• ePaper
Wednesday, July 29, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MVUTANO MAZISHI YA WAMBURA WAFIKA KORTINI, DALILI ZA MARIDHIANO ZACHOMOZA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
July 29, 2026
in Habari, Kitaifa
0
MVUTANO MAZISHI YA WAMBURA WAFIKA KORTINI, DALILI ZA MARIDHIANO ZACHOMOZA
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na Baltazar Mashaka, Mwanza

MGOGORO wa mazishi ya marehemu Wambura Mambya (54), aliyefariki Julai 21, 2026 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure, umefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana, huku pande zinazohusika zikionyesha dalili za kufikia maridhiano yatakayowezesha mazishi kufanyika kwa amani.

Shauri hilo la madai namba 19355 la mwaka 2026 lilisikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana, Chrescencia Mushi, likimhusisha mwombaji Elizabeth Nyakao dhidi ya mjibu maombi John Mambya.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Julai 30, 2026 baada ya upande wa ndugu wa marehemu kutokuwapo mahakamani wakati shauri lilipoitwa, huku wakieleza baadaye kuwa walikumbwa na changamoto ya kutofahamu utaratibu wa mahakama.

Baada ya kuahirishwa kwa shauri hilo, mawakili wa pande zote walihitimisha majadiliano yaliyozaa makubaliano ya awali, ambapo ndugu wa marehemu walieleza utayari wao wa kushirikiana ili mgogoro huo umalizike kwa maelewano.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo ya awali, mwili wa marehemu unatarajiwa kuzikwa upande wa familia kwa kuzingatia mila na desturi, huku makubaliano hayo yakitarajiwa kuwasilishwa rasmi mahakamani kwa hatua za kisheria.

 Akizungumza baada ya mazungumzo hayo, Elizabeth Nyakao alisema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa; “nimesamehe na nimeridhika na makubaliano tuliyoyafanya.”

Wakili Demetrius Mtete alisema migogoro ya aina hiyo mara nyingi hupata suluhu kupitia maridhiano ili kulinda maslahi ya pande zote na kudumisha amani katika familia.

Awali, mgogoro huo ulizuka Julai 24, 2026 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure baada ya ndugu wa marehemu na familia yake kutofautiana kuhusu mahali na utaratibu wa mazishi.

Upande wa mke mkubwa ulieleza kuwa ulitaka kushiriki kikamilifu katika mazishi ya marehemu, huku ndugu wa marehemu wakieleza kuwa walikuwa wakitekeleza maelekezo ambayo walidai marehemu aliwahi kuyatoa kuhusu mahali alipotaka kuzikwa.

 Kutokana na hali hiyo, wananchi walikusanyika hospitalini na kusababisha sintofahamu iliyohitaji mamlaka za usalama kuingilia kati ili kurejesha utulivu.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, msemaji wa familia Gradson Mambya alisema lengo lao ni kuhakikisha mazishi yanafanyika kwa utaratibu utakaoondoa migogoro na kuimarisha mshikamano wa familia.

 Kwa upande wake, Kamanda  Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna (DCP) Wilbrod Mutafunga  alisema lilichukua hatua za kudhibiti hali ya usalama katika eneo la hospitali baada ya kujitokeza kwa msongamano wa watu na mvutano kati ya pande zinazohusika.

Aidha, kamanda huyo wa polisi wamewakumbusha wananchi kuwa suala la nani mwenye haki ya kufanya mazishi ya marehemu ni miongoni mwa masuala yanayopaswa kuamuliwa na mahakama kwa mujibu wa sheria pale.

Aliwaatakaa wananchi kuepuka kutoa hukumu au kuchukua hatua zinazoweza kuvuruga mwenendo wa shauri, huku akisisitiza kuwa jukumu lao ni kulinda usalama wa watu na mali pamoja na kuhakikisha amani inadumishwa wakati taratibu za kisheria zikiendelea.

Hadi saa 10 jioni, Julai 28, 2026, juhudi za kuwapatanisha pande hizo zilikuwa zinaendelea huku mamlaka zikisisitiza umuhimu wa maelewano kuhakikisha mwili wa marehemu unazikwa kwa amani na heshima.

Mahakama inatarajiwa kuendelea kusikiliza shauri hilo Julai 30, 2026 kwa ajili ya kupokea na kuidhinisha makubaliano  yaliyofikiwa na pande mbili zinazohusika, endapo yatakidhi matakwa ya sheria.

Previous Post

RAIS DK. SAMIA ATAJA SIFA ZA MAWASILIANO SERIKALINI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

UVCCM YAWAPA POLE WALIOPATA MADHILA

UVCCM YAWAPA POLE WALIOPATA MADHILA

9 months ago
WADAIWA VIWANJA 6,560 DODOMA WAPEWA SIKU 21

WADAIWA VIWANJA 6,560 DODOMA WAPEWA SIKU 21

7 months ago

Popular News

  • MVUTANO MAZISHI YA WAMBURA WAFIKA KORTINI, DALILI ZA MARIDHIANO ZACHOMOZA

    MVUTANO MAZISHI YA WAMBURA WAFIKA KORTINI, DALILI ZA MARIDHIANO ZACHOMOZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA ATAJA SIFA ZA MAWASILIANO SERIKALINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • 50 BORA ‘FORM SIX’ KUSOMA AI NJE YA NCHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DHAHABU YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI 1.2/- YAKAMATWA IKITOROSHWA DAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA ATAKA UADILIFU, USHIRIKIANO NA MATOKEO KWA VIONGOZI WAPYA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?