• ePaper
Wednesday, April 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MAAGIZO YA RAIS SAMIA, KARIAKOO YATEKELEZWA 95%

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 24, 2026
in Habari, Kitaifa
0
MAAGIZO YA RAIS SAMIA, KARIAKOO YATEKELEZWA 95%
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

NA EMMANUEL MOHAMED

SHIRIKA la Masoko la Kariakoo, limesema tayari limetekeleza asilimia 95 ya maagizo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, aliyoyatoa wakati akilifungua soko hilo la kimataifa.

Februari 8, mwaka huu, Rais Samia alitoa maagizo kwa uongozi wa soko ya kujenga jengo la kunyonyeshea watoto na kuhakikisha kunakuwa na usalama wa bidhaa za wafanyabiashara.

Akizungumza na gazeti hili jana, Meneja Mkuu wa Shirika hilo, CPA Ashiraf Abdulkarim, alisema tayari wamewasilisha ombi la bajeti ya kujenga jengo la kunyonyeshea watoto Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Abdulkarim alisema baada ya kuwasilisha bajeti hiyo, tayari wataalamu kutoka ofisi hiyo, wakiwemo wahandisi wa majengo na afya, walifika sokoni hapo kutekeleza agizo hilo la Rais Samia.

“Wiki iliyopita, watalaamu hao, walikuja na tukawaonyesha eneo ambalo tumelitenga kujenga jengo hilo na zuri, wamekuja na watu wa afya ambao wao wataona vitu gani vinafaa kuwekwa, huduma za kuonyeshea watoto zitolewe ipasavyo,”alisema 

Alisema baada ya hatua hiyo, kinachosubiriwa ni kukabidhiwa mchoro wa ramani wa jengo hilo na baada ya wiki mbili, itakuwa tayari.

Meneja Mkuu huyo, alisema tayari amewapa mafunzo ya kudhibiti majanga ya moto wafanyabiashara zaidi ya 400 wa soko hilo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Rais Dk. Samia.

“Kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji leo (jana), tumetoa mafunzo haya kwa wafanyabiashara wa soko letu hili ili kuhakikisha hakuna janga lolote la moto linatokea,”alisema. 

Alisema shirika hilo, limeamua kuwapa mafunzo hayo kwa vitendo wafanyabiashara hao, kwa sababu itakuwa sehemu ya kudhibiti majanga ya moto, ambayo yanaweza kutokea katika soko.

KAIMU KAMANDA ZIMAMOTO

Naye, Kaimu Kamanda Mkoa wa Ilala wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Chrispin Rabiuzima, alisema mafunzo hayo ni mwendelezo wa utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia, aliyoyatoa wakati wa ufunguzi wa soko hilo jipya.

“Tutakuwa tunawapatia mafunzo mara kwa mara wafanyabiashara hawa ili kujua namna ya kutumia vifaa vya kudhibiti majanga ya moto,” alisema. 

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa soko hilo, Ramadhani Kakandilo, alisema ni jambo la kupongezwa kwa uongozi wa soko hilo la kuhakikisha wafanyabiashara wanapata mafunzo ya namna ya kukabiliana na majanga ya moto.

“Mafunzo haya yatawasaidia baadhi ya wafanyabiashara kujua namna ya kutumia vifaa hivi vya kuzimia moto ambavyo vimewekwa katika soko hili, maana wengi wamekuwa wakiona katika vyombo vya habari, lakini sasa wamejifunza kwa vitendo,” alisema.   

Previous Post

TANZANIA YATIKISA KIMATAIFA

Next Post

DK. MWIGULU ATOA MAAGIZO AFCON 2027

Next Post
DK. MWIGULU ATOA MAAGIZO AFCON 2027

DK. MWIGULU ATOA MAAGIZO AFCON 2027

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

‘BODA BODA KWANGU NI ZAIDI YA KAZI INAYONIWEKA MJINI’

‘BODA BODA KWANGU NI ZAIDI YA KAZI INAYONIWEKA MJINI’

3 months ago
MOROCCO ATOA TANO KOMBE LA MAPINDUZI

MOROCCO ATOA TANO KOMBE LA MAPINDUZI

4 months ago

Popular News

  • UCHAGUZI WA WAJUMBE EALA WAANZA RASMI

    UCHAGUZI WA WAJUMBE EALA WAANZA RASMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUME ILIYOUNDWA NA RAIS DK. SAMIA ILIVYOBEBA MATUMAINI YA AMANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DCEA YAKAMATA SHEHENA YA MIRUNGI KUTOKA KENYA, YAKAMATA BOTI BAGAMOYO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ASKOFU MNDOLWA: TUME YA JAJI CHANDE ITAIPELEKA NCHI PAZURI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WASHIRIKI MISS WORLD TANZANIA WAPEWA SOMO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?