Na MWANDISHI WETU
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imemkuta Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ana kesi ya kujibu katika shauri la uhaini linalomkabili.
Akisoma uamuzi huo Leo Agosti 21, 2026, Jaji Ndunguru, anayeongoza jopo la majaji linalosikiliza shauri hilo, amesema mahakama imejiridhisha kuwa upande wa mashtaka, unaowakilishwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), umewasilisha ushahidi wa kutosha unaoonyesha kuwa Lissu ana kesi ya kujibu.
Uamuzi huo unafungua hatua ya utetezi, ambapo Lissu atapata fursa ya kuwasilisha ushahidi na kuita mashahidi wake mbele ya mahakama ili kujibu hoja na ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka.
Hatua hiyo itaiwezesha mahakama kusikiliza upande wa utetezi kabla ya kufikia hatua inayofuata katika shauri hilo.




