• ePaper
Wednesday, June 17, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WABUNGE WAPONGEZA UWEKEZAJI KLICL

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
June 15, 2026
in Habari, Kitaifa
0
WABUNGE WAPONGEZA UWEKEZAJI KLICL
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WABUNGE wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamepongeza uwekezaji uliofanywa na Serikali kupitia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) katika Kiwanda cha Kimataifa cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro (KLICL).

Pongezi hizo zimetolewa na Waheshimiwa Wabunge mbalimbali wakati wa semina iliyoandaliwa na Wizara ya Kazi, Ajira na Mahusiano mahususi kwa PSSSF na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika maeneo ya uwekezaji na huduma.

“Uwekezaji huu katika KLICL ni bora na kiwanda hiki ni kikubwa kuliko chochote katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, tuhakikishe tunakuwa na bidhaa bora sokoni na kiwanda kiendeshwe kibiashara” alishauri Mhe. Mabula Mgangila, Mbunge wa Msalala.

Kiwanda cha KLICL kipo mjini Moshi na kinamilikiwa na PSSSF (86%) na Jeshi la Magereza (14%) na kimeajiri watu 294. Aidha, hadi sasa Serikali imewekeza jumla ya TZS 142 bilioni.

Kwa upande wake, Mbunge Jackson Kiswaga (Kalenga) alipongeza taasisi za umma, PSSSF kwa uwekezaji mzuri kwenye kiwanda na NSSF kwa kuendesha ‘Skimu ya Hifadhi’ katika viwango vinavyokubalika.

Kwa upande wake, Mbunge Rashidi Shangazi (Mlalo) pamoja na pongezi alishauri sekta binafsi ikaribishwe katika uendeshaji wa kiwanda ili kuongeza nguvu katika masoko na uzalishaji.

Akifafanua kuhusu hoja mbalimbali za Wabunge, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Fortunatus Magambo alisema kiwanda kinatoa elimu ya madhara ya uwekaji chapa mifugo na uchunaji usio bora.

“Mifugo ikiwa na chapa na ikichunwa vibaya thamani ya ngozi hupunguza kipato kwa mfugaji,” amesema Mkurugenzi Mkuu Magambo akifafanua kuhusu hatua zinazochukuliwa na kiwanda ili kupata ngozi bora.

Akizungumza kuhusu ushirikiano na sekta binafsi, Bw. Magambo alisema kiwanda na PSSSF zipo tayari kufanya kazi na sekta binafsi.

“Tunawakaribisha sekta binafsi waje tushirikiane kuendesha kiwanda hiki, hivyo mwenye mawazo na uwezo wa kushirikiana nasi anakaribishwa wakati wowote,” amesema Magambo.

Awali akitoa neno la utangulizi katika semina hiyo, Waziri wa Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu alisema lengo la kuendesha semina hiyo ni kuwajengea uelewa wabunge kuhusu fursa zilizopo KLICL na faida za ‘Skimu ya Hifadhi’.

Previous Post

WAKAGUZI WA CAF WARIDHISHWA NA MAENDELEO YA VIWANJA VYA AFCON 2027

Next Post

WABUNGE WAIPONGEZA NSSF NA PSSSF KWA KUANZISHA SKIMU YA HIFADHI KWA WALIOJIAJIRI NA UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA NGOZI

Next Post
WABUNGE WAIPONGEZA NSSF NA PSSSF KWA KUANZISHA SKIMU YA HIFADHI KWA WALIOJIAJIRI NA UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA NGOZI

WABUNGE WAIPONGEZA NSSF NA PSSSF KWA KUANZISHA SKIMU YA HIFADHI KWA WALIOJIAJIRI NA UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA NGOZI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SERIKALI YAIPA TANO YANGA

SERIKALI YAIPA TANO YANGA

9 months ago
MKWASA, MTEMI WACHOMBEZA TAIFA STARS

MKWASA, MTEMI WACHOMBEZA TAIFA STARS

7 months ago

Popular News

  • WABUNGE WAIPONGEZA NSSF NA PSSSF KWA KUANZISHA SKIMU YA HIFADHI KWA WALIOJIAJIRI NA UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA NGOZI

    WABUNGE WAIPONGEZA NSSF NA PSSSF KWA KUANZISHA SKIMU YA HIFADHI KWA WALIOJIAJIRI NA UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA NGOZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WABUNGE WAPONGEZA UWEKEZAJI KLICL

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAKAGUZI WA CAF WARIDHISHWA NA MAENDELEO YA VIWANJA VYA AFCON 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MKAKATI KUDHIBITI VIFO WAJAWAZITO WAANIKWA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WASOMI, WANASIASA WAKOSHWA TOZO KUCHANGIA BIMA YA AFYA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?