• ePaper
Saturday, June 20, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

PACOME, DEPU  WAIPA JEURI YANGA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
June 19, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
PACOME, DEPU  WAIPA JEURI YANGA
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na AMINA KASHEBA

YANGA ni jeuri baada ya Pacome Zouzou na Laurindo Dilson Maria Aurelio ‘Depu’ kuongoza mauaji kwa timu ya Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Pambano hilo, lilipigwa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha ambapo  Yanga ilishinda mabao 2-0, mabao ya ushindi yalipachikwa wavuni na  nyota hao wawili.

Kufuatia ushindi huo, Yanga imefikisha pointi 66 huku Fountain Gate ikibaki na alama zake 29.

Timu zote mbili, hadi leo zimecheza mechi 27 kila moja ambapo Yanga inaongoza ligi hiyo.

Hadi sasa Yanga imebaki na mchezo dhidi ya Azam FC, TRA United na JKT Tanzania huku watani wao wa jadi, Simba imebaki na mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, Singida Black Stars na KMC.

Katika pambano hilo, lilianza kwa kasi na kushambuliana kwa zamu  kwa lengo la kupata bao la kuongoza la mapema.

Dakika ya pili, Fountain Gate ilifanya jaribio la kufunga baada ya mchezaji wake, Juma Issa kupiga shuti lililodakwa na kipa wa Yanga, Djigui Diarra.

Aidha, Fountain Gate ilifanya mashambulizi tena katika lango la Yanga, lakini kipa Diarra alipangua mpira huo na kutoka nje ya uwanja.

Dakika ya tisa Yanga ilipeleka shambulizi katika lango la Fountain Gate, lakini mchezaji wake, Max Nzengeli alipiga shuti kali na mpira ulitoka nje.

Yanga ilifanya jaribio la kufunga dakika ya 35  kupitia nahodha wao, Bakari Mwamnyeto lakini mpira ulipaa juu ya lango.

Dakika ya 45, kipa wa Fountain Gate, Machupa Juma alifanya kazi ya ziada kupangua mpira uliopigwa na mchezaji wa Yanga, Nzengeli.

Kipindi cha pili, Yanga ilirudi na nguvu ya kushambulia kwa nguvu katika lango la Fountain Gate.

Dakika 52 Pacome Zouzoua alifunga bao la kwanza kwa Yanga baada ya kuwatoka walinzi wa Fountain Gate na kupiga shuti kali lilojaa wavuni.

Yanga iliendelea kulisakama lango la Fountain Gate na dakika ya 54 iliandika bao la pili baada ya Depu kupiga shuti lililojaaa wavuni kufuatia kupokea pasi kutoka kwa Allan Okello.

Dakika ya 67, Fountain Gate ilishindwa kufunga bao la kwanza baada ya mchezaji, Elie Mokono kukosa utulivu ndani ya eneo la hatari la Yanga na kupiga shuti lilopaa juu.

Aidha, dakika 90 za nyongeza, timu ya  Fountain Gate ilipata pigo baada ya kipa wao,  Machupa Juma kupata majereha na nafasi yake ilichukuliwa na Mdoe Athumani.

Fountain Gate iliwakilishwa na Machupa Juma, Jimson Mwanuke, Obinna Awara, Derick Mkombozi, Shaaban Pandu, Shabani Mgunda, Ismail Kader, Henry David, Juma Issa/Ramadhan Sadick, Chukwunoye Macdonald na Elie Mokono/Issa Chole.

Yanga: Djigui Diarra, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Maxi Nzengeli, Pacome Zouzoua, Mohamed Hussein, Allan Okello/Edmund John, Kouassi Yao, Mudathir Yahya, Duke Abuya na Laurindo Dilson/Prince Dube.

Previous Post

WABUNGE: AMANI ISICHEZEWE

Next Post

DHAHABU BoT HAIJAUZWA – PM MWIGULU

Next Post
DHAHABU BoT HAIJAUZWA – PM MWIGULU

DHAHABU BoT HAIJAUZWA - PM MWIGULU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

KUKOSA UMAKINI KWAIPONZA YANGA

KUKOSA UMAKINI KWAIPONZA YANGA

3 months ago
TIBA ZA KIBINGWA BENJAMIN MKAPA ZAMVUTIA DK. MWINYI

TIBA ZA KIBINGWA BENJAMIN MKAPA ZAMVUTIA DK. MWINYI

4 months ago

Popular News

  • OFISI YA WAZIRI MKUU YATHIBITISHA NYENZO MUHIMU ZA KUIMARISHA USIMAMIZI WA MAAFA NCHINI

    OFISI YA WAZIRI MKUU YATHIBITISHA NYENZO MUHIMU ZA KUIMARISHA USIMAMIZI WA MAAFA NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KIHONGOSI AWAPONDA VIONGOZI CHADEMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DHAHABU BoT HAIJAUZWA – PM MWIGULU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • PACOME, DEPU  WAIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WABUNGE: AMANI ISICHEZEWE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?