• ePaper
Thursday, May 21, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

RAIS DK. SAMIA ATOA AGIZO  KOMBE LA DUNIA 2026

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 19, 2026
in Burudani, Habari, Michezo
0
RAIS DK. SAMIA ATOA AGIZO  KOMBE LA DUNIA 2026
0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan ametoa agizo lingine kwa  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, mamlaka zote zinazohusika na michezo, kuhakikisha zinaiandaa mapema  timu ya wavulana wenye umri chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’.

Agizo hilo limetolewa ikiwa ni wiki moja baada ya kutoa agio kama hilo kwa mamlaka husika, kufanya maandalizi ya mapema kwa timu ya wanawake wenye umri chini ya miaka 20 ‘Serengeti Girls’ iliyofuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia.

Juzi, Serengeti Boys ilifuzu fainali za Kombe la Dunia 2026, zitakazofanyika Disemba, mwaka huu nchini Qatar.

Serengeti Boys ilikata tiketi ya kucheza fainali hizo baada ya kuifunga Angola mabao 3-0,  katika pambano lililopigwa Uwanja wa Mohammed VI football Academy Pitch11, nchini Morocco.

Katika mchezo huo, Tanzania ambayo ipo kundi C,  ikiwa na   Msumbiji, Angola na Mali, ilipata mabao  ya ushindi  kupitia Razaki Juma dakika ya 28 , Hassani Kizinga alifunga bao la pili dakika ya 52 huku bao la tatu likipachikwa wavuni na Sadam Hussein  dakika ya 68.

Taarifa iliyowekwa katika ukurasa wa Instagram wa Rais Samia, wenye wafuasi zaidi ya milioni tatu, Rais Samia alisema anaipongeza timu hiyo kwa kufuzu Kombe la Dunia.

Rais Samia alisema kufuzu kwa timu hiyo kumeonesha wazi uwezo, juhudi na nidhamu ya vijana wa Tanzania katika kuiwakilisha, kuipeperusha vyema bendera ya nchi katika  anga la kimataifa.

“Ninaipongeza  Serengeti Boys kwa kufuzu kushiriki Kombe la Dunia mwaka 2026, mafanikio haya ni fahari kubwa kwa taifa letu na ni ushahidi wa vipaji, juhudi na nidhamu ya vijana wetu katika kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa,” alieleza Rais Samia.

Aidha, Rais Samia ameitakia kila la kheri timu hiyo ya vijana katika maandalizi ya mashindano.

Rais Dk. Samia aliihakikishia timu hiyo ushirikiano na maandalizi bora kutoka serikalini.

Previous Post

DK. YONAZI APOKEA TAARIFA AFUA ZA UKIMWI PWANI

Next Post

 DABI YA TANO YANUKIA

Next Post
 DABI YA TANO YANUKIA

 DABI YA TANO YANUKIA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TANZANIA YASISITIZA KUTUMIA AKILI UNDE KUKABILI MAAFA

TANZANIA YASISITIZA KUTUMIA AKILI UNDE KUKABILI MAAFA

1 week ago
RAIS DK. MWINYI AELEZA FAIDA YA KULINDA TUNU YA AMANI

RAIS DK. MWINYI AELEZA FAIDA YA KULINDA TUNU YA AMANI

2 months ago

Popular News

  • KUDUMISHA SERA YA CHINA MOJA NA KUIMARISHA URAFIKI KATI YA CHINA NA TANZANIA

    KUDUMISHA SERA YA CHINA MOJA NA KUIMARISHA URAFIKI KATI YA CHINA NA TANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, COASTAL HAPATOSHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RIO USIPIME KABISA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AWAPA TABASAMU WAPIGANAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA KICHEKO  

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?