• ePaper
Wednesday, April 29, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

CCM YAFUNGUKA RIPOTI TUME YA JAJI CHANDE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 25, 2026
in Habari, Kitaifa
0
CCM YAFUNGUKA RIPOTI TUME YA JAJI CHANDE
0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na WAANDISHI WETU

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kinaunga mkono mapendekezo yote yaliyotolewa na Tume ya Kuchunguza Matukio ya Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, mwaka 2025.

Pia, kimesema baada ya kutokea matukio hayo lazima taifa lirudi pamoja kuponya majeraha kwa njia ya maridhiano.

Akizungumza na UHURU katika ofisi ndogo zilizopo Lumumba jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wasira, alisema Chama kimeridhishwa na kazi kubwa iliyofanywa na tume hiyo, kwa sababu imegusa maeneo yote muhimu ambayo yalikuwa yanazungumzwa.

“Kama nchi, lazima turudi pamoja, lazima tuponye majeraha kwa njia ya maridhiano, bahati nzuri maridhiano katika Chama chetu ni kitu ambacho kipo katika sera zetu.

“Kama mnavyojua Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, alipoapishwa kuwa Rais, alikuja na falsafa ya 4R.

“Jambo la maridhiano ni la msingi, tunakubaliana na pendekezo la tume, tunakubaliana na maoni ya tume kuhusu kuwa na baraza la ushauri la wazee, siyo la kikatiba, lakini kupata hekima,”alisema.

Wasira alisema maridhiano hayo, yawe ya kuridhiana na jamii na makundi yote ya kijamii siyo wanasiasa pekee.

“Kila kundi litatoa maoni namna gani ya kurudisha nchi katika shabaha ya kuwa na amani na umoja.

“Maridhiano siyo kwamba, tunaridhiana na chama fulani cha siasa, maana kuna vyama vingine vinaanza kutuletea kwamba, msipofanya hivi hakuna maridhiano, hii siyo sawa, mimi nadhani tunaridhiana na jamii yote, tutazungumza na makundi yote ya kijamii,”aliongeza.

Alisema makundi mbalimbali yakiwemo madhehebu ya dini, yatashiriki katika kuponya taifa na kila kundi litatoa maoni yake.

AWAPA UJUMBE VIJANA 

Akizungumzia taarifa ya tume kuhusu vijana kutumika katika ghasia kwa kigezo cha ukosefu wa ajira, Wasira alisema hakuna nchi yoyote duniani ambayo vijana wote wameajiriwa na serikali.

Pia, alisema Ilani ya CCM imetilia mkazo zaidi katika uwekezaji, ukiwemo wa viwanda ukiwa ni mpango mahsusi kwa vijana.

Alisema uwekezaji huo ni fursa kwa vijana kujiajiri na kwamba, serikali imetenga sh. bilioni 200 kwa ajili ya utoaji wa mikopo.

MATUMIZI YA MITANDAO

Akizungumza kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii, Wasira alisisitiza vijana kuitumia kwa manufaa yao na nchi badala ya kuleta mkanganyiko.

KANALI MSTAAFU SIMBAKALIA

Naye, Kanali mstaafu, Joseph Simbakalia, alisema ripoti ya tume hiyo, imeakisi dhamira njema ya kubaini ukweli wa mambo na kutenda haki.

Pia, alisema ripoti hiyo, imeshirikisha wananchi kwa uadilifu na weledi wa hali ya juu katika kukusanya taarifa za kuaminika.

“Wasilisho limedhihirisha bayana kuwa, taarifa ya tume ni matokeo ya kazi ya uchunguzi ulioshirikisha wananchi kwa uadilifu na weledi wa hali ya juu katika kukusanya taarifa za kuaminika.

“Kwa ujumla ni taarifa inayoakisi dhamira njema ya kubaini ukweli wa mambo na kutenda haki,” alisema.

Ripoti ya tume hiyo, ilikabidhiwa kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, jana Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Samia, aliiunda tume hiyo Novemba 18, mwaka jana baada ya kutokea vurugu wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu.  

Alimteua Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman kuwa mwenyekiti huku wajumbe wake wakiwa Jaji Mkuu Mstaafu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Balozi Ombeni Sefue.

Wajumbe wengine ni Mwanadiplomasia na Balozi Radhia Msuya, Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu (IGP) Said Mwema, Balozi Mstaafu Luteni Jenerali Paul Meela, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mstaafu Dk. Stergomena Tax, Balozi Mstaafu David Kapya.

VIONGOZI WA DINI

Kwa upande wake, Mkuu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini, Askofu Dk. Fredrick Shoo, aliipongeza tume ya kuchunguza matukio wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, mwaka jana kwa kufanya kazi kubwa ya kuiponya taifa kwa ujumla.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, jana, Dk. Shoo alisema ripoti hiyo ya Tume, imeponya sehemu kubwa ya Watanzania kwa kuongea ukweli na kutoa mapendekezo.

Alisema endapo mapendekezo hayo yakifanyiwa kazi, Tanzania itazidi kuwa kisiwa cha amani.

“Tunaipongeza Tume kwa kufanya kazi nzuri, naamini kazi hii waliyoifanya, itachangia katika kuendelea kuliponya taifa letu ili tuweze kurudi katika misingi yetu kama Watanzania.

“Niiombe sana serikali na wale watakaohusika kupokea mapendekezo ya Tume waliotoa, ni mapendekezo mazuri na tunaomba yafanyiwe kazi kwa haraka zaidi naamini yatatusaidia,”alisema.

Naye, Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Hassan Kabeke, alimpongeza Rais Dk. Samia kwa ujasiri wake wa kuunda Tume  iliyo bora na iliyofanya kazi yake kwa uwazi.

Alisema licha ya Tume hiyo kuwa ya uwazi, ilikuwa na mwongozo mzuri kwa sababu ya Mwenyekiti na Wajumbe wake, walikuwa sahihi kufanya kazi hiyo.

Hata hivyo, Sheikh Kabeke, alisema Tume hiyo imedhihirisha wazi kuwa, Watanzania wapo imara, wanaweza kufanya mambo yao bila ya kuingiliwa na mtu au watu wengine.

“Tume hii imefichua mambo kadhaa, ikiwemo uhodari na uwazi kwa watendaji wetu wa serikali, hiyo inatokana na kazi nzuri iliyofanywa na Tume iliyoongozwa na Jaji Chande,”alisema.

Aidha, alisema Tume imefanya kazi nzuri, imetimiza wajibu wake iliotakiwa kufanya, ikiwemo kutaja chanzo cha tatizo ya yale yote yaliyotokea Oktoba 29, mwaka jana.

“Tayari hivi sasa Watanzania na dunia kwa ujumla, wameshajua kiini cha changamoto ya yale yote yalitokea siku hiyo,”alisema.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maaskofu na Mashekh ya Haki, Amani na Maadili kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini nchini, Askofu William Mwamalanga, alisema Tume ya Jaji Chande, ipo sahihi na lengo lilikuwa kutaka kujua ukweli  wa yale yote yaliyotokea Oktoba 29, mwaka jana.

Hivyo, aliwaomba Watanzania kuwa na amani na utulivu, huku wakisubiri utekelezaji ukifanyika.

“Kuundwa kwa Tume hii ni ujasiri tosha aliouonesha Rais Dk. Samia kuwa, ni kiongozi hodari na mbunifu katika kazi zake,”alisema.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania (JMAT), Dk. Mussa Salum, alisema Tume imefanya kazi kubwa ya kizalendo ya kuchambua kwa kazi hali iliyojitokeza na kutoa ushauri kwa mamlaka.

Alisema kazi hiyo, ni ya kizalendo na mfano wa kuigwa, kwani inaonesha uwezo mkubwa uliopo kwa Watanzania katika kutatua changamoto za Watanzania pasipo kuamini kuwa, wengine kutoka nje ya nchi ndiyo wenye uwezo wa kuchunguza ya kwetu.

“Majibu ya Tume yamepokelewa, kazi yetu viongozi wa dini ni kuhakikisha tunaunganisha serikali na wananchi, kujenga taifa moja la watu wamoja.

“Tuangalie wapi tulipokosea, tujisahihishe, makosa yaliyokosewa tuyarekebishe, tukae pamoja tusonge mbele,” alisema.

Aliwasisisitiza wananchi kuwa watulivu na kusimama katika dhamira njema ya kuijenga Tanzania, siyo kuibomoa kwani ikiharibika hakuna atakayekuwa salama.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Pwani, Samaha Said, aliipongeza Tume kwa kazi kubwa waliyoifanya yenye tija kwa wananchi katika kudumisha amani, mshikamano na maridhiano.

Pia, alimpongeza Rais Samia kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuunda Tume huru, hatimaye kutoa matokeo ambayo yanalenga kuwaunganisha Watanzania na kuimarisha maridhiano ya kitaifa.

NENO LA WAFANYABIASHARA

Mwenyekiti  wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo,  Severine Mushi,  alisema ameipokea ripoti hiyo kwa moyo mkunjufu kwa kuwa, imelenga kuleta maridhiano ya kitaifa huku akimpongeza Rais Samia kwa kuunda Tume hiyo kutekeleza jukumu hilo.

“Kwa kweli, ripoti tumeipokea na tunapongeza kwa kuundwa kwa ile Tume,  tunashauri maridhiano yaende haraka mtu yeyote asiachwe nyuma katika maridhiano hayo na twende pamoja,” alisema.

Mushi, alisema uongozi wa jumuiya hiyo na wanachama, hawataki hali ya uvunjifu wa amani iliyotokea Oktoba 29, mwaka jana itokee tena, kwa kuwa, iliathiri biashara za watu mitaani kwa maduka kuchomwa, kuvunjwa na kusimama kwa biashara.

Akizungumzia uamuzi wa Rais Samia wa serikali kuchukua jukumu la kulipia gharama za matibabu kwa majeruhi wa vurugu za Oktoba 29, alisema uamuzi huo ni busara, unapaswa kuungwa mkono.

Kwa mujibu wa Mushi, majeruhi wengi wanatoka katika familia masikini, hivyo gharama za kujitibia zinakuwa gharama kubwa kwao.

Hata hivyo, aliomba Wizara ya Afya, kuwa na orodha ya majeruhi hao na kuweka dawati maalumu la matibabu ya majeruhi, wasisumbuliwe kupata huduma wanapokwenda hospitalini.

Naye, Makamu Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Machinga, Steven Lusinde, alisema ameipokea ripoti hiyo na kusema imeakisi kilichotokea Oktoba 29, mwaka jana.

Lusinde alimpongeza Mwenyekiti wa Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani, Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29,  2025, Jaji Mkuu mstaafu, Mohamed Chande Othman,  kwa kusimamia utekelezaji wa majukumu ya tume hiyo.

Pia, alimpongeza Rais Samia, kwa kuwahakikishia wananchi kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyoainishwa katika ripoti hiyo.

Aliwahimiza wananchi kuwa na subira kipindi ambacho serikali inayafanyia kazi mapendekezo ya ripoti hiyo.

Imeandikwa na Irene Mwasomola, Rehema Maigala, Simon Nyalobi na Superius Ernest .

Previous Post

4 ZAONGOZA KWA UKAME WA MABAO LIGI KUU BARA

Next Post

WATUMISHI NIRC WASHEREHEKEA MWAKA 2026, WAASWA KUIMARISHA MSHIKAMANO, UWAJIBIKAJI

Next Post
WATUMISHI NIRC WASHEREHEKEA MWAKA 2026, WAASWA KUIMARISHA MSHIKAMANO, UWAJIBIKAJI

WATUMISHI NIRC WASHEREHEKEA MWAKA 2026, WAASWA KUIMARISHA MSHIKAMANO, UWAJIBIKAJI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA: HAKUNA MAENDELEO BILA AMANI

RAIS DK. SAMIA: HAKUNA MAENDELEO BILA AMANI

4 months ago
WAZIRI NANAUKA AWAONYA VIONGOZI WANAOKWAMISHA SHUGHULI ZA VIJANA

WAZIRI NANAUKA AWAONYA VIONGOZI WANAOKWAMISHA SHUGHULI ZA VIJANA

5 months ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?