• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

RAIS DK. MWINYI : TAMKO LA PAMOJA CCM NA ACT-WAZALENDO LAFUNGUA NJIA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
July 9, 2026
in Habari, Kitaifa
0
RAIS DK. MWINYI : TAMKO LA PAMOJA CCM NA ACT-WAZALENDO LAFUNGUA NJIA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA
0
SHARES
9
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Tamko la Pamoja kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ACT-Wazalendo linafungua njia ya utekelezaji wa uundaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kuimarisha amani, umoja, mshikamano na maendeleo ya Zanzibar.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo baada ya kushuhudia utiaji wa saini wa ajenda zilizokubaliwa kwa pande zote mbili kwa ajili ya kufanyiwa kazi kufuatia Tamko la Pamoja la Muafaka wa Kisiasa Zanzibar baina ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ACT-Wazalendo katika Viwanja vya Ikulu Zanzibar leo tarehe 09 Julai, 2026.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi amesema maridhiano hayo yanaonesha dhamira ya viongozi kuweka mbele maslahi ya taifa, huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wote kuhakikisha mchakato huo unadumisha utulivu, utawala bora na maendeleo endelevu.

Halikadhalika, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amepongeza hatua hiyo akieleza kuwa maridhiano hayo yanafungua ukurasa mpya wa kuimarisha umoja, utulivu na mshikamano miongoni mwa Wazanzibari, na ni ishara ya ukomavu wa kisiasa na dhamira ya kujenga mazingira ya amani na maendeleo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Taifa, Mhe. Othman Masoud Othman, amempongeza Rais Dkt. Mwinyi kwa kuendeleza mchakato wa maridhiano, akisema umefungua njia ya kupatikana kwa ufumbuzi wa kudumu wa changamoto za kisiasa Zanzibar.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Makamu wa Rais Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi; Marais Wastaafu wa Zanzibar, Dk. Amani Abeid Karume na Dk. Ali Mohamed Shein; Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla; Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa dini, Viongozi wa Serikali za SMT na SMZ, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Mabalozi, Wawakilishi wa Taasisi za Kimataifa pamoja na wananchi mbalimbali.

Previous Post

BIL.8/- KUISUKA AZAM FC

Next Post

SIMBA, SINGIDA BS MACHO ‘KAGAME CUP’

Next Post
SIMBA, SINGIDA BS MACHO ‘KAGAME CUP’

SIMBA, SINGIDA BS MACHO ‘KAGAME CUP’

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

ICHAGUENI CCM  – DK. MWINYI

ICHAGUENI CCM  – DK. MWINYI

9 months ago
WAZIRI MKUU : WATANZANIA TUNZENI AKIBA YA CHAKULA

WAZIRI MKUU : WATANZANIA TUNZENI AKIBA YA CHAKULA

7 months ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?