• ePaper
Thursday, September 10, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WAKAGUZI WA CAF WARIDHISHWA NA MAENDELEO YA VIWANJA VYA AFCON 2027

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
June 15, 2026
in Habari, Kitaifa
0
WAKAGUZI WA CAF WARIDHISHWA NA MAENDELEO YA VIWANJA VYA AFCON 2027
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAKAGUZI kutoka Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Lakshmikanth Karunanithi na Eduard Captan, wameeleza kuridhishwa na maendeleo ya maboresho ya miundombinu ya viwanja vinavyotarajiwa kutumika katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) baada ya kufanya ukaguzi wa maeneo mbalimbali yanayoandaliwa kwa ajili ya mashindano hayo.

Katika ziara hiyo, wakaguzi hao wametembelea Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam na kukagua maendeleo ya maboresho ya sehemu ya kuchezea ,maeneo maalumu ya wageni na viongozi mashuhuri (VVIP), pamoja na sehemu zitakazotumika na wanahabari wakati wa mashindano.

Aidha,wametembelea  viwanja vya mazoezi vya Gymkhana II na Faras vinavyoandaliwa kuhudumia timu zitakazoshiriki AFCON 2027. Wakaguzi hao walipata fursa ya kujionea hatua mbalimbali za utekelezaji wa maboresho yanayoendelea katika viwanja hivyo.

Baada ya ukaguzi huo, wakaguzi wa CAF wamebainisha  kuwa kasi ya utekelezaji wa maboresho pamoja na maendeleo ya ujenzi wa miundombinu hiyo yanaonesha dhamira ya kuhakikisha viwanja vinakidhi viwango vinavyohitajika kwa ajili ya mashindano hayo makubwa ya soka barani Afrika.

Vilevile,Ukaguzi huo ni sehemu ya tathmini ya mara kwa mara inayofanywa na CAF kufuatilia maandalizi ya nchi mwenyeji kuelekea AFCON 2027 na kuhakikisha miundombinu yote inakamilika kwa ubora na kwa wakati.

Previous Post

MKAKATI KUDHIBITI VIFO WAJAWAZITO WAANIKWA

Next Post

WABUNGE WAPONGEZA UWEKEZAJI KLICL

Next Post
WABUNGE WAPONGEZA UWEKEZAJI KLICL

WABUNGE WAPONGEZA UWEKEZAJI KLICL

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA KIWANDA CHA NGUZO ZA ZEGE TABORA, UZALISHAJI WAANZA RASMI

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA KIWANDA CHA NGUZO ZA ZEGE TABORA, UZALISHAJI WAANZA RASMI

6 months ago
DK. SAMIA ASISITIZA VIJANA KULINDA AMANI

DK. SAMIA ASISITIZA VIJANA KULINDA AMANI

11 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA, NDEJEMBI TURUFU YA MAENDELEO KWA WATANZANIA

    RAIS DK. SAMIA, NDEJEMBI TURUFU YA MAENDELEO KWA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI AONYA, ATOA SIKU 60 WENYE SILAHA HARAMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NDEJEMBI MZIGONI RASMI, AKEMEA KAZI KWA MAZOEA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUME MIPANGO, NIRC WAJADILI UBORA MIRADI YA UMWAGILIAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MASAUNI AANIKA UMAHIRI WA TANZANIA INAVYOLINDA UDONGO, MATUMIZI MBOLEA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?