• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

WADAU WAMGOMEA SAMATTA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
July 8, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
WADAU WAMGOMEA SAMATTA
0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

VICTOR MKUMBO Na DEUSDEDIT UNDOLE

SIKU chache baada ya nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta kutangaza kustaafu kuichezea timu hiyo, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma, Kocha, Charles Mkwasa, Ismail Aden Rage na Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe wameibuka na kutoa maoni yao.

Samatta alitangaza kupitia mtandao wa Instagram kwamba amestaafu rasmi kuichezea Taifa Stars baada ya kudumu kikosini kwa kipindi cha takribani miaka 15.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma aliandika  kupitia mtandao wa kijamii kuwa “Kapteni asante kwa kila kitu, asante sana hudaiwi na mtu.

“Tuna ombi moja tu watu wa mpira, hatuwezi kushiriki AFCON itakayopigwa nyumbani pamoja? ukiwa dimbani halafu tukujengee mnara wako mkubwa tuache upumzike, tafadhali,”.

Staa wa Stars, Simon Msuva aliandika “Nahodha sina mengi ya kusema kwako wewe ni mtu na nusu umekuwa kiongozi bora sana na ni mfano wa kuigwa, ubarikiwe sana,”.

Kwa upande wa Mkwasa alisema Dar es Salaam,jana, kuwa bado nahodha Samatta anatajika katika kikosi cha Stars licha ya kutangaza kustaafu timu hiyo.

“Binafsi nimeshtuka na hiyo taarifa kwamba Samatta ametangaza tena hivi karibuni kuachana na Taifa Stars. Kama taarifa hizo ni za kweli, basi mimi naomba abatilishe kwani bado anahitajika na ana mchango mkubwa kikosini humo,” Mkwasa.

Alisema mwakani Tanzania kwa kushirikiana na nchi za Kenya na Uganda zitakuwa wenyeji wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), hivyo ni wazi uzoefu, umaarufu na weledi wa Samatta utaisaidia timu kufanya vyema.

Kocha huyo, alisema ni wazi anahitajika ili iwe dira ya kuwaongoza wachezaji wenzake chipukizi na wengineo hodari, ambao wataitwa kikosini humo kwa ajili ya AFCON.

“Ninadhani kikubwa kilichosukuma  Samatta afikie hatua hiyo ni vitendo vya mwendelezo vya kushambuliwa mitandaoni vinavyofanywa na baadhi ya mashabiki, kitu ambacho kinatokea kwa wachezaji wengi siyo yeye pekee,” alisema Mkwasa.

Rage alisema anampongeza Samatta kutokana na uamuzi wake na kwamba ameona kwamba amefikia mwisho na kuwaachia vijana waendelee pale alipoishia.

Alisema Samatta ametumia busara kustaafu na kutoa nafasi kwa wengine japokuwa alikuwa bado anahitajika kikosini.

“Ninampongeza Samatta kwa uamuzi wake na kwamba ninaamini amefanya jambo kwa wakati sahihi, hivyo nina imani vijana wataendelea pale alipoishia yeye,” alisema Rage.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema kuwa ni taarifa ngumu kupokelewa kwa mashabiki na wadau wa soka nchini.

“Siku hii ni sawa na siku Wareno watasikia Cristiano Ronaldo amestaafu timu ya taifa, siku hii haina tofauti na Argentina wakisikia Lionel Messi amestaafu timu yao, siku hii ni sawa na Misri wakisikia Mohamed Salah amestaafu timu ya taifa.

“Maumivu watakayopitia mataifa hayo ndio maumivu tunayopitia Watanzania tunaojua umuhimu, thamani na uwezo wa Samatta.

“Samatta ni kielelezo cha mpira wa Tanzania, unapokwenda kucheza na Ivory Coast wakimuona amesimama mbele wanajua leo mechi ipo kwa sababu wanapishana nae katika viwanja vya Ulaya.

“Hivi sasa ni wakati wa kuzalisha wakina Samatta wengine asante kwa muda wake, asante kwa jasho lake, asante kwa kutufanya tutambe Duniani,” alisema Ahmed.

Ofisa Habari wa Yanga, Kamwe alisema kuwa Samatta alitakiwa kusubiri hadi michuano ya AFCON itakapomalizika msimu ujao na ndipo atangaze kustaafu soka.

Alisema mashabiki wa soka wanastahili kumuaga Samatta kwa heshima na siyo kupitia mitandao ya kijamii kama alivyofanya.

“Samatta anatakiwa asubiri hadi michuano ya AFCON itakapomalizika msimu ujao ndipo afanye maamuzi kwani mashabiki wanahitaji kumuaga kwa heshima kutokana na mazuri aliyoyafanya akiwa Stars,” alisema.

Previous Post

DK. NCHIMBI : DITF 2050 IWE KITOVU CHA UBUNIFU NA BIASHARA ZA KIMATAIFA

Next Post

BIL.8/- KUISUKA AZAM FC

Next Post
BIL.8/- KUISUKA AZAM FC

BIL.8/- KUISUKA AZAM FC

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SERIKALI KUIFANYA TANZANIA KITOVU CHA BIASHARA – DK. YONAZI

SERIKALI KUIFANYA TANZANIA KITOVU CHA BIASHARA – DK. YONAZI

4 months ago
CCM YATAJA VIPAUMBELE VYAKE WILAYA YA KALAMBO

CCM YATAJA VIPAUMBELE VYAKE WILAYA YA KALAMBO

11 months ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?