• ePaper
Sunday, May 10, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

MTIHANI MZITO KWA MOALIN

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 9, 2026
in Burudani, Habari, Michezo
0
MTIHANI MZITO KWA MOALIN
0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na VICTOR MKUMBO

UNAWEZA kusema ni mtihani mzito kwa Kocha Abdihamid Moalin anakwenda kukabiliana nao katika mchezo wa kwanza baada ya kukabidhiwa mikoba ya kuinoa timu ya Yanga wakati ikiikabili Coastal Union.

Yanga itakuwa mwenyeji wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union, utakaochezwa Uwanja wa KMC, jijini Dar es Salaam kuanzia saa 12:15 jioni.

Moalin atakutana na mtihani huo kwa mara ya kwanza akiliongoza benchi la ufundi la Yanga kufuatia kutimuliwa kazi kwa aliyekuwa mtangulizi wake Pedro Goncalves.

Moalin alirejeshwa Yanga tangu Machi 23, mwaka huu akiwa kocha msaidizi chini ya Goncalves.

Tangu Moalin aliporejea Yanga akiwa kocha msaidizi, tayari amekaa benchi la ufundi katika mechi tano za Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo awali aliwahi kuajiriwa nafasi ya mkurugenzi wa ufundi kwa vipindi tofauti chini ya aliyekuwa kocha Sead Ramovic na kubeba taji la Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho na Ligi ya Muungano msimu wa mwaka 2024/2025.

Alipowasili kwa mara nyingine, Moalin alikuwa katika benchi la ufundi Yanga ilipoichapa Prisons mabao 3-0, baadaye Yanga ikiifunga Pamba Jiji ugenini mabao 3-0.

Pia, Yanga ilipoirarua Mbeya City mabao 6-0, Yanga ilipotoka sare ya 2-2 ugenini dhidi ya Simba kabla ya kuichapa KMC bao 1-0 kocha huyo alikuwepo.

Hata hivyo, Goncalves ameondoka katika kikosi hicho na mikoba yake ikichukuliwa na Moalin ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa pointi 51 baada ya kucheza mechi 21.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, jana, Kocha wa Muda wa Yanga, Moalin alisema wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata ushindi mnono katika mchezo huo.

Moalin alisisitiza kwamba mechi dhidi ya Coastal Union haitakuwa rahisi kwani wamekuwa wakiwapa upinzani mkali kila mara.

Alisisitiza maandalizi yao yamekwenda vizuri na jana jioni walifanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo huo na wachezaji wote wapo fiti.

“Maandalizi ya mchezo dhidi ya Coastal Union yamefanyika salama na kila mchezaji yupo imara kukabiliana na mchezo huo, nina matumaini na vijana wetu kuwa watatupatia kila kilicho bora, kitu ninachoweza kuwaahidi mashabiki wa Yanga ni mchezo mzuri,” alisema.

Aliongeza kuwa Coastal Union ni timu nzuri, lakini watacheza nayo kwa kuiheshimu kuhakikisha Yanga inachukua alama tatu katika pambano hilo.

Kwa upande wake mchezaji wa Yanga, Abutwalib Mshery alisema wachezaji wote wamekuwa wakihamasishana mazoezini kuhakikisha wanafanya vyema katika mechi zote zilizobakia msimu huu.

“ Kocha Moalin siyo mgeni ndani ya kikosi cha Yanga, hivyo watafuata maelekezo yote kuhakikisha timu inapata ushindi katika mchezo huo muhimu, lakini ratiba imekuwa ngumu kwa kiasi kikubwa kutokana na mechi kufuatana kwa ukaribu,”alisema.

Naye Kocha wa Coastal Union, Fikiri Elias alisema mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu na wenye upinzani mkali kutokana na uimara uliopo kati ya vikosi hivyo viwili.

 “Tunatambua mchezo utakuwa mgumu na wenye upinzani mkali kutokana na ubora wa vikosi vyote, lakini sisi tunazitaka pointi tatu ili kujinasua katika janga la kushuka daraja,” alisema.

Mchezaji wa Coastal Union, Geofrey Manyasi alisema wachezaji wote wameahidi kupambana na kupata ushindi japokuwa watachezea ugenini.

Jana, Azam FC ilichapwa mabao 4-1 na TRA United katika pambano lililopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.

Katika hatua nyingine, Singida Black Stars itaikaribisha Mtibwa Sugar huku JKT Tanzania ikipepetana na Mbeya City.

Katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga ipo kileleni ikiwa na pointi 51 huku Coastal Union ikishikilia nafasi ya 12 kwa pointi 22, timu zote zimeshacheza mechi 21 kila mmoja.

Previous Post

MWIGULU ATAJA MWAROBAINI MAFURIKO DARAJA LA DUMILA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA AWALILIA WATUMISHI WALIOFARIKI AJALI YA BOTI KIGOMA

RAIS DK. SAMIA AWALILIA WATUMISHI WALIOFARIKI AJALI YA BOTI KIGOMA

2 months ago
VYAMA 18 Z’BAR VYASAINI FOMU KUELEKEA UCHAGUZI

VYAMA 18 Z’BAR VYASAINI FOMU KUELEKEA UCHAGUZI

9 months ago

Popular News

  • MTIHANI MZITO KWA MOALIN

    MTIHANI MZITO KWA MOALIN

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU ATAJA MWAROBAINI MAFURIKO DARAJA LA DUMILA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA ATIA NENO BEI MAFUTA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA MBELE KWA MBELE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WATAALAMU WAFUNGUKA MITAZAMO YA MIKATABA 8

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?