• ePaper
Friday, October 9, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

NDEJEMBI ATOA MSISITIZO TEKNOLOJIA KATIKA UKUSANYAJI KODI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 6, 2026
in Habari, Kitaifa
0
NDEJEMBI ATOA MSISITIZO TEKNOLOJIA KATIKA UKUSANYAJI KODI
0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

MAKAMU wa Rais Deogratius Ndejembi amesema matumizi ya mifumo ya kisasa ya teknolojia ni chachu katika ukusanyaji wa kodi hivyo yanapaswa kutiliwa mkazo ili kuongeza uwazi, kuimarisha usimamizi wa kodi na kurahisisha ulipaji kodi.

Makamu wa Rais ameyasema hayo jijini Arusha Oktoba 06, 2026 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa wa Chama cha Wasimamizi wa Kodi wa Jumuiya ya Madola (CATA) na kueleza kuwa  teknolojia ni nyenzo muhimu katika kuboresha ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuimarisha huduma kwa walipa kodi ndiyo maana mkutano huo umekuja na kauli mbiu inayogusa teknolojia.

Amesema pamoja na umuhimu wa teknolojia, mafanikio katika ukusanyaji wa mapato hayawezi kutegemea teknolojia pekee, bali yanahitaji sera nzuri, madhubuti, zinazoeleweka na zinazotabirika, pamoja na usimamizi wa kodi wenye ufanisi na unaokidhi mahitaji ya walipakodi.

Makamu wa Rais pia amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika masuala ya kodi, akibainisha kuwa biashara zinazovuka mipaka, makampuni ya kimataifa, miamala ya kidijitali pamoja na mali za kifedha zinazohifadhiwa nje ya nchi zimefanya ushirikiano kati ya mamlaka za kodi kuwa muhimu zaidi.

Amesema Tanzania inaendelea kuimarisha ushiriki wake katika ushirikiano wa kimataifa wa kodi, ikiwemo kubadilishana taarifa za kodi na kutoa msaada wa kiutawala baina ya nchi huku akieleza kuwa ushirikiano huo ni muhimu katika kuongeza uhakika wa kodi, kubadilishana taarifa, kuzuia na kutatua migogoro ya kikodi.

Amesema uratibu mzuri kati ya nchi unaweza kusaidia kulinda mapato ya Serikali huku ukipunguza uwezekano wa kutozwa kodi mara mbili na kuondoa sintofahamu kwa wawekezaji halali.

“Nchi inayovutia uwekezaji siyo ile isiyokuwa na kodi, bali ni ile yenye kanuni za kodi zilizo wazi, thabiti na zinazosimamiwa kwa haki, zikiungwa mkono na taratibu bora za forodha na ukusanyaji wa mapato,” amesema.

Awali akizungumza katika mkutano huo Rais wa CATA Mhe. Abu Tariq Jamaluddin amesema matumizi ya teknolojia ya kisasa yamekuwa yakisaidia nchi wanachama wa CATA kurahisisha utawala wa kodi kwa kuweka mazingira rahisi ya ukusanyaji wa mapato na kuwasaidia walipakodi kufuata sheria za kodi.

Amesema kauli mbiu ya mkutano huo inalenga kuhimiza matumizi zaidi ya teknolojia na kueleza kuwa CATA itaendelea kuwezesha matumizi ya teknolojia katika ukusanyaji wa kodi ili kuimarisha usimamizi wa kodi baina ya nchi wanachama.

Amesema kupitia mkutano huo nchi washiriki wataweza kubadilishana ujuzi na uzoefu kuhusu usimamizi   wa kodi na matumizi ya teknolojia.

Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao ndiyo waandaaji wa mkutano huo Bw. Yusuph Juma Mwenda amesema Mamlaka hiyo imepiga hatua kubwa katika matumizi ya teknolojia ambayo yameboresha zaidi huduma za usimamizi wa kodi kwa kuongeza uwazi na ufanisi.

Amesema kupitia matumizi ya teknolojia TRA imekuja na mfumo wa IDRAS unaosimamia kodi za ndani ambao unamuwezesha Mlipakodi kutoa risiti za kielektroniki kwa kutumia simu ya mkononi bila kuwa na mashine hali ambayo imeongeza uhiari katika kulipa kodi na kupunguza kuonana kwa walipakodi na maofisa wa TRA.

Amesema kupitia mkutano huo wataweza kubadilishana ujuzi na mataifa mengine akieleza kuwa matumizi ya teknolojia ya kisasa pia kwa Tanzania yameongeza wigo wa kodi kutokana na kuwapa uhuru walipakodi kujisajili kupitia mtandao na kupata namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN).

Previous Post

RAIS DK. SAMIA AHIMIZA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UMMA KATIKA MKUTANO WA IPU

Next Post

DK. HOMERA AZINDUA MIFUMO YA KUBORESHA HUDUMA ZA UMEME

Next Post
DK. HOMERA AZINDUA MIFUMO YA KUBORESHA HUDUMA ZA UMEME

DK. HOMERA AZINDUA MIFUMO YA KUBORESHA HUDUMA ZA UMEME

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

KIPA CAMARA APASULIWA GOTI

KIPA CAMARA APASULIWA GOTI

11 months ago
MASTAA YANGA WAUTAJA UBINGWA LIGI KUU BARA

MASTAA YANGA WAUTAJA UBINGWA LIGI KUU BARA

4 months ago

Popular News

  • WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BRITISH AIRWAYS KUREJEA TANZANIA, KUANZA SAFARI MEI 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA AICHIMBA YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMULIZI MKASA WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUUAWA KWA RISASI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TPA YAELEZA SIRI UTOAJI HUDUMA BORA BANDARINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?