• ePaper
Sunday, June 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

OMR YANAWIRI KARATA WANAWAKE MEI MOSI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 27, 2026
in Habari, Kitaifa
0
OMR YANAWIRI KARATA WANAWAKE MEI MOSI
0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

OFISI ya Makamu wa Rais, imebuka mshindi wa nafasi ya tatu kupitia mchezo wa karata upande wa wanawake katika Mashindano ya Mei Mosi, 2026 yanayoendelea mkoani Njombe.

Mchezaji aliyepeleka shangwe upande wa timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais ni Shinuna Mohamed aliyemfunga Annastazia Majenga kutoka Chuo cha Maendeleo ya Mipango Vijijini (IRDP) alama 2-0 katika mchuano uliofanyika Uwanja wa CCM Sabasaba mwishoni mwa wiki.

Akizungumzia ushindi huo, Shinuna aliishukuru menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuthamini michezo na kusema mafanikio hayo yawahusu watumishi wote.

Alisema ushindi huo ni historia kwake ikizingatiwa ilikuwa mara yake ya kwanza kushiriki mashindano makubwa ya karata, ambayo alipaswa kutumia mbinu za ziada kuwafunga wapinzani wake.

“Timu zote zimejiandaa vyema na mashindano haya, nilitumia uzoefu wangu kwa kusoma mbinu za wapinzani na kuweza kuwafunga…Ninajivunia mafanikio haya, naahidi kuweka bidii zaidi mashindano yajayo nishike nafasi za juu,” alisema Shinuna.

Aidha, mchezaji huyo alisema mchezo wa karata ni mgumu kama ilivyo mpira wa miguu, ambapo inahitajika maandalizi ya kutosha kupata matokeo mazuri.

Shinuna alisema amefurahia kukutana na wachezaji wazoefu wa mashindano makubwa ikiwemo SHIMIWI, ambao walimfanya atumie akili nyingi kuwashinda katika mchezo wa karata.

Kwa upande wake, Katibu wa Klabu ya Michezo Ofisi ya Makamu wa Rais, Marwa Nyaisawa alieleza ushindi wa Shinuna ni kielelezo cha ari, mshikamano na juhudi zinazoendelea kuoneshwa na wachezaji wa kikosi kizima cha Ofisi ya Makamu wa Rais katika mashindano ya Mei Mosi mwaka huu.

“Tumekuwa na mwendelezo mzuri wa timu yetu katika mashindano ya Mei Mosi pamoja na kushiriki mara ya kwanza, hii inadhihirisha dhamira tuliyojiwekea ya kupata mafanikio tuliyodhamiria,” alisema Nyaisawa.

Alisema mashindano ya Mei Mosi mwaka huu yamewapa uzoefu kwa mashindano mengine baadaye.

Nafasi ya kwanza katika mchezo wa karata kwa upande wa wanawake imekwenda kwa Malkia Nondo kutoka timu ya Mahakama, huku kwa wanaume ikichukuliwa na Susu Jeremia wa kikosi cha Wizara ya Afya.

Previous Post

SIMBA, MLANDEGE NI KUFA AU KUPONA

Next Post

TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

Next Post
TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

BIL. 36.6/- ZAPAISHA UCHUMI WA VIJANA

BIL. 36.6/- ZAPAISHA UCHUMI WA VIJANA

6 months ago
BONDIA MWAKYEMBE KUTOA ZAWADI YA KRISMASI

BONDIA MWAKYEMBE KUTOA ZAWADI YA KRISMASI

6 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

    RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • AFRIKA KUCHOCHEA UTUNZAJI MAZINGIRA KUPITIA NISHATI SAFI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWAKINYO AOMBA RADHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, SIMBA NI KIVINGINE ZAIDI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MEXICO YAANZA KWA KISHINDO WC, KADI ZATEMBEA HATARI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?