• ePaper
Wednesday, May 13, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

VIONGOZI WA AFRIKA NA UFARANSA WAJADILI UWEKEZAJI NA MAENDELEO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 12, 2026
in Habari, Kitaifa
0
VIONGOZI WA AFRIKA NA UFARANSA WAJADILI UWEKEZAJI NA MAENDELEO
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

 Na MWANDISHI WETU


WAZIRI MKUU, Dk. Mwigulu Nchemba, ameshiriki katika ufunguzi wa Mkutano wa Ushirikiano kati ya Afrika na Ufaransa (Africa Forward: Africa–France Partnership for Innovation and Growth Summit) unaofanyika jijini Nairobi, Kenya.
 
Mkutano huo umewakutanisha Wakuu wa Nchi na Serikali, viongozi wa sekta binafsi, wadau wa maendeleo pamoja na wawekezaji kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Afrika na Ufaransa katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara, teknolojia, nishati, afya, Akili Unde (AI), kilimo, uchumi wa buluu pamoja na viwanda.
 
Akizungumza baada ya mkutano huo, Waziri Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba amesema mkutano huo umekuwa wa manufaa kwa Bara la Afrika na Ufaransa kwa pamoja kwani majadiliano yamegusa namna ya kuzifanya pande hizo mbili ziweze kunufaika na ushirikiano huo.
 
Amesema rasilimali zinazopatikana barani Afrika zinatosheleza ikiwa zitatumika vizuri katika kujenga uchumi wa Afrika.
 
“Lengo kubwa la jitihada hizi ni kupambana na umasikini lakini pia na kutengeneza ajira kwa makundi makubwa ikiwemo la vijana pamoja na wanawake,” amesema.
 
Akizungumza katika mkutano huo, Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa Dkt. William Samoei Ruto, alizitaka nchi za Afrika kutafakari upya mifumo ya kiuchumi kwa kuimarisha ukusanyaji wa rasilimali za ndani, uwekezaji pamoja na ushirikiano wa kikanda ili kuhakikisha kunakuwa na maendeleo ya muda mrefu.
 
Kwa upande wake, Rais wa Jamhuri ya Ufaransa, Emmanuel Macron, amesema Bara la Afrika linapiga hatua kubwa za maendeleo na ni bara ambalo halisubiri majawabu ya changamoto bali linatoa majawabu ya changamoto mbalimbali lilazokabiliana nazo.
 
“Hatuko hapa tu kuja kuwekeza katika Bara la Afrika pamoja nanyi, tunawahitaji viongozi wakubwa wa biashara wa Afrika kuja kuwekeza nchini Ufaransa,” alisema.

Previous Post

CG MWENDA ASISITIZA USALAMA, BIASHARA NA MAPATO KATIKA MKUTANO WA WCO ESA

Next Post

MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA AFYA

Next Post
MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA AFYA

MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA AFYA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA : UTAKUWA UCHAGUZI WA AMANI

DK. SAMIA : UTAKUWA UCHAGUZI WA AMANI

8 months ago
DK. SAMIA ASEMA MIAKA MITANO IJAYO, SERIKALI ITAENDELEA KUIMARISHA MASLAHI YAO

DK. SAMIA ASEMA MIAKA MITANO IJAYO, SERIKALI ITAENDELEA KUIMARISHA MASLAHI YAO

7 months ago

Popular News

  • BEHEWA LA AFYA LAIBUA WADAU

    BEHEWA LA AFYA LAIBUA WADAU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • IDADI WAGONJWA AFYA YA AKILI TISHIO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BALOZI DK. BASHIRU AONGOZA JUMUIKO LA KADEFO AKITAJA JITIHADA ZA RAIS DK. SAMIA KUENDELEZA KAGERA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TPA YATANGAZA KUPUNGUZA TOZO YA UENDESHAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • POINTI UBINGWA YANGA SC KUSAKWA LEO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?