• ePaper
Sunday, August 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

BIL.8/- KUISUKA AZAM FC

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
July 8, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
BIL.8/- KUISUKA AZAM FC
0
SHARES
11
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

WAKATI Ligi Kuu Tanzania Bara msimu 2025/26 ukiwa umemalizika, uongozi wa klabu ya Azam FC umetangaza bajeti ya sh.bilioni nane kwa ajili ya kusuka kikosi chao cha msimu ujao.

Katika msimu  uliomalizika hivi karibuni, Azam haikuambulia chochote baada ya kumaliza nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 64 na kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho(FA) na kuwa mshindi wa pili baada ya kufungwa na Simba bao 1-0.

Kwa mujibu wa kiongozi mmoja wa timu hiyo, alisema tayari wametenga bajeti hiyo kuhakikisha wanafanya usajili wa viwango vya juu.

Alisema tayari Kocha Mkuu wa timu hiyo, Florent Ibenge ametoa ripoti ya wachezaji ambao wataachwa ndani ya kikosi hicho na wale ambao wataingia kuongeza nguvu msimu ujao.

“Msimu ujao tunataka uwe msimu wa tofauti, tumetenga fedha hiyo kwa ajili ya kuleta wachezaji wapya wenye viwango vikubwa, tutafanya marekebisho ya baadhi ya wachezaji ambao mwalimu anawahitaji na tutawaondoa wale ambao hawakuwa na mchango katika timu,” alisema kiongozi huyo ambaye hakutaka jina lake liwekwe hadharani.

Alipoulizwa jana na mwandishi wa habari hii,msemaji wa timu hiyo, Hasheem Ibwe alisema kama timu wametenga fedha nyingi kuhakikisha wanafanya usajili mzuri.

Alisema hawakuwa na msimu mzuri, lakini hawatakubali msimu ujao kuwa wanyonge tena.

“Tumetenga bajeti kubwa ya kuhakikisha tunamsajili mchezaji yeyote ambaye tunamuhitaji, msimu ujao tunataka uwe msimu bora na kufikia malengo ambayo tumejiwekea,” alisema Ibwe.

Ofisa habari huyo aliwataka mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kuendelea kuwapa sapoti ya kutosha wachezaji wao, wafanye vizuri.

Hata hivyo, tetesi zinaeleza kuwa Azam FC inatarajiwa kuwaacha wachezaji zaidi ya wanane ili kusuka kikosi kipya.

Previous Post

WADAU WAMGOMEA SAMATTA

Next Post

RAIS DK. MWINYI : TAMKO LA PAMOJA CCM NA ACT-WAZALENDO LAFUNGUA NJIA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA

Next Post
RAIS DK. MWINYI : TAMKO LA PAMOJA CCM NA ACT-WAZALENDO LAFUNGUA NJIA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA

RAIS DK. MWINYI : TAMKO LA PAMOJA CCM NA ACT-WAZALENDO LAFUNGUA NJIA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WAZIRI MCHENGERWA AAGIZA UCHUNGUZI HOSPITALI YA TEMEKE

WAZIRI MCHENGERWA AAGIZA UCHUNGUZI HOSPITALI YA TEMEKE

8 months ago
KOCHA SIMBA AIPANIA MASHUJAA

KOCHA SIMBA AIPANIA MASHUJAA

7 months ago

Popular News

  • KIINI DABI KARIAKOO KUPIGWA ZANZIBAR

    KIINI DABI KARIAKOO KUPIGWA ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TAMU, CHUNGU DABI YA K’KOO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AKUTANA NA VIONGOZI WA TEC

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AWAPA RAHA VIGOGO USHIRIKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BILIONI 30/- KUJENGA UWANJA WA KISASA SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?