• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

KUMEKUCHA ‘SIMBA DAY’ 

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
July 17, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
KUMEKUCHA ‘SIMBA DAY’ 
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAKATI Simba imetangaza panga  kwa wachezaji saba ikiwa ni sehemu ya kutaka kusuka kikosi chao kitakachoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara 2026/27, tamasha lao, limepangwa  kufanyika Agosti 8, mwaka huu.

Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa klabu hiyo, Simba ilichapisha ujumbe wenye neno ‘Asanteni’  ukiambatana na picha pamoja na majina ya wachezaji hao, baadhi yao wakiwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo msimu uliopita huku wengine wakicheza kwa mkopo katika klabu tofauti.

Wachezaji waliotangazwa kuondoka ni Chamou Karaboue, Naby Camara, Edwin Balua, Joshua Mutale, Awesu Awesu, Omari Omari na kipa Moussa Camara.

Hatua hiyo ni sehemu ya maboresho ya kikosi yanayofanywa na Simba kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na mashindano ya kimataifa.

Baadhi ya nyota hao walikuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha Simba katika msimu uliomalizika na walitoa mchango wao mkubwa katika mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.

Aidha,  taarifa hiyo, imeeleza kwamba uongozi wa klabu hiyo, utaendelea kufanya mabadiliko zaidi ya kikosi chao, ili kuimarisha timu kwa ajili ya msimu ujao.

Wakati huo huo, baada ya vikao vya muda mrefu hatimaye viongozi wa Simba umepitisha Agosti 8, mwaka huu, kuwa ‘Simba Day’ itafanyika jijini Dar es Salaam huku uzinduzi ukifanyika Ngorongoro, Arusha, Julai 25, mwaka huu.

Taarifa za ndani ya klabu hiyo, zimeeleza kuwa hivi sasa uongozi huo upo katika utaratibu wa kufanya tathmini  ya  uwanja utakaofanyika tamasha hilo na ratiba kamili itatoka.

Tamasha hilo limekuwa likifanyika kila mwaka na hutumika kwa ajili ya kutambulisha kikosi kipya ambacho kitatumika katika msimu wa mashindano wa 2026/2027.

Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally alisema tamasha hilo lipo na watatangaza lini litafanyika na uwanja gani baada ya uzinduzi utakaofanyika Ngorongoro.

“Msimu huu tutakuwa na tamasha bora tofauti na yale yaliopita, muda mfupi kuanzia leo tutatangaza lini tutafanya tamasha hilo muhimu kwetu na mahali ambapo litafanyia,” amesema Ahmed.

Ahmed alisema msimu huu tamasha hilo litakuwa na vitu vingi tofauti, ‘suprises’ za kutosha na wasanii wengi kwani wanahitaji kuwa na tamasha la tofauti na la kihistoria.

“Simba Day ya mwaka huu linafikisha miaka 17 tangu kuanzishwa kwake tangu mwaka 2009,”alisema kiongozi huyo.

Previous Post

WAZIRI MKUU : TUUNGANE KUOKOA MAISHA YA WATANZANIA

Next Post

NSSF YAWAPA NAFUU WAAJIRI, YAWATAKA KUCHANGAMKIA MSAMAHA WA TOZO

Next Post
NSSF YAWAPA NAFUU WAAJIRI, YAWATAKA KUCHANGAMKIA MSAMAHA WA TOZO

NSSF YAWAPA NAFUU WAAJIRI, YAWATAKA KUCHANGAMKIA MSAMAHA WA TOZO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SITAWAANGUSHA

SITAWAANGUSHA

3 months ago
RAIS DK. SAMIA AHIMIZA AMANI, MSHIKAMANO

RAIS DK. SAMIA AHIMIZA AMANI, MSHIKAMANO

6 months ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?