• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

YANGA, SIMBA VITA KALI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
June 10, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
YANGA, SIMBA VITA KALI
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

WAKATI kikosi cha timu ya Yanga kikijiandaa kuelekea mkoani Kigoma, kocha wa Simba Steve Barker amesema timu yake inahitaji kuwa makini  katika mechi zao na kuacha kuwafikiria  Yanga.

Timu hizo zipo katika vita kali ya kila mmoja kutaka kuibuka na ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Katika msimamo wa Ligi Yanga inaongoza ligi hiyo ikiwa pointi 60 huku timu ya Simba ikishika nafasi ya pili, ikiwa na alama 58 na kusababisha ushindani kuongezeka.

Yanga imebaki na michezo mitano dhidi ya timu za Mashujaa FC, Fountain Gate FC, Azam FC, TRA United na JKT Tanzania.

Simba wao wamebaki na mchezo dhidi ya Pamba Jiji, Mbeya City, Mtibwa Sugar, Singida Black Stars na KMC.

Kuelekea mchezo wa Juni 13, mwaka huu, Yanga itacheza na Mashujaa FC katika Uwanja wa Lake Tanganyika huku mkoani Kigoma.

Timu hizo, zitashuka dimbani huku Mashujaa FC ikiwa na kumbukumbu ya kupokea kichapo cha mabao 6-0 katika  mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Simba yenyewe inatarajiwa kushuka dimbani Juni 14, mwaka huu kupambana na Pamba Jiji katika mchezo utakaochezwa Uwanja KMC huku timu hizo zikiwa na kumbukumbu ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza.

Kuelekea pambano hilo la Juni 13, mwaka huu, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe alisema timu yao imejipanga vizuri kuhakikisha wanapata ushindi huo kwa vile vita ni kubwa ya kusaka ubingwa huo.

“Tunajua utakuwa mchezo mgumu kwani mechi hizi za mwisho wa msimu mara nyingi zinakuwa ngumu na zenye changamoto kubwa,” alisema.

 Kamwe alisema wachezaji wote ambao waliokuwa katika kikosi cha timu ya Taifa wamerejea na wanaendelea na programu ya mazoezi.

Kwa upande wa kocha wa Mashujaa FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, alisema hana hofu na Yanga kwani timu yao imefanya maandalizi ya kutosha kupata ushindi.

“Tunajua hautakuwa mchezo rahisi lakini hatutakubali kuona tunapoteza katika uwanja wetu wa nyumbani,” alisema Julio.

Kwa upande wa Simba, kocha Steve Barker akizungumzia kuhusu maandalizi ya kikosi chake kabla ya kuivaa Pamba Jiji alisema wachezaji wake wapo fiti.

 “Tunaingia katika mechi zetu zilizobaki tukiwa makini zaidi kwani hatupaswi kuwafikiria Yanga, tunapaswa kuwa makini sisi wenyewe, tufanye vizuri,” alisema Barker.

Hata hivyo, kocha huyo alisema bado muda wa kuzungumzia suala la ubingwa kwa sasa kwani mechi zote zilizobakia ni ngumu na zenye changamoto kubwa.

Meneja habari na mawasiliano wa timu hiyo, Ahmed Ally alisema wamebaki na mechi tano muhimu na lengo lao kubwa ni kuhakikisha wanavuna pointi zote 15.

 “Niseme tu ukweli tuna mechi ngumu zilizobakia hakuna iliyokuwa nyepesi lakini kwa ubora tuliokuwa nao kwa sasa inawezekana kuvuna alama 15,” alisema Ahmed.

Previous Post

TANZANIA, SINGAPORE KUSHIRIKIANA KIMKAKATI

Next Post

SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI – DK. MWIGULU

Next Post
SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI – DK. MWIGULU

SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI – DK. MWIGULU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

ULEGA ASHUSHA MAAGIZO KWA WAKANDARASI NCHINI

ULEGA ASHUSHA MAAGIZO KWA WAKANDARASI NCHINI

5 months ago
DK. NCHIMBI : TUTAJENGA BARABARA WILAYANI LUDEWA

DK. NCHIMBI : TUTAJENGA BARABARA WILAYANI LUDEWA

10 months ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?