ya klabu hiyo.

“Sowah alikuwa akituhumiwa kwa makosa kadha wa kadha ya utovu wa nidhamu ambayo ni malalamiko yaliyokuja kutoka kwenye benchi la ufundi, baada ya pale akarejeshwa kutoka Dodoma akarejea Dar es Salaam kusubiri taratibu za klabu ziweze kukamilika na hatimaye haki yake iweze kupatikana.

“Baada ya pale alipelekwa katika kamati ya nidhamu ya Simba ambayo inaongozwa na Mwenyekiti wake, kamanda mstaafu Kova (Suleiman), Sowah akaitwa mbele ya kamati akasomewa mashtaka yake yote ambayo amekiri na mengine amekataa maelezo na baada ya pale kamati ikajiridhisha ya kwamba mchezaji huyu ana makosa ya utovu wa nidhamu, baada ya kujiridhisha huko akapewa adhabu.” alisema Meneja huyo.

Ahmed alisema adhabu hiyo ni kwanza faini ya pili ameamrishwa aende akafanye mazoezi na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20.

“Adhabu hii inaanza mara moja kuanzia hivi sasa, atakuwa anafanya mazoezi na timu yetu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ikiwa ni kipindi cha kumwangalia kama kutakuwa kuna mabadiliko yoyote ndani yake katika upande wa nidhamu basi adhabu yake hiyo itaisha na atarejea timu kubwa.

“Kama akishindwa basi tutajua hukumu itakuwaje hapo baadae. Kwa hiyo huo ndio mustakabali wa Sowah na Simba Sports Club ya kwamba yupo katika kuitumikia adhabu yake aliyopewa ambayo ni kufanya mazoezi na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ikiwa ni kipindi cha kumwangalia mwenendo wake,” alisema Ahmed.

Previous Post

RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

Next Post

TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

Next Post
TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

NYOTA YANGA WAPEWA TANO

NYOTA YANGA WAPEWA TANO

5 days ago
DK. SAMIA, BALOZI NCHIMBI WAAHIDIWA KURA ZA KISHINDO

DK. SAMIA, BALOZI NCHIMBI WAAHIDIWA KURA ZA KISHINDO

8 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?