• ePaper
Thursday, May 21, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

KOCHA SIMBA KICHEKO  

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 19, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
KOCHA SIMBA KICHEKO  
0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na AMINA KASHEBA

KOCHA wa Simba, Steve Barker, viwango vinavyoendelea kuonyeshwa na wachezaji wake vinamfanya kutembea kifua mbele na kuwa na uhakika wa kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho (FA).

Barker ametoa kauli hiyo saa chache baada ya kuiongoza Simba kuibuka na ushindi wa mabao 4-0, dhidi ya TRA, katika mechi ya robo fainali iliyochezwa Uwanja wa KMC, Dar es Salaam.

Ushindi huo wa kishindo umeipeleka Simba  hatua ya nusu fainali ambayo itapambana na Coastal Union, mchezo utaofanyika Juni 20, mwaka huu, katika dimba la Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Mabao ya Simba yalifungwa na Clatous Chama  dakika ya sita, Anicet Oura dakika ya 26 wakati Selemani Mwalimu alifunga dakika ya 64 na Bashiri Kibaila alimalizia bao la ushindi dakika ya  78.

Akizungumza baada ya mchezo, kocha huyo alisema katika siku za hivi karibuni, wachezaji wake wamekuwa wakionesha viwango vya juu na kupata ushindi ambao unamshangaza.

Alisema pamoja na kukabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa timu pinzani, Simba bado ipo imara na inajua jinsi ya kubadili michezo yake na kupata matokeo mazuri

“TRA United sio timu ndogo, ina kikosi bora lakini ubora wa wachezaji wangu umeizidi timu hiyo ambayo imekuwa ikitoa upinzani mkali Ligi Kuu na FA,” alisema.

 Aliongeza kuwa, baada ya kufuzu nusu fainali, anakiandaa kikosi chake kufanya vyema katika hatua hiyo na kukata tiketi ya kucheza fainali.

“Nimefurahi kuona kila mchezaji anafanya kazi yake na kuonesha kiwango kizuri, David Kameta ‘Duchu’ amekuwa mchezaji bora katika mchezo, pia nimefurahishwa na kiwango cha Bashiri Kibaila ambaye amefunga bao la nne,” alisisitiza.

Meneja  Habari na Mawasiliano  Simba, Ahmed Ally, alisema benchi la ufundi linakwenda kujipanga kujipanga upya kuelekea hatua ya nusu fainali.

“Tunaenda kujipanga kuikabili Coastal Union , tunajua timu hiyo ina wachezaji wenye uzoefu mkubwa, tupo tayari kufika fainali,” alitamba  Ally.

Kocha wa TRA United, Etienne Ndayiragije, aliipongeza Simba kwa kucheza vizuri na kupata ushindi.

“Nashukuru Mungu hakuna majeruhi hivi sasa, tunajiandaa na mechi za Ligi Kuu baada ya kutolewa FA,” alisema Etienne.

Previous Post

 DABI YA TANO YANUKIA

Next Post

RAIS DK. SAMIA AWAPA TABASAMU WAPIGANAJI

Next Post
RAIS DK. SAMIA AWAPA TABASAMU WAPIGANAJI

RAIS DK. SAMIA AWAPA TABASAMU WAPIGANAJI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

ALAMA TATU KUMUENZI JPM

ALAMA TATU KUMUENZI JPM

2 months ago
WALIOONGOZA KURA ZA MAONI WAPEWA JUKUMU

WALIOONGOZA KURA ZA MAONI WAPEWA JUKUMU

8 months ago

Popular News

  • KUDUMISHA SERA YA CHINA MOJA NA KUIMARISHA URAFIKI KATI YA CHINA NA TANZANIA

    KUDUMISHA SERA YA CHINA MOJA NA KUIMARISHA URAFIKI KATI YA CHINA NA TANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, COASTAL HAPATOSHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RIO USIPIME KABISA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AWAPA TABASAMU WAPIGANAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA KICHEKO  

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?