• ePaper
Monday, May 25, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WAZIRI MKUU AHIMIZA MALEZI YA KIMAADILI NA USHIRIKIANO WA KIJAMII

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 24, 2026
in Habari, Kitaifa
0
WAZIRI MKUU AHIMIZA MALEZI YA KIMAADILI NA USHIRIKIANO WA KIJAMII
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI MKUU, Dk. Mwigulu Nchemba amesema jamii inapaswa kurejea katika misingi ya malezi ya pamoja na uwajibikaji wa kijamii ili kujenga kizazi chenye maadili, kinachoheshimu viongozi, wazazi pamoja na taasisi za jamii.

“Tunataka kujenga jamii inayoguswa na changamoto za wengine. Maadili mema yanaanzia kwenye malezi ya familia na jamii kwa ujumla,” amesema Dk. Mwigulu.

Dk. Mwigulu amesema hayo leo Jumapili, Mei 24, 2026 aliposhiriki Ibada ya Pentekoste katika Kanisa Kuu la KKKT Usharika wa Iringa Mjini iliyoongozwa na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Dk. Blaston Gavile.

Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za dini katika kuimarisha huduma za kijamii, malezi ya maadili na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayogusa maisha ya wananchi.

“Ushirikiano kati ya Serikali na taasisi za dini ni jambo kubwa sana katika maendeleo ya nchi yetu. Shule nyingi kongwe na taasisi mbalimbali za huduma zilianzishwa na taasisi za dini kabla hata ya Serikali kuendelea kuzijenga na kuzisimamia,” amesema Dk. Mwigulu.

Aidha, Waziri Mkuu amesema kuanzia mwaka 2028 Serikali itaanza rasmi utekelezaji wa elimu ya lazima ya miaka 10 kwa watoto wote wa Kitanzania kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha nne kwa lengo la kuongeza ujuzi na kuwajengea vijana uwezo wa kujitegemea.

“Hatusemi shule ya msingi iwe miaka 10, tunasema elimu ya lazima kwa mtoto wa Kitanzania iwe miaka 10 ili watoto wetu wapate maarifa na ujuzi wa kutosha kwa maisha yao ya baadaye,” amesema.

Dk. Mwigulu amesema hatua hiyo pia inalenga kupunguza changamoto za watoto kuacha shule katika umri mdogo pamoja na kukabiliana na changamoto za ndoa za utotoni kwa kuhakikisha watoto wanabaki shuleni kwa muda mrefu zaidi.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amepongeza KKKT Dayosisi ya Iringa kwa kuendelea kuwahudumia watoto yatima na watu wenye mahitaji maalum huku akieleza kuwa Serikali inaendelea kufanya maboresho ya sera na mifumo ya utoaji wa huduma kwa makundi hayo.

Amesema Serikali imeanza kufanya marekebisho ya mfumo wa utoaji wa mikopo kwa watu wenye ulemavu ili hata mtu mmoja mmoja aweze kunufaika badala ya kulazimika kuunda vikundi.

“Tunataka kujenga mfumo unaowatambua watu wenye mahitaji maalum kwa utu wao na kuhakikisha wanapata huduma na msaada stahiki bila usumbufu,” amesema.

Kwa upande wake, Askofu wa KKKT Dayosisi ya Iringa, Dkt. Blaston Gavile amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Waziri Mkuu katika kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi pamoja na kuendelea kusimamia maendeleo ya Taifa kwa karibu.

“Hakika kwa kipindi hiki kifupi tangu kuteuliwa kwako tumeona moyo wako wa kuwatumikia Watanzania. Umetenga muda wako kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua kwa busara, uelewa na hekima kubwa,” amesema Dkt. Gavile.

Aidha, amesema KKKT inaunga mkono maono ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayolenga kujenga uchumi imara, huduma bora za jamii na maendeleo endelevu kwa Watanzania wote.

Previous Post

WAZIRI MKUU AVITAKA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KUWA MACHO DHIDI YA WAVUNJA AMANI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TAIFA STARS, ZAMBIA NI MECHI YA HESHIMA

TAIFA STARS, ZAMBIA NI MECHI YA HESHIMA

8 months ago
DK. MWIGULU AELEZA MCHANGO WA SEKTA YA AFYA KATIKA UKUAJI UCHUMI

DK. MWIGULU AELEZA MCHANGO WA SEKTA YA AFYA KATIKA UKUAJI UCHUMI

2 months ago

Popular News

  • WAZIRI MKUU AHIMIZA MALEZI YA KIMAADILI NA USHIRIKIANO WA KIJAMII

    WAZIRI MKUU AHIMIZA MALEZI YA KIMAADILI NA USHIRIKIANO WA KIJAMII

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI MKUU AVITAKA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KUWA MACHO DHIDI YA WAVUNJA AMANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KILIO CHA BANDO CHATUA BUNGENI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ZIARA YA KIHONGOSI YAACHA NEEMA KWA WANAWAKE MARA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA YAJIPANGA KUDHIBITI MIJI HOLELA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?