• ePaper
Thursday, May 21, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

RAIS DK. SAMIA AWAPA TABASAMU WAPIGANAJI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 20, 2026
in Habari, Kitaifa
0
RAIS DK. SAMIA AWAPA TABASAMU WAPIGANAJI
0
SHARES
22
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MUSSA YUSUPH, Dodoma

AMIRI Jeshi Mkuu, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha tabasamu kwa mashujaa waliopigana Vita ya Kagera, kufuatia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, kutangaza mpango wa kuwaingiza katika malipo ya pensheni.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dk. Samia ya kutaka wazee hao kuingizwa katika malipo hayo ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao katika taifa.

Akihitimisha hoja ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027, bungeni jijini, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Rhimo Nyansaho, alisema wapiganaji walioshiriki Vita ya Kagera walikuwa katika makundi matatu.

Aliyataja makundi hayo ni wanajeshi waliokuwa jeshini wakati wa vita, wananchi waliojitolea kupigania nchi na mgambo walioshiriki ulinzi wa taifa.

“Wizara imekamilisha kuwatambua na kuandaa utaratibu wa kuingiza katika daftari la pensheni wazee waliopigana Vita ya Kagera, hatua inayolenga kuwatambua rasmi na kuwahudumia kwa heshima stahiki kutokana na mchango wao katika ulinzi wa nchi,” alieleza.

Amefafanua baada ya kumalizika vita, baadhi ya wapiganaji hao walipata nafasi katika vyombo vya ulinzi na usalama, wengine walikosa sifa za ajira kwa wakati huo kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo majeraha waliyopata katika uwanja wa mapambano.

Dk. Nyansaho alisema katika kipindi hicho, serikali kupitia uongozi wa wakati huo ilitoa sh. 5,000, malipo yaliyofahamika kama “Ahsante Nyerere” kwa baadhi ya waliokuwa wapiganaji, hatua iliyolenga kuonesha shukurani kwa mchango wao.

Hata hivyo, Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dk. Samia alitoa maagizo kwa Wizara ya Ulinzi kufanya tathmini kuhakikisha wazee hao wanatambuliwa rasmi na kuingizwa katika mfumo wa pensheni kama sehemu ya kuthamini mchango wao kwa taifa.

Vita ya Kagera vilipiganwa baina ya Tanzania na Uganda kuanzia mwaka 1978 hadi mwaka 1979.

Vita hiyo ilianza baada ya majeshi ya Uganda chini ya aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo, Diktekta Idd Amin, kuvamia Mkoa wa Kagera na kusababisha vifo, uharibifu wa mali na kuwafanya wananchi wengi kukimbia makazi yao.

Kufuatia uvamizi huo, Tanzania chini ya uongozi wa Rais wa Awamu ya Kwanza, Hayati Julius Nyerere ilipeleka majeshi yake kupambana dhidi ya majeshi ya Uganda.

Baada ya kuondoa wanajeshi wa Uganda eneo la Kagera, Tanzania iliendelea na operesheni hadi ndani ya Uganda kwa kushirikiana na makundi ya wapinzani wa Idd Amin.

Hatimaye, Aprili mwaka 1979 Mji Mkuu wa Uganda, Kampala uliangukia chini ya majeshi ya Tanzania ambapo Idd Amin aliondolewa madarakani na kukimbilia uhamishoni.

VIPAUMBELE

Katika hatua nyingine, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), imeanisha vipaumbele vinane inavyotarajia kuvitekeleza katika mwaka wa fedha 2026/2027.

Vipaumbele hivyo ni pamoja na kuliimarisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa zana, vifaa vya kisasa, kiteknolojia, mawasiliano na rasilimali watu.

Pia, imesema hali ya mipaka ya nchi yenye urefu wa kilometa 5,923.41 ambayo inahusisha eneo la nchi kavu, anga na maji ambapo vyombo vya ulinzi vimeendelea kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha ulinzi na usalama katika mipaka hiyo.

Akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/2027 bungeni jijini hapa jana, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Rhimo Nyansaho, alisema hakuna matukio yaliyoashiria uvunjifu wa amani baina ya Tanzania na nchi inazopakana nazo.

Alisema katika mwaka wa fedha 2026/2027, wizara yake itatekeleza majukumu mbalimbali kwa kuzingatia maeneo nane ya vipaumbele.

Alibainisha kipeumbele cha kwanza ni kuliimarisha jeshi kwa zana na vifaa vya kisasa, kiteknolojia, mawasiliano na rasilimali watu.

Pia, alisema kipaumbele cha pili ni kuendelea kuweka mazingira mazuri ya utendaji kazi kwa wanajeshi ikiwemo kutunza vifaa na zana, mazoezi, mafunzo, maslahi, huduma za afya na makazi.

“Kuendelea kuimarisha uwezo wa Jeshi la Kujenga Taifa kwa kuboresha miundombinu, ili liweze kuchukua vijana wengi zaidi watakaopata mafunzo ya awali ya kijeshi na stadi za kazi,” alibainisha.

Dk. Nyansaho alisema vipaumbele vingine ni kuendelea kuliimarisha Jeshi la Akiba, kuendelea kulinda miradi ya kimkakati kwa maslahi mapana ya taifa, kuimarisha mashirika na taasisi za utafiti wa masuala ya kijeshi, kuanzisha viwanda vipya katika sekta ya ulinzi vitakavyozalisha bidhaa kwa matumizi ya kijeshi na kiraia.

Pia, alisema vipaumbele vingine ni kuanzisha viwanda vipya kwa kushirikiana na sekta binafsi, kuimarisha ushirikiano na Umoja wa Mataifa (UN) Umoja wa Afrika (AU) Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na kati ya nchi na nchi katika masuala ya ulinzi.

Kadhalika, alisema wizara yake itaendelea kushirikiana na mamlaka za kiraia katika kukabiliana dhidi ya majanga na dharura inapohitajika.

HALI YA MIPAKA

Waziri huyo alisema katika mwaka huu wa fedha, hali ya mipaka ya nchi yenye urefu wa kilometa 5,923.41, ambayo inahusisha eneo la nchi kavu, anga na eneo la maji, vyombo vya ulinzi vimeendelea kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha ulinzi na usalama katika mipaka hiyo.

“Mipaka ya nchi kavu ni baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Kenya, Malawi, Msumbiji, Rwanda, Uganda, Zambia na mipaka ya Bahari ya Hindi inayojumuisha nchi za Comoros na Shelisheli.

“Katika kipindi husika hapakuwa na matukio yaliyoashiria uvunjifu wa amani baina ya nchi yetu na nchi tunazopakana nazo. Hata hivyo, zimekuwepo changamoto kadhaa za kiulinzi na kiusalama katika baadhi ya mipaka ikiwemo uharibifu wa alama za mipakani, ukosefu wa barabara za ulinzi kwa baadhi ya mipaka na nyingine kuharibika pamoja na migogoro ya ndani katika baadhi ya nchi tunazopakana nazo,” alisisitiza.

MAONI YA KAMATI

Akiwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge, Ulinzi na Usalama, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Najma Giga, alisema mafunzo ya JKT ni muhimu kwa vijana kwani huwajengea uzalendo, ukakamavu, umoja wa kitaifa na stadi za maisha na kazi.

Hata hivyo, alisema kamati inashauri serikali iongeze nafasi za vijana kujiunga JKT kwa kuongeza uwezo wa kambi na kuboresha miundombinu ya mafunzo.

“Aidha, mafunzo ya stadi za kazi yaendane na mahitaji halisi ya soko la ajira, sambamba na kuanzisha mfumo wa ufuatiliaji wahitimu ili kupata mrejesho wa matokeo ya mafunzo hayo,” alisisitiza.

Pia, alisema hatua ya taasisi za ulinzi kuongeza matumizi ya nishati safi, kuzalisha mkaa banifu na kutengeneza mitambo ya gesi vunde, ni ya kupongezwa kwa kuwa inasaidia kupunguza matumizi ya nishati chafu, kulinda mazingira na kuwapa ujuzi vijana walipo katika mafunzo ya JKT.

Previous Post

KOCHA SIMBA KICHEKO  

Next Post

RIO USIPIME KABISA

Next Post
RIO USIPIME KABISA

RIO USIPIME KABISA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DEPU, OKELLO WAMOTO, YANGA IKISHINDA 6-0

DEPU, OKELLO WAMOTO, YANGA IKISHINDA 6-0

4 months ago
DK. NCHIMBI : WANANCHI MIKOA 11 KUMPA RAHA DK. SAMIA

DK. NCHIMBI : WANANCHI MIKOA 11 KUMPA RAHA DK. SAMIA

8 months ago

Popular News

  • KUDUMISHA SERA YA CHINA MOJA NA KUIMARISHA URAFIKI KATI YA CHINA NA TANZANIA

    KUDUMISHA SERA YA CHINA MOJA NA KUIMARISHA URAFIKI KATI YA CHINA NA TANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, COASTAL HAPATOSHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RIO USIPIME KABISA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AWAPA TABASAMU WAPIGANAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA KICHEKO  

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?