• ePaper
Friday, May 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

NI KISASI SIMBA QUEENS,YANGA LEO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 15, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
NI KISASI SIMBA QUEENS,YANGA LEO
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

NASRA KITANA na AMINA   KASHEBA

MIAMBA ya soka la wanawake, Simba  Queens na Yanga Princess, leo zinashuka dimbani kuumana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Bara.

Pambano hilo, limepangwa kufanyika saa 11.00 jioni katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Katika msimamo wa ligi, Simba Queens inaongoza ikiwa na pointi 43 wakati Yanga Princess ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 39, timu zote zimecheza mechi 15.

Simba Queens itacheza pambano hilo huku ikiwa na kumbukumbu ya kuifunga Yanga Princess mabao 2-0, katika mchezo uliofanyika Desemba 28, mwaka jana katika dimba hilo hilo la Azam Complex.

Hadi sasa, Simba Queens inashikilia rekodi ya ligi ya wanawake kwa kutwaa ubingwa mara tano ikiwa sawa na JKT Queens.

Rekodi zinaonesha kuwa mechi zote zilizoikutanisha Simba Queens na Yanga Princess kuanzia mwaka 2019 hadi kufikia 2026, katika Ligi Kuu ya Wanawake na Ngao ya Jamii, timu hizo zimecheza mara 13.

Simba Queens imeshinda mechi saba wakati Yanga Princess ikishinda michezo miwili.

Timu hizo kwa kipindi hicho, zimefanikiwa kutoka sare mara nne na kufanya mchezo wa leo kuwa na ushindani mkubwa.

Kocha wa Simba Queens, Mussa Hassan ‘Mgosi’ alisema kikosi chake kimejiandaa kikamilifu kuibuka na  ushindi na kujiwekea mazingira mazuri ya kubeba ubingwa.

Mgosi, mshambuliaji wa zamani wa Simba (wanaume), alisema mchezo utakuwa mgumu kutokana na ushindani uliopo katika harakati za kuwania ubingwa msimu huu.

“Simba ina malengo ya kubakiza taji,  hatuwezi kuchukua ubingwa kwa kufungwa, hivyo nimeiandaa timu  kupata ushindi muhimu,” alisema Mgosi.

Kocha huyo alisema anatambia rekodi ya kuifunga timu hiyo pinzani inayonolewa na mchezaji wa zamani wa Yanga Princess na timu ya taifa,   Edna Lema.

“Tangu nilipoanza kuifundisha Simba Queens , Yanga haijawahi kukifunga kikosi changu, sina shaka na uwezo wa wachezaji ambao wana uzoefu mkubwa katika ligi ya ndani na michuano ya kimataifa,” alisema Mgosi.

 Alisema katika mchezo wa leo, ana uhakika kuwa Simba Queens itaendeleza rekodi.

Nyota wa Simba Queens, Aisha Mnunka, alisema kiufundi walimu wamemaliza kila kitu, kilichobaki ni wachezaji kutekeleza jukumu lao uwanjani na kuzipigania alama tatu.

Aisha alisema katika mchezo wa mzunguko wa kwanza walifanikiwa kupata ushindi, hivyo wana imani wapinzani  watakuja tofauti, wao hawatakubali kupoteza.

“Tunajua utakuwa mchezo mgumu lakini tutaingia uwanjani kwa kuwaheshimu wapinzani wetu na kuondoa hofu ya mchezo huo ili kuendeleza ushindi wetu,” alisema Aisha.

Kocha Msaidizi wa Yanga Princess, Said Maulid alisema maandalizi yao yamekamilika kuelekea mchezo huo kwani malengo yao ni kulipa kisasi.

Alisema mchezo huo huenda ukawa mgumu kutokana na ukubwa wake na kila timu inahitaji kuonyesha ubabe kwa mpinzani.

“Utakuwa mchezo mgumu lakini hatutakubali kupoteza, tumefanya kazi kasoro zote zilizojitokeza ili tufanyevizuri na kupunguza idadi ya pointi dhidi ya wapinzani,” alisema Said.

Mchezaji wa Yanga Princess, Maimuna Hamis, alisema wachezaji wote wako imara na mchezo huo ni muhimu kwa ajili ya kuwapa mwanga katika mbio za ubingwa.

Alisema watatumia mbinu ambazo walimu wamewapatia ili waweze kupata matokeo chanya.

“Kila mchezaji ana morari ya kutosha kuelekea mchezo huo muhimu, tumejiandaa vyema kwani lengo ni kupata ushindi,” alisema Maimuna.

TFF YATOA NENO

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania  (TFF), Clifford Ndimbo alisema mchezo huo wa watani wa jadi hautakuwa na kiingilio.

“Utakuwa mchezo wenye ushindani mkubwa kwani kila mmoja anahitaji kupata pointi tatu kwa ajili ya kuhakikisha kuwa nafasi nzuri katika msimamo,” alisema.

Previous Post

YANGA YAGEUZA KIBAO

Next Post

MTIFUANO MKALI NNE BORA LIGI KUU TANZANIA BARA

Next Post
MTIFUANO MKALI NNE BORA LIGI KUU TANZANIA BARA

MTIFUANO MKALI NNE BORA LIGI KUU TANZANIA BARA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WAKUU WA VYOMBO VYA HABARI NA WAHARIRI WAANDAMIZI NCHINI, WATOA MAAZIMIO WATANZANIA KUTUNZA AMANI

WAKUU WA VYOMBO VYA HABARI NA WAHARIRI WAANDAMIZI NCHINI, WATOA MAAZIMIO WATANZANIA KUTUNZA AMANI

7 months ago
SIMBA, YANGA AKILI ZOTE KIMATAIFA

SIMBA, YANGA AKILI ZOTE KIMATAIFA

8 months ago

Popular News

  • MTIFUANO MKALI NNE BORA LIGI KUU TANZANIA BARA

    MTIFUANO MKALI NNE BORA LIGI KUU TANZANIA BARA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NI KISASI SIMBA QUEENS,YANGA LEO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA YAGEUZA KIBAO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NEEMA YAWASHUKIA WAVUVI NA WAFUGAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KIHONGOSI AKEMEA ‘WANAOVIMBA’ CCM

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?