• ePaper
Sunday, June 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 27, 2026
in Habari, Kitaifa
0
TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI
0
SHARES
12
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

RAIS wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhokya, amewataka waajili nchini kutekeleza Amri ya nyongeza ya Kima cha Chini cha mishahara kwa wafanyakazi wa sekta binafsi kama inavyofanywa na Serikali.

Nyamhokya ametoa kauli hiyo leo Aprili 27, 2026 alipotembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano katika maonesho ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi yanayoendelea mkoani Njombe.

Alisema Serikali ilitangaza kima hicho cha chini cha mishahara ambacho kimeanza kutumika mwezi Januari mwaka huu, ambapo hadi sasa takwimu zinaonesha ni takribani asilimia 80 tu ya waajili katika sekta binafsi wameanza kutekeleza.

“Nitoe wito kwa waajili wa sekta binafsi nchini kutekeleza amri hii ya serikali kwa kuongeza mishahara husika… hatua itakayochangia ustawi na morali ya wafanyakazi,” alisisitiza Rais huyo wa TUCTA.

Akiwa katika banda hilo, Nyamhokya alipokea maelezo ya elimu zinazotolewa, ikiwemo elimu ya huduma za ajira, kinga ya jamii, sheria za kazi nchini pamoja na mahusiano baina ya Serikali na Makundi ya Kijamii yanayo jumuisha Taasisi za Dini, Mashirika yasiyo ya Kiserikali,Wadau wa Siasa na Asasi za kiraia.

Alipongeza maafisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa elimu wanayoitoa kwa umma kwenye maonesho hayo, akisema inaakisi huduma za wizara kwa wananchi na wafanyakazi.

Pia, Nyamhokya amewaasa wananchi na wafanyakazi kuendelea kutembelea banda hilo ili kupata elimu zaidi ikiwemo elimu ya kinga ya jamii.

Katika hatua nyingine, Rais wa TUCTA amewasihi wafanyakazi mkoani Njombe na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi katika sherehe za Mei Mosi zinazotarajiwa kufanyika kitaifa katika mkoa huo.

Previous Post

OMR YANAWIRI KARATA WANAWAKE MEI MOSI

Next Post

WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

Next Post
WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA KUUNGURUMA MOROGORO

DK. SAMIA KUUNGURUMA MOROGORO

10 months ago
RAIS DK. SAMIA ALIVYOIPAISHA MICHEZO

RAIS DK. SAMIA ALIVYOIPAISHA MICHEZO

5 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

    RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • AFRIKA KUCHOCHEA UTUNZAJI MAZINGIRA KUPITIA NISHATI SAFI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWAKINYO AOMBA RADHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, SIMBA NI KIVINGINE ZAIDI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MEXICO YAANZA KWA KISHINDO WC, KADI ZATEMBEA HATARI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?