• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

BIL. 36.6/- ZAPAISHA UCHUMI WA VIJANA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 24, 2025
in Habari, Kitaifa
0
BIL. 36.6/- ZAPAISHA UCHUMI WA VIJANA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka

0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ELIZABETH JOHN 

SERIKALi imeeleza kuwa inaendelea kuchukua hatua madhubuti za kuwawezesha vijana kiuchumi na kijamii kwa kuimarisha ajira, ujuzi, ujasiriamali na matumizi ya teknolojia, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2025–2030.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka, amesema serikali inalenga kuhakikisha vijana wanapata ajira zenye staha, ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko na fursa za kujiajiri kupitia sekta mbalimbali za uzalishaji.

Amesema Ilani ya CCM imeweka lengo la kuzalisha ajira zisizopungua milioni nane katika kipindi cha miaka mitano ijayo kupitia kuongeza uzalishaji, kuvutia uwekezaji na kukuza sekta zenye fursa kubwa kwa vijana.

Amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, aliahidi kwa wananchi katika siku 100 za madarakani atatoa sh. bilioni 200 ambazo zitawasaidia wanawake, vijana na makundi maalumu.

Amesema fedha hizo zitalenga kusaidia miradi ya ujasiriamali, kuongezwa fursa za kiuchumi na kuimarisha ustawi wa makundi hayo.

Amesema halmashauri nchini zimekuwa zikitenga asilimia 10 ya mapato yao ya ndani kwa ajili ya mikopo kwa makundi maalum, ambapo asilimia nne hutengwa mahsusi kwa vijana.

“Katika kipindi cha mwaka 2021 hadi 2025, sh. bilioni 36.64 zimetolewa kwa vijana kupitia halmashauri mbalimbali nchini, ikiwa ni sehemu ya jitihada za serikali kuwawezesha kiuchumi,” amesema.

Ameeleza kuwa fedha hizo zimenufaisha jumla ya vikundi 2,867 vya vijana vinavyojihusisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi, zikiwemo kilimo, ufugaji, ujasiriamali na utoaji wa huduma, kwa lengo la kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa mitaji inayowakabili vijana.

“Katika fedha hizo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Maendeleo ya Vijana, itapata sh. bilioni nane, ambazo zitatumika kwa miradi ya kuwasaidia vijana, ikiwemo mikopo ya kuanzisha biashara ndogo ndogo na mafunzo ya ujuzi wa kazi,” amesema.

Waziri Nanauka ametaja changamoto zinazowakabili vijana kuwa ni pamoja na ukosefu wa ajira, ajira zisizo rasmi na tija, upungufu wa ujuzi na changamoto ya mitaji kwa vijana wajasiriamali na kampuni changa.

“Ili kukabiliana na changamoto hizo, serikali inaendelea kuimarisha utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 (Toleo la 2024) na kuhakikisha kuwa vijana wanaandaliwa vyema na wanapata fursa za kujiajiri na kuajiriwa.

“Mikakati yetu itaelekezwa katika maeneo 13 ya kipaumbele yaliyoainishwa katika sera hiyo, ikiwemo elimu na mafunzo ya ufundi stadi, uvumbuzi na ubunifu, uchumi wa kidijitali, ukuzaji wa ajira, ushiriki wa vijana katika shughuli za kijamii na kiuchumi, uzalendo na maadili, afya na ustawi, malezi na makuzi, taaluma ya maendeleo ya vijana, uongozi, usawa wa kijinsia, mazingira na ujumuishwaji wa vijana wenye ulemavu.

“Pia, serikali inaendelea kuimarisha mifumo ya ajira ndani na nje ya nchi, ikijumuisha ulinzi wa haki za wafanyakazi wanaofanya kazi nje ya nchi, pamoja na kuimarisha programu za mafunzo kazini na uzoefu wa kazi kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Ujuzi (SDL),” amesema.

Amesema serikali kupitia wizara yenye dhamana ya kazi na ajira, inaendelea kuandaa na kuimarisha mikakati ya kuongeza fursa za ajira ndani na nje ya nchi, ikijumuisha uimarishaji wa huduma za ajira, usajili na uidhinishaji wa waajiri na mawakala wa ajira, ulinzi wa haki za wafanyakazi wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi, pamoja na kuimarisha mifumo ya ulinganifu wa ujuzi na mahitaji ya soko.

Waziri huyo alisema serikali pia inaelekeza nguvu katika sekta zenye uzalishaji mkubwa kama kilimo, biashara, madini na uvuvi kwa kuongeza tija, kuongeza thamani ya mazao na kupanua ajira kwa vijana katika mnyororo mzima wa uzalishaji.

Amesema katika sekta ya viwanda, mfumo wa kongani za uwekezaji (TISEZA) unaendelezwa ili kuvutia miradi itakayoongeza ajira na ujuzi kwa vijana.

Amesisitiza kuwa, mwelekeo huo unaenda sambamba na hatua za serikali za kuendeleza programu za uwekezaji zinazoweka vijana katikati, ikiwemo uanzishaji wa mikakati ya vijana kumiliki na kuendesha miradi ya uzalishaji na viwanda vidogo.

Amesema ili kurahisisha upatikanaji wa mitaji, serikali imeanza kuimarisha mifumo ya dhamana ya mikopo kuwezesha vijana wengi zaidi waweze kupata mikopo bila vikwazo vya dhamana.

“Hatua hizi zinakusudia kuongeza uaminifu wa taasisi za fedha kutoa mikopo kwa vijana na kupanua wigo wa upatikanaji wa fedha kwa miradi yenye tija,” alisema.

Amesema katika kuongeza fursa za biashara na soko, serikali inaendelea kusimamia utekelezaji wa Kanuni za Ununuzi wa Umma zinazoelekeza kutengwa kwa asilimia 30 ya bajeti ya ununuzi wa umma kwa ajili ya makundi yenye kipaumbele ikiwemo vijana, wanawake, wazee na watu wenye ulemavu.

“Hii ni fursa muhimu kwa vijana kujenga biashara endelevu kupitia utoaji wa bidhaa na huduma kwa serikali na taasisi zake.

“Serikali inaendelea kuhamasisha na kuratibu mifumo ya fedha na bidhaa za kifedha zinazohusiana na uchumi wa buluu zinazotekelezwa kupitia taasisi za fedha ikiwemo Benki ya CRDB, NMB na upanuzi wa ushirikiano na benki nyingine ili kuwezesha biashara na miradi ya vijana katika sekta za uvuvi, usindikaji, usafirishaji wa bidhaa za baharini na maziwa, pamoja na huduma za bahari na ukanda wa pwani.

“Katika falsafa yetu ya utoaji wa huduma, tumejipanga kuhakikisha serikali inafikika kwa vijana kwa urahisi na kwa wakati, na tunatumia teknolojia kama nyenzo ya msingi ya kuharakisha huduma, kupokea maoni, na kuunganisha vijana na fursa.

“Ndiyo maana tumeanza hatua za kuanzisha jukwaa la kidijitali la huduma jumuishi (Youth Digital One Stop Platform) kuwezesha upatikanaji wa taarifa za ajira, mafunzo, fursa za mikopo, masoko na huduma nyingine kwa namna iliyorahisishwa,”amesema.

Waziri Nanauka alisema serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi, mashirika ya kiraia na wadau wa maendeleo kuhakikisha vijana wanakuwa kitovu cha maendeleo ya taifa na kushiriki kikamilifu katika uchumi wa sasa na wa baadaye.

“Tumeshafanya na tunaendelea kufanya kikao kazi na Maafisa Maendeleo ya Vijana wa Mikoa na Halmashauri katika Mikoa 26 na Halmashauri 184, kuweka uelewa wa pamoja na mwelekeo wa Wizara.

“Napenda kutoa taarifa kuwa Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana ina vituo vitatu vya maendeleo ya vijana, Sasanda (Songwe), Ilonga (Morogoro) na Marangu (Kilimanjaro). Dhamira ya serikali ni kuvifufua na kuviboresha viwe vituo hai vya kutoa ujuzi wa vitendo, kujenga nidhamu, uzalendo na kuwezesha vijana kupata stadi za ujasiriamali na ajira. Katika maboresho hayo, tunalenga pia kuwa na programu maalumu ya ‘Open Coding School’ kuongeza ujuzi wa TEHAMA na uchumi wa kidijitali kwa vijana,” amesema.

Amesisitiza kuwa, utekelezaji wa ajenda hiyo unahitaji ushirikishwaji mpana wa wadau, hivyo serikali itaendelea kujenga ushirikiano na sekta binafsi, mashirika ya kiraia, taasisi za fedha, vyuo na taasisi za utafiti, pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa maendeleo.

Previous Post

SERIKALI KUANZISHA KITENGO MAALUM KUPOKEA MAONI YA WANANCHI SAA 24

Next Post

BARKER APEWA WATATU SIMBA

Next Post
BARKER APEWA WATATU SIMBA

BARKER APEWA WATATU SIMBA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA AMELETA MIRADI MIKUBWA LINDI – MAJALIWA

DK. SAMIA AMELETA MIRADI MIKUBWA LINDI – MAJALIWA

7 months ago
UFAULU MITIHANI KIDATO CHA II, DARASA LA NNE WAONGEZEKA

UFAULU MITIHANI KIDATO CHA II, DARASA LA NNE WAONGEZEKA

3 months ago

Popular News

  • MAFANIKIO YA KISHINDO SGR

    MAFANIKIO YA KISHINDO SGR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NYAMBUI AFUNGUKAAMANI KATIKA MICHEZO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, MBEYA CITY KAZI IPO LEO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AFICHUA KUWA NA KIPAJI CHA SOKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?