• ePaper
Friday, June 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Uncategorized

‘NAFUU YA MAFUTA KUANZA KUONEKANA JULAI’ NDEJEMBI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
June 26, 2026
in Uncategorized
0
‘NAFUU YA MAFUTA KUANZA KUONEKANA JULAI’ NDEJEMBI
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi amesema Watanzania wataanza kushuhudia kushuka kwa bei za mafuta kuanzia mwezi Julai mwaka huu kufuatia kuanza kushuka kwa bei ya mafuta ghafi katika soko la dunia baada ya kusitishwa kwa mapigano ya Mashariki ya Kati.

Akijibu mwongozo wa Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Subira Mgalu, Bungeni jijini Dodoma leo, Juni 26, 2026, Waziri Ndejembi amesema Serikali imezielekeza EWURA, TPDC na PBPA kuhakikisha manufaa ya kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia yanawafikia walaji nchini.

Amesema licha ya athari za vita kati ya Iran, Israel na Marekani zilizosababisha usumbufu katika usafirishaji wa mafuta kupitia Mlango wa Hormuz, Tanzania iliendelea kuwa na uhakika wa upatikanaji wa mafuta bila kukumbwa na uhaba.

Ndejembi amesema hatua za haraka zilizochukuliwa na Serikali zilihakikisha mafuta yanapatikana katika maeneo yote ya nchi, huku Tanzania ikiendelea kuwa miongoni mwa nchi zenye bei nafuu za mafuta katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Ameeleza kuwa baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano, bei ya mafuta ghafi imeanza kushuka hadi kufikia takribani dola 70 kwa pipa, hali inayotarajiwa kuleta nafuu katika soko la ndani kadri shehena mpya zilizonunuliwa kwa bei ya chini zitakavyoingia nchini.

“Watanzania wataanza kuona punguzo la bei kuanzia mwezi Julai, na kadri shehena mpya za mafuta zilizonunuliwa kwa bei nafuu zitakavyoendelea kuwasili nchini, ndivyo bei zitakavyozidi kushuka,” amesema Waziri Ndejembi.

Aidha, amesema wataalamu wa soko la dunia wanatarajia ndani ya wiki nane hadi 10 bei za mafuta kurejea katika viwango vilivyokuwepo kabla ya kuanza kwa mgogoro huo mwezi Februari mwaka huu.

Waziri Ndejembi ameongeza kuwa Serikali itaendelea kufuatilia mwenendo wa soko la dunia huku ikiimarisha mikakati ya muda mrefu ya kuhakikisha upatikanaji wa mafuta nchini, ikiwemo kuongeza vyanzo vya uagizaji wa mafuta na kuharakisha utekelezaji wa mpango wa ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta mkoani Tanga ili kuimarisha usalama wa nishati nchini.

Previous Post

SERIKALI YAZITAKA TAASISI ZOTE KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL-NINO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA : WANAWAKE TUNA UWEZO KUONGOZA

DK. SAMIA : WANAWAKE TUNA UWEZO KUONGOZA

9 months ago
MAWAZIRI SABA NA MIKAKATI YA KAZI

MAWAZIRI SABA NA MIKAKATI YA KAZI

7 months ago

Popular News

  • ‘NAFUU YA MAFUTA KUANZA KUONEKANA JULAI’ NDEJEMBI

    ‘NAFUU YA MAFUTA KUANZA KUONEKANA JULAI’ NDEJEMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAZITAKA TAASISI ZOTE KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL-NINO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SAMAMBA AWAFUNDA WAKAGUZI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RUNGU ZITO KUWASHUKIA WAWEKEZAJI ‘JANJAJANJA’

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, SIMBA KAZI KAZI UBINGWA LIGI KUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?