• ePaper
Friday, August 28, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

HATIMAYE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
August 22, 2026
in Habari, Kitaifa
0
HATIMAYE
0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na Waandishi Wetu

HATIMAYE ile siku iliyosubiriwa kwa hamu na Watanzania, ni leo, ambayo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amezindua Bwawa la kihistoria la kuzalisha umeme la Julius Nyerere (JNHHP).

JNHPP ni maono ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, aliyoyajenga na waasisi wenzake kuanzia mwaka 1976, hatimaye leo yametimia chini ya uongozi imara wa Rais Dk. Samia.

Kufuatia tukio hilo kubwa la kihistoria, baadhi ya wanasiasa wakongwe na wachumi; wametoa maoni tofauti kuhusu kukamilika JNHPP, huku wakiwataka Watanzania kutumia fursa ya umeme huo kujiimarisha kiuchumi.

ANNA ABDALLAH

Akizungumza na UHURU, mwanasiasa mkongwe aliyewahi kuwa waziri katika awamu  tofauti nchini, Anna Abdallah, alisema, Rais Dk. Samia ameithibitishia dunia uhodari na uchapakazi wake kupitia utekelezaji wa mradi huo, ambao ameundeleza baada ya mtangulizi wake, Hayati Dk. John Magufuli.

“Namshukuru na kumpongeza Rais Dk. Samia kwa uamuzi aliyoufanya wa kuendeleza mradi huu, sasa tunatembea kifua mbele, sio hapa nchini hata Afrika Mashariki na dunia kwa ujumla.

“Ndoto za Mwalimu Nyerere tumeziona zikitekelezwa kupitia Rais Dk. Samia, tumshukuru Mungu kwa kutupa Rais huyu,”alisema.

Alisema mradi huo uliwahi kupangwa kutekelezwa tangu enzi za mkoloni, lakini ulishindikana na ukawa na upinzani.

Kwa mujibu wa Anna, baadhi ya vikwazo vilidai mradi huo utaharibu mazingira, jambo ambalo sio sahihi, kwa sababu sasa maji yameongezeka na uhifadhi umekuwa mzuri.

“Leo historia inaandikwa, hii inatoa ujumbe kwa Waafrika wenzetu kwamba, kuamua kwa usahihi ni jambo muhimu sana, na si kila tunachoshauriwa ni kweli, walituambia mazingira yataharibika si kweli,” alisema.

KATE KAMBA

Mwanasiasa mwingine mkongwe, aliyewahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Kate Kamba, alisema sasa ni wakati wa wananchi kutumia umeme kufanyia kazi fursa mbalimbali zinazotumia nishati hiyo.

“Tusiuangalie umeme, tuangalie fursa zinazotokana na umeme, tujitahidi kufanya mambo ya viwanda, na kuhamasisha kila nyumba iwe na umeme,”alisema. 

Pia, alisema Rais Dk. Samia amefanya kazi kubwa ya kukamilisha mradi huo, ikiwemo kutoa fedha na kuhakikisha unakamilishwa.

MZEE JOSEPH BUTIKU

Mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti  wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF),  Joseph Butiku,  alisema kufanikisha kwa mradi huo kumedhihirisha utendaji kazi bora wa Rais Dk. Samia.

Kwa mujibu wa Butiku, hajaona Rais Dk. Samia akishindwa kazi, katika kukamilisha miradi ya maendeleo iliyoko mbele yake.

Alisema Rais Dk. Samia ametekeleza ahadi yake ya kuimalizia miradi mikubwa ya maendeleo iliyoachwa na mtangulizi wake, Hayati Dk. Magufuli.

 “Rais wetu anafanya kazi vizuri, nampenda kwa kazi zake na ninatetea kazi nzuri anazofanya, alisema atatekeleza shughuli zote zilizoachwa na  Rais Hayati Dk. Magufuli na sasa anatekeleza.

“Na ikumbukwe alifanya kazi na Dk. Magufuli na yeye anaendelea kukamilisha kazi, sisi tushukuru tumepata bwawa na faida zake zinafahamika, sina haja ya kuanza kuzieleza,”alisema.

COASTER KIBONDE

Kwa upande wake,     Mwenyekiti  wa chama cha siasa cha upinzani cha Makini,  Coaster  Kibonde,  alipongeza uthubutu wa serikali kwa kujenga bwawa hilo kwa kutumia fedha za ndani.

Mwenyekiti huyo alisema, haikuwa kazi rahisi kwa kuwa baadhi ya mataifa na wakosoaji wa ndani na nje ya nchi walipinga kuwepo kwa mradi huo.

Kibonde alishauri serikali kulinda miundombinu ya bwawa hilo, kuepusha na vitendo vya hujuma kwa kuwa kuna vibaraka wanaoweza kutumwa kufanya hujuma mradi huo.

WAMACHINGA

Mwenyekiti wa Chama cha Machinga Mkoa wa Dar es Salaam, Yusuph Namoto, alisema bwawa hilo litaleta ahueni kwa wajasiriamali, ambao bidhaa zao nyingi wanazouza zinazalishwa viwandani kwa kutumia umeme.

 “Tunasema ni faida kwetu hasa wajasiriamali, kwa kuwa bidhaa zetu zinazalishwa viwandani na tutazipata kwa bei nafuu, hii inatokana na viwanda vilivyopo vitatumia umeme kwa gharama nafuu, tofauti na hivi sasa vinatumia gharama kubwa kuzalisha kutokana umeme mdogo,”alisema.

Mwenyekiti huyo, alisema wajasiriamali wadogo wakiwemo wachomeleaji vyuma, saluni za kike, kiume na wauza maji watakuwa na uhakika na ajira zao kwa kuwa umeme utakuwa ukipatikana kwa uhakika.

WACHUMI

Mtaalamu wa Uchumi, Profesa Samwel Wangwe, alisema upatikanaji wa umeme wa uhakika una nafasi kubwa katika kukuza shughuli za kiuchumi, kwa kuwa sekta mbalimbali ikiwemo viwanda, biashara, kilimo na huduma nyingine zinahitaji nishati hiyo kwa lengo la kufanya kazi kwa uhakika.

Profesa Wangwe alisema mradi unaozinduliwa leo, unatakiwa kusambazwa sehemu kubwa nchini kwa lengo la kuleta matokeo mazuri kwa wananachi.

Akizungumzia suala la uwekezaji nchini katika sekta ya umeme, Profesa  Wangwe alisema ongezeko la uzalishaji wa umeme linaweza kuimarisha mazingira ya uwekezaji nchini.

“Kila mwekezaji anahitaji umeme wenye uhakika kwa ajili ya kuzalishia bidhaa zake, hivyo mradi huo wa umeme ni moja ya chanzo cha mapato nchini,”alisema.

Aidha, Profesa Wangwe alisema kuwepo kwa mradi huo wa umeme kutaongeza fursa za ajira na kipato kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Pia, Profesa Wangwe alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha umeme unatumika kuongeza thamani ya bidhaa, kukuza viwanda na kuimarisha huduma kwa jamii.

Wangwe alisema mabadiliko ya tabianchi yasirudishe nyuma jitihada za kuzalisha bidhaa kwa kutumia nishati ya umeme.

Aliiomba serikali itumie ubunifu mwingine wa kulinda chanzo cha umeme, ikiwemo kutumia umeme wa upepo na gesi ili shughuli za uzalishaji mali ziweze kuendelea.

PROFESA KINYONDO

Kwa upande wake Mhadhiri wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Profesa  wa Uchumi, Abel Kinyondo, alisema nishati ya umeme ni nguzo muhimu ya uchumi wa taifa.

Profesa Kinyondi alisema nchi yoyote iliyoendelea ni lazima iwe na umeme wa uhakika, ambao utasaidia uzalishaji.

“Hakuna chanzo kingine cha maendeleo dhidi ya nishati ya umeme, ambayo inampa mtu fursa nyingi za uzalishaji mali.

“Nakumbuka binadamu wa kwanza alianza kupata maendeleo baada ya kugundua moto wa kufikicha kijiti na moto ukatokea; baada ya hapo hakuweza tena kula nyama mbichi ila alikuwa anaichoma halafu anakula, hapo ndipo utaona faida ya nishati hiyo,”alisema.

Aidha, Profesa Kinyondo alisema, kuwepo kwa umeme wa uhakika pia ni fursa ya vijana wengi kupata ajira katika viwanda vidogo na vikubwa.

DK.MMARI

Kwa upande mchambuzi wa masuala ya uchumi, Dk. Donald Mmari, alisema mradi huo utaleta mafanikio makubwa mijini na vijijini,

 “Wananchi wategemee umeme wa uhakika, kwa sababu uzalishaji mali unategemea nishati hiyo kwa lengo la kufanya kazi kwa urahisi,”aliongeza.

Pia, Dk. Mmari alimshukuru Rais Dk. Samia kwa kufanikisha ujenzi wa mradi huo.

 “Tufike mahali tuseme ukweli, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anaweza majukumu mengi aliyoachiwa naona anayatekeleza kwa vitendo,”alisema. 

Imeandaliwa na Irene Mwasomola, Rehema Maigala na Saimon Nyalobi

Previous Post

SAFARI KUTOKA STIEGLER’S GORGE HADI BWAWA LA JULIUS NYERERE

Next Post

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA KUKABILI UKAME

Next Post
TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA KUKABILI UKAME

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA KUKABILI UKAME

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

KIBANO KIKALI WALIOZIMA ‘X-RAY’ TEMEKE

KIBANO KIKALI WALIOZIMA ‘X-RAY’ TEMEKE

8 months ago
YANGA, SIMBA VITA KALI

YANGA, SIMBA VITA KALI

3 months ago

Popular News

  • TUME MIPANGO, NIRC WAJADILI UBORA MIRADI YA UMWAGILIAJI

    TUME MIPANGO, NIRC WAJADILI UBORA MIRADI YA UMWAGILIAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MASAUNI AANIKA UMAHIRI WA TANZANIA INAVYOLINDA UDONGO, MATUMIZI MBOLEA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NDEJEMBI KUMRITHI BALOZI DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUME YA MADINI YATOA SIKU 30 KWA WALIOKIUKA MIKATABA YA MSAADA WA KIUFUNDI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA ARIDHIA DK. NCHIMBI KUJIUZURU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?