Na NASRA KITANA
TIMU za soka za Taifa Stars na Guinea -Bissau zinatarajiwa kupambana leo katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika(AFCON 2027).
Kuelekea mchezo huo, kocha wa timu hiyo, Miguel Gamond amesema timu yake, imefanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha inapata ushindi.
“Tumejipanga vizuri kuhakikisha tunapata ushindi katika mchezo wetu dhidi ya Guinea Bissau, tunajua utakuwa mchezo mgumu na wenye changamoto kubwa,” alisema.
Gamondi alifafanua kuwa ana imani kubwa na wachezaji wake kwani kila mmoja anajua nini anatakiwa kufanya ili kupata ushindi.
Nyota wa timu hiyo, Simon Msuva alisema kama wachezaji wamejipanga vizuri kupata ushindi ambao ni kwanza kabla kucheza na Madagascar.
Baada ya mchezo huo wa leo, Tanzania itacheza mechi nyingine ya kufuzu AFCON 2027 dhidi ya Madagascar Septemba 29, mwaka huu, mchezo utakaochezwa nchini Morocco (Casablanca)kwani Madagascar wanautumia uwanja huo kama wa nyumbani.




