• ePaper
Friday, May 8, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MWIGULU ATAJA MWAROBAINI MAFURIKO DARAJA LA DUMILA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 8, 2026
in Habari, Kitaifa
0
MWIGULU ATAJA MWAROBAINI MAFURIKO DARAJA LA DUMILA
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ATHNATH MKIRAMWENI

WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, ameagiza mamlaka husika kutafuta suluhu ya kudumu ya changamoto ya mchanga unaoziba eneo la Daraja la Dumila, wilayani Kilosa, akisema hatua za muda mfupi hazitoshi.

Akizungumza katika ziara yake, mkoani Morogoro katika eneo hilo, Dk. Mwigulu alisema hali ya daraja hilo imekuwa hatarishi kutokana na mchanga mwingi unaokusanyika kila msimu wa mvua kuhatarisha mawasiliano ya barabara hiyo muhimu.

Alisema haiwezekani serikali kuendelea kutumia fedha nyingi kila mwaka kuondoa mchanga, huku tatizo likijirudia mara kwa mara bila kupatikana suluhisho la kudumu.

“Tunataka jawabu la kudumu, siyo kuendelea kutumia fedha kila mwaka halafu mvua ikinyesha tatizo linarudi tena,” alisema.

Dk. Mwigulu alieleza daraja hilo ni muhimu kwa kuwa linaunganisha si tu mikoa ya Tanzania bali nchi jirani, hivyo ni lazima lichukuliwe hatua za haraka kabla ya madhara makubwa kutokea.

Aliwataka viongozi wa Wakala wa Barabara  Vijijini na Mijini(TARURA) na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na mamlaka za serikali za mitaa kukaa pamoja na kuweka utaratibu wa haraka wa kuondoa mchanga.

Pia, aliagiza wananchi na wadau wanaohitaji mchanga kuruhusiwa kuchukua bure katika maeneo yatakayoelekezwa rasmi, kusaidia kupunguza gharama za serikali.

“Badala ya kuzuia watu wanaohitaji mchanga, waelekezeni sehemu sahihi wachukue bure, ili mchanga uondoke na daraja letu libaki salama,” alisisitiza.

Alisema hakuna sababu ya serikali kuendelea kuingia gharama kubwa za kuondoa mchanga wakati wananchi wanaweza kusaidia kufanya kazi hiyo kwa manufaa ya wote.

Alisema serikali imekuwa ikitumia mamilioni ya shilingi kila mwaka kufanya shughuli za kusafisha eneo hilo.

Dk. Mwigulu aliagiza ndani ya siku mbili viongozi husika waitishe kikao na wadau wote kuweka mipaka na utaratibu wa kitaalamu wa uchimbaji kuhakikisha nguzo za daraja haziharibiwi.

“Eneo linalosumbua waruhusuni watu waondoe mchanga bure, ndani ya siku mbili wadau wote waitwe muwaelekeze maeneo ya kutoa mchanga huo. Malizeni hili Jumatatu muwe mmewaelekeza wanachimba wapi,” alisema.

Dk. Mwigulu alisema hatua hiyo itasaidia kulinusuru daraja hilo dhidi ya mafuriko yanayoweza kulisababisha kupoteza uwezo wake wa kuhudumia wananchi.

Akiwa Morogoro, Dk. Mwigulu alisikiliza changamoto mbalimbali zikiwemo za migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji, dhuruma za fedha.

KABUDI, MALIMA

Kwa upande wake, Mbunge wa Kilosa, Profesa Palamagamba Kabudi alisema mji wa Dumila unakua na idadi ya watu inaongezeka lakini bado wanakabiliwa na changamoto ya maji.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima alimshukuru Dk. Mwigulu kufika kukagua usalama na uhai wa daraja la mto Mikumi.

“Daraja hili ni la kimkakati sana na tunakwenda tukilitunza kama mboni ya jicho kwa sababu likipata madhara, upande huu wa Tanzania kwenda huko mbele unakatika wote, hivyo tumekaa tunaliangalia.

“Mchanga katika daraja umejaa sana kutokana na shughuli za kilimo zinazofanyika japo tumekuwa tukiutoa lakini bado unaendelea kujaa,” alisema.

Previous Post

RAIS DK. SAMIA ATIA NENO BEI MAFUTA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

PBPA YAAGIZWA KUHARAKISHA UPOKEAJI NA USAZAMBAZAJI WA MAFUTA NCHINI

PBPA YAAGIZWA KUHARAKISHA UPOKEAJI NA USAZAMBAZAJI WA MAFUTA NCHINI

1 month ago
UWANJA WA BENJAMIN MKAPA WAFIKIA 90%

UWANJA WA BENJAMIN MKAPA WAFIKIA 90%

5 months ago

Popular News

  • MWIGULU ATAJA MWAROBAINI MAFURIKO DARAJA LA DUMILA

    MWIGULU ATAJA MWAROBAINI MAFURIKO DARAJA LA DUMILA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA ATIA NENO BEI MAFUTA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA MBELE KWA MBELE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WATAALAMU WAFUNGUKA MITAZAMO YA MIKATABA 8

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AKEMEA VIONGOZI ‘KUVIMBA’

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?