• ePaper
Wednesday, June 24, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

YANGA, AZAM FC HAIJAISHA HADI IISHE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
June 23, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
YANGA, AZAM FC HAIJAISHA HADI IISHE
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na AMINA KASHEBA

NI dhahiri kuwa mechi ya Yanga dhidi ya Azam FC bado haijaisha, kwani timu hizo bado zina kibarua kingine zitakapopambana katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga na Azam FC zitapepetana tena kesho, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaopigwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Vigogo hivyo vitapambana ikiwa ni siku tatu baada ya Yanga kukubali kipigo cha mabao 3-2, katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (FA), iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita, katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Kipigo cha Yanga

Macho na masikio kutoka kwa mashabiki wa timu hizo, wadau wa soka ni kuona kama  Yanga inayotetea taji la Ligi Kuu itakubali tena kichapo au  itashinda mechi hiyo muhimu dhidi ya Azam na kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa.

 Katika msimamo wa ligi, Yanga inaongoza ikiwa na pointi 66 huku mtani wake wa jadi, Simba, ikiwa na alama 64, zikitofautiana kwa alama mbili.

Kama Yanga itapoteza mchezo dhidi ya Azam  huku Simba ikashinda mchezo ujao dhidi ya Mtibwa Sugar, kuna uwezekano wa kupoteza ubingwa.

Lakini kama Yanga itashinda huku Simba ikipoteza, Yanga itakuwa bingwa, kutokana na hali hiyo, pambano kati ya Azam na Yanga ni la kukata na soka na lazima limalizwe kwa ushindi mnono. 

KAULI YA MOALIN

Kocha wa Yanga, Moalin alisema mechi dhidi ya Azam ni jaribio lingine gumu ambalo linapaswa kujibiwa kwa kupata ushindi na si vinginevyo.

Molanin alisema pamoja na kupoteza mechi ya FA, timu yake si dhaifu kama inavyoelezwa na mashabiki ambao hawaitakii Yanga mema.

Alisema anaamini kuwa makosa yaliyojitokeza katika pambano lililopita hayawezi kujirudia na kikosi chake kipo tayari kujibu mapigo.

“Mchezo uliopita ulikuwa na ushindani mkubwa, yaliyopita yanapaswa kusahaulika na kujipanga kwa kile kilichopo mbele yetu,” alisema Moalin.

“Wachezaji wangu walipata nafasi kadhaa za kufunga, lakini walishindwa kuzitumia vizuri kupata bao, hilo tatizo limechangia kufungwa  na Azam FC, “ aliongeza.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe, alisema haikuwa bahati kwa Yanga kucheza fainali za msimu huu hivyo nguvu zote zimeelekezwa katika mechi zilizobaki za ligi.

“Timu ilicheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga, ilirudisha mabao ya utangulizi lakini bahati haikuwa upande wetu,” aliongeza Kamwe.

 TAMBO ZA IBENGE

Kocha wa Azam FC, Florent Ibenge,  alisema ni muda wa kukiongoza tena kikosi chake kupata matokeo mazuri dhidi ya Yanga.

Ibenge alisema wachezaji wake wapo katika hali nzuri na jana waliendelea na mazoezi kujiwinda na mechi nyingine na Yanga.

Nahodha wa Azam, Himid Mao, alisema timu yao ipo tayari kujiuliza tena kwa Yanga.

Mao aliwapongeza wachezaji wenzake kwa kufanya vyema katika mechi iliyopita na kuahidi kutakata tena mbele ya Yanga katika mchezo wa kesho.

Previous Post

MAFANIKIO YA MIAKA 30 TRA, YAGUSA WABUNGE

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. MWIGULU ASHUSHA MAAGIZO YA KAZI NA UTU

DK. MWIGULU ASHUSHA MAAGIZO YA KAZI NA UTU

3 months ago
TASAF ILIVYOCHOCHEA KILIMO, KUBADILI MAISHA YA WANANCHI

TASAF ILIVYOCHOCHEA KILIMO, KUBADILI MAISHA YA WANANCHI

6 months ago

Popular News

  • YANGA, AZAM FC HAIJAISHA HADI IISHE

    YANGA, AZAM FC HAIJAISHA HADI IISHE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA MIAKA 30 TRA, YAGUSA WABUNGE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • HATUTAVUMILIA UHUJUMU WA MIRADI – NDEJEMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA KUZINDUA JENGO LA BILIONI 17/- KCMC

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BODABODA WAKINGIWA KIFUA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?