• ePaper
Friday, October 9, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DK. HOMERA AZINDUA MIFUMO YA KUBORESHA HUDUMA ZA UMEME

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 6, 2026
in Habari, Kitaifa
0
DK. HOMERA AZINDUA MIFUMO YA KUBORESHA HUDUMA ZA UMEME
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nishati, Dk. Juma Zuberi Homera, amezindua mifumo mipya ya kuhudumia wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) pamoja na Mkataba wa Huduma kwa Wateja ulioboreshwa, ikiwa ni hatua inayolenga kuhakikisha wateja wakubwa na wadogo wa Shirika hilo wanapata huduma kwa haraka na urahisi.

Akizindua mifumo hiyo jijini Dar es Salaam tarehe 6 Oktoba 2026, Dkt. Homera amesema TANESCO imeonesha dhamira ya kupiga hatua zaidi katika kuboresha huduma kwa wateja, akieleza kuwa hatua hiyo ina umuhimu mkubwa katika maslahi ya Taifa, hususan katika utekelezaji wa Dira 2050 na maono ya Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan, ya kuhakikisha taasisi zinatumia ubunifu na teknolojia katika kuboresha huduma kwa wananchi.

Mifumo aliyoizindua ni pamoja na ‘Twiga Assistant’ suluhisho la kisasa linalotumia akili mnemba (AI) na kumwezesha mteja kupata huduma saa 24 kwa siku bila kulazimika kupiga simu TANESCO na  ‘Twiga Premium Portal’ jukwaa maalum la kidijitali litakalowawezesha wateja wakubwa kupata huduma mbalimbali kwa urahisi zaidi.

Aidha, Dk. Homera amezindua namba maalum 185 kwa ajili ya wateja wakubwa, itakayowawezesha kupata huduma za haraka, za moja kwa moja na zenye kipaumbele pamoja na uzinduzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Wakubwa ili kuhakikisha kundi hilo linapata huduma zinazokidhi mahitaji yake.

Pamoja na kuipongeza TANESCO kwa ubunifu huo uliofanywa na wataalamu wa ndani, Dkt. Homera amelitaka Shirika hilo kuhakikisha Mkataba wa Huduma kwa Wateja unatekelezwa kwa vitendo katika ngazi zote na ahadi zilizomo ndani yake zinakuwa sehemu ya utamaduni wa kazi wa kila mtumishi. Pia, amesisitiza mifumo yote iliyozinduliwa ifanye kazi kwa ufanisi muda wote na itumike kwa vitendo ili kuleta matokeo yaliyokusudiwa kwa wananchi.

Vilevile, ameelekeza TANESCO kutoa elimu ya kutosha kwa makundi yote ya wateja kuhusu mifumo hiyo na namna ya kuitumia kupata huduma na kutatua changamoto mbalimbali.

Ameitaka pia TANESCO kuongeza matumizi ya takwimu na maoni ya wateja katika kufanya maamuzi, huku kila lalamiko la mteja likitumika kama fursa ya kuboresha huduma.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kulinda taarifa za wateja na mifumo ya kidijitali kwa kuzingatia sheria na viwango vya usalama wa taarifa, sambamba na kukiwezesha kikamilifu Kitengo cha Huduma kwa Wateja Wakubwa kutoa huduma bora na kwa wakati.

Katika hatua nyingine, Dkt. Homera amesema uwekezaji unaofanywa na Serikali katika Sekta ya Nishati umeendelea kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini, ambapo uwezo wa kuzalisha umeme umefikia MW 4,606, sawa na ongezeko la asilimia 21.32, huku mahitaji ya juu ya umeme yakifikia MW 2,316, ikiwa ni ongezeko la asilimia 12.97 ikilinganishwa na mwaka 2025.

Amesema ongezeko hilo la mahitaji ya umeme linaenda sambamba na kuongezeka kwa idadi ya wateja wanaohitaji kuhudumiwa, hivyo mifumo hiyo mipya itachangia utekelezaji wa malengo ya Serikali, ikiwemo Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayotambua nishati kuwa kichocheo muhimu cha ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nchi.

Katika hafla hiyo, Dk. Homera amesisitiza utekelezaji wa maelekezo ya Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha Tanzania inafikia uwezo wa kuzalisha megawati 8,000 ifikapo mwaka 2030 akieleza kuwa lengo hilo linawezekana kutokana na Wizara na taasisi zake, ikiwemo TANESCO, kuwa na wataalamu wanaofanya kazi kwa weledi, sambamba na kuendelea kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme, ukiwemo Mradi wa Umeme wa Jua wa Kishapu ambao awamu yake ya pili inahusisha  MW 100

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi Asilia, Dkt. James Mataragio, amesema huduma zilizozinduliwa, zikiwemo Twiga AI Chatbot, Twiga Premium Customer Portal, Premium Customers Toll Free Line, Premium Customer Service Section  pamoja na Mkataba wa Huduma kwa Wateja ulioboreshwa, zinaendana na dhamira ya Serikali ya kuhakikisha kuwa pamoja na kuimarisha upatikanaji wa umeme nchini, huduma zinazotolewa kwa wananchi zinaendelea kuboreshwa kupitia teknolojia, ubunifu na mifumo ya kisasa.

Previous Post

NDEJEMBI ATOA MSISITIZO TEKNOLOJIA KATIKA UKUSANYAJI KODI

Next Post

VIGOGO SIMBA MACHO KILA KONA

Next Post
VIGOGO SIMBA MACHO KILA KONA

VIGOGO SIMBA MACHO KILA KONA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. NCHIMBI AAHIDI USHIRIKIANO WA KINA JUMUIYA YA KIMATAIFA

DK. NCHIMBI AAHIDI USHIRIKIANO WA KINA JUMUIYA YA KIMATAIFA

2 months ago
JK AMWOMBEA KURA DK. SAMIA

JK AMWOMBEA KURA DK. SAMIA

1 year ago

Popular News

  • WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BRITISH AIRWAYS KUREJEA TANZANIA, KUANZA SAFARI MEI 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA AICHIMBA YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMULIZI MKASA WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUUAWA KWA RISASI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TPA YAELEZA SIRI UTOAJI HUDUMA BORA BANDARINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?