• ePaper
Sunday, September 20, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Makala

MSISITIZO WA VIONGOZI TAHADHARI YA EL-NINO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 17, 2026
in Makala
0
MSISITIZO WA VIONGOZI TAHADHARI YA EL-NINO
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

SUPERIUS ERNEST Na HOPE MWAMASANGULA (UDOM)

AGOSTI 18, mwaka huu, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa utabiri wa msimu wa mvua ya vuli, unaotarajiwa kuanzia mwishoni mwa Septemba na kuendelea hadi Desemba.

Katika utabiri huo, TMA ilitoa tahadhari ya kuwepo kwa mvua kubwa ya kiwango cha El-Nino, katika baadhi ya mikoa na kuwataka wananchi na mamlaka husika kuchukua tahadhari za haraka kuepuka athari zinazoweza kusababishwa na mvua hiyo.

TMA, ilitaja baadhi ya athari zinazoweza kujitokeza ni makazi kuzingirwa na maji, hasa maeneo ya mabondeni na yale ya tambarare yenye uwezekano wa kujaa maji mengi.

Kuathirika kwa shughuli za kilimo, ufugaji, kuharibika kwa miundombinu ya barabara na usafirishaji.  

Mamlaka iliwaasa wananchi na sekta mbalimbali kama ya kilimo, ufugaji, uvuvi na usafirishaji kuchukua tahadhari ambazo zitaepusha madhara makubwa yatakayotokana na mvua hiyo.

Kwa utabiri na msisitizo wa TMA wa kuchukua tahadhari ya mvua hizo, serikali kupitia mamlaka zake mbalimbali imeendelea kufanya maandalizi ya kukabiliana na hali hiyo.

AGIZO LA RAIS DK. SAMIA

Akizindua Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Megawati 2,115 wa Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere, JNHPP, Agosti 22, mwaka huu, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, aliwaagiza Wakuu wa Mikoa, Wilaya na wa taasisi za serikali kuanza maandalizi, kabla ya mvua kubwa iliyotabiriwa na TMA.

Lengo la agizo hilo la Rais Dk. Samia ni kuchukua tahadhari mapema kuzuia maafa na madhara kwa wananchi.

Rais Dk. Samia alisisitiza viongozi hao, kuchukua hatua na kutopuuza tahadhari hiyo ya TMA, kuhusu uwezekano wa mvua kubwa inayohusishwa na hali ya El-Nino.

Rais Dk. Samia alisisitiza kuwa, tahadhari za TMA zisibaki katika taarifa pekee, zifuatwe na hatua za vitendo zichukuliwe, ikiwemo maandalizi ya mazingira na mifumo ya kukabiliana na athari za mvua.

Lengo la kauli hiyo ya Rais Dk. Samia kwa viongozi hao ni kujitayarisha katika maeneo yao, kuweka mazingira sawa mvua itakaponyesha isisababishe maafa makubwa kwa wananchi.

MAKAMU WA RAIS

Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi, alitoa tahadhari kwa wanachi na viongozi kujiandaa, akiwahimiza kuhakikisha majiji yote yanajipanga vyema kukabiliana na mvua hiyo.

Ndejembi alizitaka wizara zote na taasisi na mamlaka husika  ikiwemo Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA), Wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD) na zingine zinazoguswa na hali hiyo, kuhakikisha maeneo yote yenye mitaro yanasafishwa na uchafu unaondolewa kabla ya mvua kuanza.

Aliongeza kuwa, vyombo vya ulinzi ikiwemo jeshi, vishirikishwe kuhakikisha wanaongeza nguvu na kufanya kazi kwa pamoja, kutekeleza majukumu hayo.

Ndejembi alisema zinaweza kutokea athari zisizozuilika, hivyo serikali inajipanga kupunguza athari ambazo zinaweza kujitokeza.

Alisema: “Ni ukweli usiopingika kwamba, miji mikubwa ndiyo yenye idadi kubwa ya watu, ambayo inatekeleza shughuli mbalimbali ikiwemo biashara, hivyo athari za mafuriko zinaweza kuwa kubwa na kuathiri wananchi wengi katika majiji makubwa.

 “Niwatake waheshimiwa mawaziri, mfanye kampeni ya haraka katika maeno hayo kuhakikisha mikondo ya maji, mitaro inafanyiwa usafi kwa haraka,”alisema.

Aliongeza kuwa, maeneo ambayo wakandarasi wapo ‘saiti’ wamechonga barabara, kujaza vifusi na kuviacha bila kusambaza, mvua zinapokuja barabara hizo, zinageuka kuwa kero kwa wananchi hasa ambao wanatumia magari madogo, vifusi vinajaa utelezi na maeneo hayapitiki, hivyo wahakikishe vinasambazwa kabla ya mvua kuanza.

Katika maeneo ambayo madaraja na makaravati yanajengwa, yasitelekezwe kwa sababu mvua inayokuja ni kubwa, hivyo wataalamu wasimamie kazi hizo zifanywe kwa ukamilifu.

WAZIRI MKUU

Pia, Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, katika hotuba yake ya kuhitimisha Mkutano wa Nne wa Bunge, alisema maeneo yote hatarishi yatambuliwe mapema, tathimini za vihatarishi zifanyike hatua zichukuliwe haraka.

Alisema ni muhimu kuhahikikisha vifaa vya uokoaji, huduma za dharura na mifumo ya mawasiliano inakuwa katika hali ya utayari.

Dk. Mwigulu alisisitiza kuwa, idara na taasisi zinazohusika na miundombinu na usafi wa mazingira zihakikishe barabara zinapitika wakati wote, mitaro na makaravati isafishwe.

Akizungunza na viongozi wa dini, aliwaasa waendelee kufanya maombi kuhusiana na mvua zinazotarajiwa kunyesha, kumuomba Mungu kuepusha mvua zinazoweza kusababisha athari kubwa.

Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu amekuwa akitoa msisitizo huo wa tahadhari ya El-Nino, kwa wakuu wa mikoa kupitia ziara zake anazozifanya katika mikoa mbalimbali.

Aliwahimiza kuhakikisha wanachukua tahadhari mapema kwa kufanya maandalizi ya kuepusha athari zaidi kuhusu mvua hiyo.

WAZIRI WA OMW-TAMISEMI

Kwa upande wake, Waziri wa OMW, TAMISEMI, Profesa Riziki Shemdoe, alielekeza viongozi wa wilaya na halmashauri kote nchini kuhakikisha wanafanya kazi ya kuzibua mitaro, mifereji ya maji, kujilinda na kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua hiyo.     

Aliwataka wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri na mameneja wa TARURA nchini, kuhakikisha wanashirikiana na taasisi nyingine katika kujiandaa, kuwa na utayari kukabiliana na athari za mvua za El-Nino kwa kuhakikisha miundombinu ya kupitisha maji inakuwa katika hali nzuri inakidhi mahitaji.

“Nimuelekeze meneja wa TARURA wilaya ya Kilwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa; kushirikiana na wananchi kuzibua mifereji ya maji iliyoziba kipindi cha mvua ya El-Nino, maji yasipate nafasi ya kuchepuka na kuvamia makazi ya wananchi na kuleta madhara, Mkuu wa Wilaya ya Kilwa simamia jambo hili,” alisema.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Profesa Palamagamba  Kabudi, alitolea ufafanuzi fedha zilizopangwa kukabiliana na suala hilo la kuzuia na kupunguza athari za mvua hiyo ya El-Nino.

Profesa Kabudi alisema serikali kupitia kamati za usimamizi wa maafa na sekta mbalimbali kushirikiana na kuchukua hatua kuhakikisha mvua hizo, zinatumika katika shughuli za uzalishaji ikiwemo kilimo, ufugaji, uvunaji wa maji na uvuvi.

Alihimiza wananchi kuelimishwa na kuhimizwa kuchukua hatua muhimu za kupunguza athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo ikiwemo kuweka akiba ya chakula na kulima mazao sahihi na mbegu bora.

Profesa Kabudi aliendelea kuwa, kutekeleza mipango ya kujiandaa na kukabiliana na athari ya El-Nino, kwa kuzingatia mpango wa taifa wa kudhibiti matokeo ya mvua hiyo na kuandaa rasilimali zitakazotumika.

Vilevile, alisema wanashirikisha wadau wote wa maafa wakiwemo wananchi, taasisi na sekta binafsi katika maeneo yao.

“Maeneo yote hatarishi yatambuliwe mapema, kufanyiwa tathmini na kuchukua hatua stahiki ikiwemo kuhamasisha wananchi waondoke katika maeneo hayo,”alisema.

Vilevile, kuzuia uwezekano wa milipuko ya magonjwa ya binadamu, wanyama na mimea.

Kabudi alizitaka wizara, mikoa, taasisi na wadau wengine wanaohusika na miundombinu wafanye ukaguzi na kuhakikisha inaimarishwa na kusafishwa yakiwemo madaraja, makaravati na mitaro hatua itakayosaidia upatikanaji wa huduma muhimu kabla, baada na wakati wa mvua ikiwemo usafirishaji, maji na umeme.

“Kuimarisha usimamizi wa mazingira ukiwemo udhibiti wa taka ngumu na utengenezaji wa njia za maji, kingo za mito, kuhakikisha kuwa vifaa vya uokoaji.

“Kuhakikisha mifumo ya mawasiliano inapatikana katika hali ya utayari wakati wote na kutenga maeneo salama yatakayotumika kwa ajili ya makazi ya dharura pindi maafa yatakapotokea,”alisema.

Alihimiza wizara kufuatilia taarifa zitakazoendelea kutolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa, kuchukua hatua stahiki za kujiandaa kila siku ikiwemo kutoa taarifa za maafa haraka ili zitolewe ufafanuzi.

WAKUU WA MIKOA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, alitoa wito kwa watumishi wote, watendaji wa vijiji, mitaa, kata na watu wa maendeleo ya jamii kuhakikisha wanaangalia maeneo yao kama kila mtu anajenga nyumba imara kupunguza athari zinazoweza kutokana na mvua hizo.

Aidha, alipokutana na viongozi wa dini mkoani hapo, Rosemary aliwashukuru kwa kuliombea taifa, viongozi na wananchi na kuwahimiza kuendelea kuomba athari zitakazoweza kusababishwa na mvua ya El-Nino zipungue, licha ya maandalizi mengine kama kurekebisha miundombinu yanayoendelea kutekelezwa.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Martine Shigela, aliwataka wananchi wa mkoa huo, kuchukua tahadhari dhidi ya mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha nchini.

Aliwataka wananchi wanaoishi maeneo ya mabondeni wahame na kwenda maeneo salama kuepuka madhara.

MSISITIZO WA TMA

Kupitia kauli ya Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Ladislaus Chang’a, alisisitiza wananchi kuendelea kufuatilia taarifa zinazotolewa na mamlaka hiyo, kufahamu mwenendo wa hali ya hewa.

Chang’a Alisema katika kipindi hiki cha kuelekea katika msimu wa mvua za vuli, wanaendelea kufuatilia mifumo yao ya utabiri wa hali ya hewa, kwa lengo la kupata taarifa sahihi za kuwahabarisha wananchi kuhusu mwenendo wa mvua hizo.

Vilevile, wamekuwa wakiwahimiza waandishi wa habari ambao ni wadau wao wakubwa, kuepuka kuandika habari zinazolenga kupotosha umma, bali wazingatie weledi wa kutafuta habari kutoka vyanzo sahihi vya ofisi yao kuhusu hali ya hewa.

Previous Post

KIVUMBI SIMBA, AZAM FC

Next Post

UBUNIFU MITEGO YA PANYA ULIVYOMUINUA KIUCHUMI KILONGOLA

Next Post
UBUNIFU MITEGO YA PANYA ULIVYOMUINUA KIUCHUMI KILONGOLA

UBUNIFU MITEGO YA PANYA ULIVYOMUINUA KIUCHUMI KILONGOLA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MWANZA KINARA USIMAMIZI MAAFA

MWANZA KINARA USIMAMIZI MAAFA

4 months ago
‘MIFUMO YA UUZAJI MAZAO YA WAKULIMA, WAIMARISHWA’

‘MIFUMO YA UUZAJI MAZAO YA WAKULIMA, WAIMARISHWA’

1 year ago

Popular News

  • NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE

    NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JK ATOA USHUHUDA DALILI SARATANI TEZI DUME

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA KIFUA MBELE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KASI MAANDALIZI AFCON 2027 YAIKUNA CAF

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • FUNZO JIPYA KADI NYEKUNDU YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?