• ePaper
Saturday, May 30, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DK. MWIGULU ASHIRIKI MKUTANO WA NGAZI YA WAKUU WA NCHI JIJINI BRAZZAVILLE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 26, 2026
in Habari, Kitaifa
0
DK. MWIGULU ASHIRIKI MKUTANO WA NGAZI YA WAKUU WA NCHI JIJINI BRAZZAVILLE
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI MKUU Dk. Mwigulu Nchemba, ameshiriki Mkutano wa 61 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ambao umeshirikisha Wakuu wa Nchi na Serikali za Afrika na wawakilishi wao ambapo yeye amemwakilisha Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Mkutano huo ambao umeanza leo (Jumanne, Mei 26, 2026) jijini Brazzaville, Jamhuri ya Kongo ulifunguliwa na Rais wa nchi hiyo, Denis Sassou-Nguesso na kuhudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali na Makamu wa Rais kutoka nchi mbalimbali.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo ulioanza katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kintele (Kintele International Conference Centre), Rais Nguesso amesema Afrika haipaswi kuishia kujivunia kuwa na utajiri wa rasilmali bali izitumie vizuri rasilimali hizo kuwanufaisha wananchi wake.

Amesema ili kuyafikia mageuzi yanayotakiwa, Afrika inahitaji kuwa na miradi ya kimkakati yenye mageuzi. “Tunahitaji kukuza masoko ya fedha na kuziwezesha taasisi za kikanda ili ziweze kukabiliana na vihatarishi vya kiuchumi kupitia ushirikiano imara. Hii itasaidia kuifanya Afrika kuwa na udhibiti wa rasilimali zake na hatimaye kuimarisha uchumi wa nchi pamoja kuboresha maisha wananchi.”

Baada ya ufunguzi, Waziri Mkuu pia alishiriki mdahalo wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu mustakabali wa ufadhili wa maendeleo barani Afrika (Presidential High-Level Panel on Africa’s Development Financing) ambao uliwashirikisha Rais wa Jamhuri ya Congo, Denis Sassou Nguesso, Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faustin Archange Touadéra Rais wa Jamhuri ya Gabon, Brice Clotaire Oligui Nguema na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Sidi Ould Tah.

Vilevile, Waziri Mkuu alishiriki kwenye mdahalo wa uzinduzi wa taarifa ya African Economic Outlook 2026 na mkutano wa wadau wa maendeleo kuhusu ufadhili wa Mpango wa Uwekezaji wa Blue Fund for the Congo Basin.

Previous Post

DK. YONAZI AIELEZA MSUMBIJI UZOEFU WA TANZANIA INAVYOKABILI UKAME

Next Post

FAIDA ZA KURASIMISHA BABA NA MAMA LISHE

Next Post
FAIDA ZA KURASIMISHA BABA NA MAMA LISHE

FAIDA ZA KURASIMISHA BABA NA MAMA LISHE

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TPLB YAGUSIA WAZO LA FIFA USAWA WA KALENDA

TPLB YAGUSIA WAZO LA FIFA USAWA WA KALENDA

6 months ago
SIMULIZI YA KUSIKITISHA ANAYEDAIWA KUUA MKE

SIMULIZI YA KUSIKITISHA ANAYEDAIWA KUUA MKE

3 months ago

Popular News

  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MASTAA YANGA WAUTAJA UBINGWA LIGI KUU BARA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?