• ePaper
Friday, October 9, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

VIGOGO SIMBA MACHO KILA KONA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 7, 2026
in Burudani, Habari, Michezo
0
VIGOGO SIMBA MACHO KILA KONA
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

HOMA ya pambano la Simba na Yanga imezidi kupanda huku viongozi wa Wekundu wa Msimbazi wakiwa macho kila kona kuelekea mchezo huo.

Timu hizo, zinatarajiwa kupambana Jumamosi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaopigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 usiku.

Katika pambano hilo, Simba itakuwa mwenyeji wa mchezo huo wa dabi ya Kariakoo mechi ambayo presha imeanza kupanda kila upande ukiwa macho kuhakikisha unashinda mchezo huo.


Kwa upande wa Wekundu wa Msimbazi, waliweka kambi maalumu ya siku 10, Polokwane nchini Afrika Kusini, kujiandaa na mechi hiyo.

Pia, kikosi hicho kilipata nafasi ya kucheza mechi mbili za kirafiki, huku ikipoteza michezo hiyo.

Tayari timu hiyo imerejea nchini na vigogo wa timu hiyo wamekuwa makini sana kuhakikisha wachezaji wao wanapata utulivu wa kutosha kuelekea pambano hilo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally alisema, Simba wanautazama mchezo huo kwa jicho pana la kuhakikisha wanapata ushindi.

Ahmed alisema kitendo cha kuwapeleka kambi Afrika Kusini, kinatuma ujumbe kwao kwamba wanautaka mchezo wa Oktoba 10 kushinda na mechi zingine zinazofuata za ligi hiyo.

“Wachezaji wote wapo vizuri baada ya kurejea na mwalimu hakutaka kuwapumzisha kwani wameanza kambi ya nyumbani kuelekea katika mchezo huo muhimu,”alisema.

Ahmed  alifafanua kuwa viongozi wote wa klabu hiyo, wanautazamia mchezo huo wa macho matatu kwani wanataka kuendelea kupata ushindi kwa mechi ya saba mfululizo katika ligi hiyo na kufuta uteja mbele ya watani zao wa jadi,Yanga.

“Wachezaji wote wapo fiti, kambi ya Afrika Kusini imetusaidia kwa kiasi kikubwa, hivyo kila mchezaji anautaka huo mchezo na nina imani kubwa kuwa tutapata ushindi na kujizoelea pointi tatu muhimu,” alisema.

Meneja huyo aliongeza kuwa wachezaji wao, wanautazama kwa jicho jingine la kuwafunga watani wao wa jadi ili kuwapa raha mashabiki wa Simba.

Hata hivyo, Ahmed alisema  mechi ya Simba na Yanga ni mechi ya maamuzi kwani inaenda kutoa picha halisi na kujiridhisha ya kuwa usajili uliofanyika ni bora.

“Kucheza na Yanga ni kipimo halisi cha kuona ni jinsi gani usajili tulioufanya na maandalizi tulioyoyafanya hivyo tunawaomba mashabiki na wapenzi wa Simba kujaa kwa wingi uwanjani ili kuipa sapoti timu yao na kufanya vizuri,” alisema Ahmed.

Simba na Yanga zilikutana mara ya mwisho katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo uliopo Mbweni, Dar es Salaam, Mei 3, mwaka huu.

Pambano hilo, lilikuwa la Ligi Kuu ya Tanzania Bara  msimu uliomalizika ambapo timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.

Previous Post

DK. HOMERA AZINDUA MIFUMO YA KUBORESHA HUDUMA ZA UMEME

Next Post

TANZANIA U-23 BAHATI MBAYA

Next Post
TANZANIA U-23 BAHATI MBAYA

TANZANIA U-23 BAHATI MBAYA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MAREKANI YAKOSHWA KASI MAENDELEO Z’BAR

MAREKANI YAKOSHWA KASI MAENDELEO Z’BAR

7 months ago
VIONGOZI WA AFRIKA NA UFARANSA WAJADILI UWEKEZAJI NA MAENDELEO

VIONGOZI WA AFRIKA NA UFARANSA WAJADILI UWEKEZAJI NA MAENDELEO

5 months ago

Popular News

  • WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BRITISH AIRWAYS KUREJEA TANZANIA, KUANZA SAFARI MEI 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA AICHIMBA YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMULIZI MKASA WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUUAWA KWA RISASI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TPA YAELEZA SIRI UTOAJI HUDUMA BORA BANDARINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?